Hivi kumbe mahari zinafika milioni 7? Wazazi kuna muda mwengine ni chanzo cha watoto kutoolewa au kufosiwa ndoa kwa watu wasiowapenda

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,455
kijana ana miaka 28 yupo normal kiuchumi ana shughuli zake, kapata mchumba mwenye 23, wanapendana perfect match, kufika kwao kupeleka posa wazazi wanahitaji MILIONI 7

wazazi kuna muda mwengine ni chanzo cha watoto kuto olewa au kufosiwa ndoa kwa watu wasiowapenda
 
Inategemea na aina ya familia na aina ya mwanamke, status yake ikoje, status ya familia ya wazazi wake ikoje. Milion 7 ndogo kama anatoka familia yenye kipato pia huyo binti pia inategemea naye yupo kwenye level zipi.
 
Ndo

Mzazi mwenye akili hata kama ni Tajiri, na anayejua shida za ndoa, hawezi chukua mahali kubwa..Unaangalia mama yake, unaona shida atakazokutana nazo kijana..unatamani kumpa bure kikubwa amvumilie huko kwenye ndoa
 
kijana ana miaka 28 yupo normal kiuchumi ana shughuli zake, kapata mchumba mwenye 23, wanapendana perfect match, kufika kwao kupeleka posa wazazi wanahitaji MILIONI 7

wazazi kuna muda mwengine ni chanzo cha watoto kuto olewa au kufosiwa ndoa kwa watu wasiowapenda
kuna mkoa wa Kagera kwenye mahari ujipange.
 
Ndo

Mzazi mwenye akili hata kama ni Tajiri, na anayejua shida za ndoa, hawezi chukua mahali kubwa..Unaangalia mama yake, unaona shida atakazokutana nazo kijana..unatamani kumpa bure kikubwa amvumilie huko kwenye ndoa
Acha kutia huruma unataka k ya bure Kila siku halafu unatia huruma Mimi mwanangu humchukui chini ya million 10 hutaki lala mbele unajua nimetumia ghara gani tangia namshawishi mama yake mimba ikatungwa akazaliwa akakua mpaka unamuona halafu uje ubebe tu kirahisi
 
kijana ana miaka 28 yupo normal kiuchumi ana shughuli zake, kapata mchumba mwenye 23, wanapendana perfect match, kufika kwao kupeleka posa wazazi wanahitaji MILIONI 7

wazazi kuna muda mwengine ni chanzo cha watoto kuto olewa au kufosiwa ndoa kwa watu wasiowapenda
Spend as you earn..
Unaombwa mahari sawa na uwezo wako...
Hivi Kwa mfano boda anaweza ombwa mahari hiyo...
Vipi Je Bakhresas' ,si hata milioni 100
 
Sitoi mahari itakayozidi million.

Suala la kuniambia kumlisha sjui shule hayo ni mahitaji yake na ilikuwa ni wajibu wako kwake kama mzazi

Vipi asipoolewa hizo fidia utapata wapi ??

wazazi wengi huweka njaa ya mahari kubwa na sio kuwatakia khery wanae hao...

MAHARI HAITAZIDI ONE MIO NA NITAKUWA KWENYE HICHO KIKAO KUMSKILIZA BABA MKWE.
 
Acha kutia huruma unataka k ya bure Kila siku halafu unatia huruma Mimi mwanangu humchukui chini ya million 10 hutaki lala mbele unajua nimetumia gharamagani tangia namshawishi mama yake mimba ikatungwa akazaliwa akakua mpaka unamuona halafu uje ubebe tu kirahisi
Unajitafutia matatizo tu, kwanza Mahari hua hailipwi yote na Mahari ikilipwa Nusu hua haina deni kwamba utanishika shati nimalize Mahari, sababu ni kwanini inakua hivyo ili kukitokea lolote unakua free kumpokea mwanao na kuniita tukae chini tuyazungumze, sasa nikikukatia 10M yote kikitokea chochote nisikae nikasikia mtoto wako karudi nyumbani kwako na umempokea na ukaweka ngumu asirudi kwangu, oya Mzee unajitafutia matatizo na usichojua wanaofanya hivyo wengi ndio yanatokea km hayo yanayotokea unanikazia Mahari 10M nakwambia Mzee shika kwanza 5M hio 5M nyingine nakutafutia ila nichukue Mwali kwanza akazae wajukuu wako unanikazia, nasema fine nakukamatisha 10M yote ila hakikisha unamwambia mwanao kabisa kwamba likitokea lolote la kutokea asikimbilie kwako maana utakua umeshamuuza mazima na hauna mamlaka nae tena, umenielewa?
 
Uislamu pekee ndio suluhisho la changamoto nyingi katika maisha,huwa watu wanabeza katika mahari ndogo na blablabla kibao,Uislamu unataka mahari ziwe nyepesi vijana wasikwame kwenye kuoa na kuepuka zinaa

Sasa nyie hao hao ambao mnabeza kuwa ndoa za kiislamu ni cheap,now mpo hapa kulialia kuwa mahari ni ghali mno

Hamjui ndoa sio biashara kwamba wazazi waingize faida
 
kijana ana miaka 28 yupo normal kiuchumi ana shughuli zake, kapata mchumba mwenye 23, wanapendana perfect match, kufika kwao kupeleka posa wazazi wanahitaji MILIONI 7

wazazi kuna muda mwengine ni chanzo cha watoto kuto olewa au kufosiwa ndoa kwa watu wasiowapenda
wazazi wengin, wanazingua yan unakuta wanataka kwa lazima utafkiri walikopesha wakwe.
 
Back
Top Bottom