Hivi kuna maelezo yeyote ya kitaalamu yaliyotolewa na mamlaka husika juu ya changamoto ya mtandao

100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
4,155
14,010
Ni takribani siku kadhaa sasa tangu internet nchini imekuwa na changamoto.

Hadi sasa tunachofahamishwa ni kwamba kuna nyaya huko baharini zimeleta hitilafu, hilo ndilo kila mmoja nchini utasikia akisema, sasa najiuliza na huu mtandao ulivyo chini ina maana kuna nyaya zilibaki ndizo zinaleta mtandao huu hafifu? Au tumekodi satellite kama backup kwa muda.

Hao wataalamu wa IT huko TCRA na mamlaka husika hawana uwezo kufanya press conference na vyombo vya habari kuelezea wananchi kwa kina au kutoa elimu mwanzo mwisho kuhusu jambo lililotokea na mfumo mzima wa huo mkonga unavyofanya kazi, je umeleta hasara ipi? Je kuna ulazima wa kuwa na back up kwa wakati ujao? Ilishawahi kutokea mara ngapi? Mitandao ya simu itafidia gharama za watumiaji walioathirika na hili tatizo? Kuna mengi ya kuelezea tena kwa maelezo ya kitaalamu ili wananchi waelewe. Au na hao IT na wao ni weupe vichwani kutoa maelezo, au pengine wateja au wananchi hawapaswi kuwa na uelewa wa kinachoendelea? Kingine serikali iangalie mawaziri wenye uelewa mkubwa kuhusiana na wizara husika.

Hili suala limeathiri shughuli za wengi, kuna vijana wana hizi online TVs, kuna vijana wana trade stocks n.k kwa kifupi internet imesaidia wananchi wengi kujiajiri kuna watu internet ndio maisha yao, lakini kwa jinsi mamlaka zinavyochukulia hili suala ni kama jambo la kawaida tu. Suala la mtandao ni issue serious. Kushirikiana na wananchi kunaweza pelekea utatuzi wa tatizo hili kwa siku zijazo.

Ukimuuliza mtu mbona mtandao upo chini utasikia kuna nyaya huko baharini zina hitilafu. Hizo nyaya zenyewe hajui hata zinafanana vipi. Ukimuuliza hitilafu imesababishwa na nini hapo jibu hana.

Wanasiasa na mamlaka husika nyie mmeajiriwa na wananchi lazima kuhakikisha wananchi wanapata updates kwa kila kinachoendelea kwa maelezo ya kitaalamu yasiyoleta shaka, vijana sasa wamesoma wana uelewa mkubwa kuhusu ulimwengu huu wa kidijitali.

Katika kituko cha karne ni pale kuna shida ya internet halafu mamlaka husika zinakwenda kutoa taarifa mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii, sasa hao wananchi wanapata vipi taarifa?

Hii nchi tuna safari ndefu.
 
Ni takribani siku kadhaa sasa tangu internet nchini imekuwa na changamoto.

Hadi sasa tunachofahamishwa ni kwamba kuna nyaya huko baharini zimeleta hitilafu, hilo ndilo kila mmoja nchini utasikia akisema, sasa najiuliza na huu mtandao ulivyo chini ina maana kuna nyaya zilibaki ndizo zinaleta mtandao huu hafifu? Au tumekodi satellite kama backup kwa muda.

Hao wataalamu wa IT huko TCRA na mamlaka husika hawana uwezo kufanya press conference na vyombo vya habari kuelezea wananchi kwa kina au kutoa elimu mwanzo mwisho kuhusu jambo lililotokea na mfumo mzima wa huo mkonga unavyofanya kazi, je umeleta hasara ipi? Je kuna ulazima wa kuwa na back up kwa wakati ujao? Ilishawahi kutokea mara ngapi? Mitandao ya simu itafidia gharama za watumiaji walioathirika na hili tatizo? Kuna mengi ya kuelezea tena kwa maelezo ya kitaalamu ili wananchi waelewe. Au na hao IT na wao ni weupe vichwani kutoa maelezo, au pengine wateja au wananchi hawapaswi kuwa na uelewa wa kinachoendelea? Kingine serikali iangalie mawaziri wenye uelewa mkubwa kuhusiana na wizara husika.

Hili suala limeathiri shughuli za wengi, kuna vijana wana hizi online TVs, kuna vijana wana trade stocks n.k kwa kifupi internet imesaidia wananchi wengi kujiajiri kuna watu internet ndio maisha yao, lakini kwa jinsi mamlaka zinavyochukulia hili suala ni kama jambo la kawaida tu. Suala la mtandao ni issue serious.

Ukimuuliza mtu mbona mtandao upo chini utasikia kuna nyaya huko baharini zina hitilafu. Hizo nyaya zenyewe hajui hata zinafanana vipi. Ukimuuliza hitilafu imesababishwa na nini hapo jibu hana.

Hii nchi tuna safari ndefu.
Mkuu,

Nakuelewa sana maumivu yako. Pole sana.

Ni jambo moja kuwa na tatizo kama hili, ni jambo tofauti kuwa na tatizo halafu hakuna hata updates.

Miezi michache iliyopita kuna meli iligonga nguzo ya daraja mjini Baltimore, Maryland USA. Daraja likaanguka. NIkawa naangalia wale viongozi kuanzia meya mpaka gavana wanavyoitisha press conferences kuwajulisha watu nini kimetokea, maendeleo, njia mbadala za kutumia, na hata pale ambapo walikuwa hawana majibu walikuwa wanasema kwa sasa ni mapema mno hatuna majibu, tunafanyia kazi, tutawajulisha tena maendeleo baada ya muda fulani.

