Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,582
Nimeamua kuliandika hili jambo ili lijadiliwe na members wa hapa Jf.
Kuishi kijijini ni sababu ya kuwachukia wanaoishi mjini?
Katika familia yetu, tumezaliwa wengi na asilimia kubwa tumesambaa kwenye miji mbalimbali kikazi. Mzazi wetu alipofariki tulipeana taarifa, tukakutana mjini ili kupanga namna ya kuendesha msiba, tukasafiri kwenda kijijini kwetu kwa ajili ya kumuhifadhi mzazi wetu.
Cha kushangaza, wanakijiji walikuwa wameweka mgomo kutochimba kaburi, walikuwa wamechimba kama futi moja hivi kwenda chini eti sehemu iliyobaki inabidi tuwalipe kwa sababu huwa hatushiriki msiba pale kijijini. Kwa kuwa mimi ndo msemaji wa familia, nilipitisha mchango na badala ya kuwalipa faini wanakijiji nilitafuta mafundi wakachimba kaburi la kujengea tukawa tumefanikiwa kumuhifadhi mzazi wetu.
Si hilo tu walikuwa na vimigomo vingi hata kushindwa kutusaidia kuchota maji, jambo lililopelekea kukodi wapishi toka mjini.
Hivi tulifanyiwa hivyo kwa sababu ya kuishi mjini au kuna jingine? Msomaji naomba mchango wako kama uliwahi kukutana na hali kama hii.