Hivi kumbe wanawake mnatuchukulia hivi! Da... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kumbe wanawake mnatuchukulia hivi! Da...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tuko, Jun 6, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hii inatokana na kipindi cha 'Habari ndiyo hiyo' cha TBC1 jana.
  Topic ilikuwa "wanaume wa cku hizi"
  Sijui mwandaaji wa kipindi aliwaza nini kuleta topic hii (ni mwanaume) ila almost wanawake wote aliowahoji alianza swali la kwanza ...unawachukuliaje wanaume wa siku hizi?...

  Majibu ya wanawake sasa... Du!

  Wa kwanza ...Hawaeleweki, ni waongo, wanatuhadaa...
  Wa pili ...wanapenda kulelewa, ni waongo....
  Wa tatu ...ni waongo, hawaaminiki...


  Kipindi kiliendelea na kati ya wanawake zaidi ya saba waliohojiwa, isipokuwa mmoja, wengine walionyesha kuwa wanaume wa siku hizi ni waongo, hawaaminiki, wanapenda kulelewa. Cha kusikitisha ni kuwa majibu haya yalitoka kwa wanawake wa rika tofauti, waliwepo wadada waliwili ambao kimwonekano walikuwa na miaka kumi+ au early twenties!!! Ni mmoja tu alisema kuwa ni watulivu, wana upendo akitolea mfano mchumba wake.

  Hivi kinadada, kwanini hatuaminiani hivyo jamani??!
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwasababu hamuaminiki!!

  Sio wote...baadhi yenu msio na mshipa wa aibu wala huruma.Hao wote waliojibu naamini wamejibu kutokana na experience...badilikeni mpendwe mpaka mchukie!
   
 3. W

  WONDERWOMAN Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  mnatutenda kila kukichaaaaaaaaa
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Na wanawake wa siku hizi nao wakoje? Au wao ni malaika na siku zote ni wema, waadilifu, waaminifu, wakweli, wenye heshima, na wenye mapenzi ya kweli?
   
 5. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0

  WE unasemaje?unaonaje?
  wamesingiziwa?
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Wanawake banaa utafikiri wao huwa ni Malaika
   
 7. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  women are angels,
  angels from heaven others angels from hell.
   
 8. L

  LADY M Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yap. nimeipenda hiyo. kwa mtazamo wangu, sio wanaume wote wakwel. kat ya percent 100 percent 10 ndiyo waaminifu. but frankly 90 percent ni wanafiki, waongo, na co waaminifu. tena wengne bila mshpa wa aibu wanakwambia washana mko weng. so inabd mwanaume mmoko awe na wanawake zaid ya wanne! jaman jaman tumwogope MUNGU vinginevyo Ukimwi na magonjwa mengne nyemelezi hayataisha ng"o!
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Umeshakula lunch!??Usiwe na hasira bwana mada inahisu wanaume acha wanawake waponde...next week zamu yetu kusemwa..ntakununulia muda wa dakika 15 hewani useme yote yakukerayo!!
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Toka lini unajali kama nimekula au la? Jana tu umetoka kuninyima ulichopika....mwanamke una roho mbaya wewe.....
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Najali bwana...hapa tu nimekupikia ugali mgumuuuuu na mchuzi wa samaki pia mchicha pembeni!!
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Haabaaa haabaa haabaaa.....kumbe unayajua fika mahitaji ya Nzagamba wa Ikungulyabashashi. Obeja gete nkima one.
   
 13. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Sina hakika Rose, maana mi ni mwanaume, so siwezi kujijaji...

  Hata hivyo majibu ya wanawake yalinishangaza, nikajiuliza hivi angehojiwa mke wangu angejibuje?!
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Sina uhakika kama umeolewa au una Mchumba/Boyfriend, ila naomba nikuulize kama unaye, je ungeulizwa leo unawachukuliaje wanaume wa siku hizi, na ukatoa jibu kwa reference ya uliye naye au uliyewahi kuwa naye, unadhani jibu utakalotoa ndilo analodhania utatoa? I mean hatashangaa?
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Obeja gete nkima one.....???!Embu nitafsirie wakati nakumiminia mtindi kwenye glass!!
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ashangae nini...kwani hua hamjijui kama ni WAZURI au WABAYA??!Sidhani kama kuna mtu kipofu kiasi cha kutojijua yeye ni mtu wa aina gani!!
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hebu harakisha kumimina huo mtindi bana. Nna njaa mimi….mambo ya tafsiri baadae nkishashiba. Kwanza natoza ushuru kwa huduma za kutafsiri.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ushuru tena?!Mbona mi sijalipwa kupika??!
  Nwy nakubembeza...nitafsirie basiNyaniizzo...pleaeeeeeese!!
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Njoo hapa chemba nikwambie.
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  We ninong‘oneze tu bwana.....
   
Loading...