Nilivyowaona wanafanya vile nikafikiria sana Tanzania na kusema tunaweza kujifunza mengi kwenye Disaster Management kutoka kwao.

Huku kwetu Nape akisha tweet ki vague tweet tu ndiyo imetoka hiyo.
 
Inasikitisha sana. Najiuliza sana wanatufanyia hivyo.
Ni kiburi.

Sijui ni kujisahau majukumu wanayopaswa kufanya.

Au ndio ile vijana tunasema kuchukuliana poa/kutokujali.

Ama ni dharau, kwamba hawa tunawamudu na hawatofanya lolote.

Usemavyo ni kweli, hata kama jibu hawana waseme jibu hatuna.

Ni nchi nzuri lakini ni watu wachache inapelekea nchi inakuwa kama shimo la choo.
 
Kenya wamerudisha Kwa asilimia 100%
Sasa hapo ndio utajua Technology haitaji bwebwe na maneno mengi sio kazi za kupeana Kwa connection..
Tuna waziri mzigo anatia hasara Sana
Hana uelewa wowote kuhusu field ya IT.
 
Sisi Hatuna Hayo Maelezo, Hebu Tusaidie Wewe Mkuu Uliesikia, Si Vibaya Uka Share Hapa
Screenshot_20240514-203634_X.jpg
 
Kenya wamerudisha Kwa asilimia 100%
Sasa hapo ndio utajua Technology haitaji bwebwe na maneno mengi sio kazi za kupeana Kwa connection..
Tuna waziri mzigo anatia hasara Sana
Hapo anatakiwa waziri aliye na maarifa ya teknolojia na habari.Haya ni maeneo technical sana.
 
Ni takribani siku kadhaa sasa tangu internet nchini imekuwa na changamoto.

Hadi sasa tunachofahamishwa ni kwamba kuna nyaya huko baharini zimeleta hitilafu, hilo ndilo kila mmoja nchini utasikia akisema, sasa najiuliza na huu mtandao ulivyo chini ina maana kuna nyaya zilibaki ndizo zinaleta mtandao huu hafifu? Au tumekodi satellite kama backup kwa muda.

Hao wataalamu wa IT huko TCRA na mamlaka husika hawana uwezo kufanya press conference na vyombo vya habari kuelezea wananchi kwa kina au kutoa elimu mwanzo mwisho kuhusu jambo lililotokea na mfumo mzima wa huo mkonga unavyofanya kazi, je umeleta hasara ipi? Je kuna ulazima wa kuwa na back up kwa wakati ujao? Ilishawahi kutokea mara ngapi? Mitandao ya simu itafidia gharama za watumiaji walioathirika na hili tatizo? Kuna mengi ya kuelezea tena kwa maelezo ya kitaalamu ili wananchi waelewe. Au na hao IT na wao ni weupe vichwani kutoa maelezo, au pengine wateja au wananchi hawapaswi kuwa na uelewa wa kinachoendelea? Kingine serikali iangalie mawaziri wenye uelewa mkubwa kuhusiana na wizara husika.

Hili suala limeathiri shughuli za wengi, kuna vijana wana hizi online TVs, kuna vijana wana trade stocks n.k kwa kifupi internet imesaidia wananchi wengi kujiajiri kuna watu internet ndio maisha yao, lakini kwa jinsi mamlaka zinavyochukulia hili suala ni kama jambo la kawaida tu. Suala la mtandao ni issue serious. Kushirikiana na wananchi kunaweza pelekea utatuzi wa tatizo hili kwa siku zijazo.

Ukimuuliza mtu mbona mtandao upo chini utasikia kuna nyaya huko baharini zina hitilafu. Hizo nyaya zenyewe hajui hata zinafanana vipi. Ukimuuliza hitilafu imesababishwa na nini hapo jibu hana.

Wanasiasa na mamlaka husika nyie mmeajiriwa na wananchi lazima kuhakikisha wananchi wanapata updates kwa kila kinachoendelea kwa maelezo ya kitaalamu yasiyoleta shaka, vijana sasa wamesoma wana uelewa mkubwa kuhusu ulimwengu huu wa kidijitali.

Hii nchi tuna safari ndefu.
Comments reserved
 
Kuna jamaa hapa nimewasimulia wananijibu ACHANA NA VIJANA WA CHADEMA WANAPENDA ULALAMISHI😊

sijui which is which
 
Mi ndo nimejuwa wiiki hii kwamba tunatumia cable zinazopita baharini
Kila siku tunajifunza kitu kipya.

Jana nilikuwa namwambia rafiki yangu mmoja, yeye alikuwa anataka Watanzania wachukue ownership ya internet na kuwa activists zaidi, nikamwambia wengi hawaelewi internet inavyofanya kazi, nikamwambia kuwa Watanzania wengi wanatumia internet kama uchawi tu.
 
Haya maelezo wametoa jana, je we unaona hayo maelezo yanajitosheleza?
Labda nikuulize hio link nyingine wanayotumia tunapata internet yenye speed hafifu kwa maelezo yao ni ipi? Ni satellite ama nyaya zingine?
Pdf lenyewe la kiingereza, kwa nini wasitoe maelezo yaliyonyooka kwenye vyombo vya habari vinavyoeleweka? Au wanaogopa maswali?
 
Back
Top Bottom