Hivi kumbe kuna wanaume hutumia mapenzi ya dawa?

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
7,505
25,118
Hello guys,
Nakumbuka tukiwa O-level mwishoni, kulikuwa kuna couple moja bomba kabisa ambayo kwa akili za kipindi kile kiukweli tulikuwa tunaitamani,
Maana ilikuwa na show-off inayobamba hasa, kufuatana ilikuwa ni mwendo wa kumbikumbi, lunch time kulishana ni kawaida uzuri by the time tulikuwa kwa ile point karibu na exams hata hatufuatiliwi kivile, so we were free to mingle.!

Siku na miezi ikapita, hatmae mwaka mwingine tuko duniani huko shule ishaisha by the time..! the girl alikuwa beste angu though not that much lakini kuna ile anaweza ni trust na mambo yake,
Kaja kunitembelea, Sasa boy wake kampigia akaipokea kwa heshima na taadhima I don't really remember kama Kuna siku nimewahi zungumza na mtu kwa nidhamu kiasi kikuu namna ile.!!
I didn't mind it sababu ni watu na mapenzi yao nikajiambia tu kama mahusiano yanahitaji unyenyekevu hivii then I'm doomed, maana akili zangu zenyewe mbili mbele.!!

After a while binti akaanza kunipa kesi zisizoisha, ni ugomvi na matusi kila wakikosana kitu kidogo, Nikajitia 'Mama ushauri', shauri weeeh' najenga mahusiano ya watu, yakanifika kooni sasa maana wakigombana mvua ya matusi anayomiminwa walaqhii' ni matusi mapya, atatukanwa anzia yeye mpaka wazazi wake na hapo unakuta analia maskini hadi huruma ananifowadia zile meseji, Mie tu nisiye muhusika nahisi mtetemo wa moyo.!

Yakanishinda kwakweli nikaanza tu kumuambia mama kama yamekushinda achia ngazi huyu si mwanaume wa kuwa naye hata kama mmekosana ndo mitusi hivii?? Anaapa 'namuacha this time nimechoka' siku mbili mingi kesharudi zake bwaana mie naishia kuonekana kashwetani, ila yakimshinda atanirudia tena nitamshauri the same thing, ataapa the same thing na atarudi zake tena..!! Nikamuacha nikamuambia tu usiniletee tena hizo case kwakweli.!!

Sasa last year kafunga ndoa na mwanaume mwingine kabisa,
Hatukuwa tumeonana muda sana, mpaka this year majuzi hapo baada ya kuwa kajifungua, kaongeza karembo duniani, Katika story ndo namuuliza what happened kuhusu that guy.!!

Ndo kunielezea ilivyokuwa kumbe hayakuwa matusi tu, akavua shati kunionyesha makovu ya vipigo kachakazwa hasa, Nilistaajabu sababu hii hakuwahi nambia, kuna jino kavunjwa alituambia alianguka na pikipiki ndo anakuja kunambia alipigwa, nikabaki seriously?? Boyfriend anakuchakaza hivi na upo tu huendi pahala??
Anasema alikuwa hawezi kumuacha anamchapa hata na mikanda akirudi tu anamuomba radhi anajikuta yumooo.!!

Kuna auntie yake ndo alikuwa anamsimulia hayo maswahibu, akaingilia kati akayafikisha kwa familia, kwa mujibu wake yeye wakaenda mtafutia tiba wakakuta kumbe alikuwa kafungwa na yule mwanaume..!!
Ndo kutolewa katika hiyo dhahama na kurudi katika akili zake za kawaida..!!

Nilishangazwa sababu nilijua hii tabia wanayo tu wadada looqh' na the guy alivyokuwa innocent hafananii.
'Wonders shall never cease'..!!
 
Kuna mshkaji ana familia yake na yupo katika 40s,alikua anatembea na binti wa IFM basi yule jamaa alimfunga yule binti tena alikua yupo proud na anaona kawaida inshort kuna washkaji wake wengine pia walimsupport na washawahi jaribu michezo hiyo.

Lakini mpaka leo sijapprove kama inafanya kazi maana hata huyo jamaa pesa alikua anatoa pia na kumfunga alimfunga
 
Unapata raqha gani while unajua kabisa hapa sipendwi ni hizi dawa.!
It's better uache mapenzi yazungumze yenyewe.!!
 
Kuna mshkaji ana familia yake na yupo katika 40s,alikua anatembea na binti wa IFM basi yule jamaa alimfunga yule binti tena alikua yupo proud na anaona kawaida inshort kuna washkaji wake wengine pia walimsupport na washawahi jaribu michezo hiyo.

Lakini mpaka leo sijapprove kama inafanya kazi maana hata huyo jamaa pesa alikua anatoa pia na kumfunga alimfunga
Kifungo kilikuwa ni pesa tu hapo hamna namna
 
Usikute kazusha tu kuwa alikuwa kafungwa na mwanaume ili aonekane ni victim wakat inawezekana alikuwa kapenda na mambo yote alifanyiwa akiwa na akili zake nzuri tu
Nuh' sidhani, asingekuwa na sababu ya kufanya hivyo.!!
 
Back
Top Bottom