Hivi kufa kwa viwanda vya umma ni kwa sababu ya vyama vingi?

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Na: Dotto Bulendu
Nimesikiliza angalau kipande cha mchango wa Ndugu George Simbachawene kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa,nilichokigundua sasa ipo hoja inapazwa kwa kasi kuwa.....

1.Kufa kwa viwanda nchini Tanzania ni sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama vingi nchini.

2.Kufa kwa Mashamba makubwa yaliyotoa ajora za kutosha ni kwa sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama Vingi nchini.

3.Uwekezaji ambao haukuwa na tija kwa taifa letu kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu Vyama vingi.

4.Tatizo la ajira nchini ambalo linakuwa siku baada ya siku limesababishwa na mfumo wa Vyama vingi nchini.

5.Kashfa kubwa za Rushwa kama EPA,Escrow,Richmond,Meremeta,Dowans n.k zilisababishwa na nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

6.Kufa kwa Shirika la Reli,Shirika la Ndege/Anga kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuanzisha mfumo wa Vyama vingi.

Ndiyo maana George Simbachawene anasema nchi kama China ina chama kimoja tu na uchumi wake sasa ni imara.

Simbachawene anatamani Tanzania tubaki na chama kimoja ili tujenge taifa lenye nguvu duniani.Sijui kwa nini George hajatumia mifano ya mataifa ambayo yameendelea na yana mfumo wa vyama Vingi?

George Simbachawene ambaye kama sikosei aliondoshwa kwenye Wizara ya Madini na Mh Rais kutokana na kutuhumiwa na Kamati ya Mh Rais ile ya Makanikia,anasema huko nyuma nchi ilikuwa kwenye presha muda wote na akataja harakati kama..

1.Movement for Change
2.Oparesheni Sangara n.k

Kwa mtazamo wa Ndugu Simbachawene,harakati hizi zilichangia kuchelewesha maendeleo nchini.

Nakumbuka harakati hizi zlikuwa zinapiga kelele dhidi ya hiki anacholia nacho Mh Rais Magufuli kila kukicha,wizi,Rushwa,kujilimbikizia mali,Uwekezaji wa hasara.

Je Simbachawene anataka kusema Vyama vya upinzani vingekaa kimya wakati Buzwagi wanawasainisha mawaziri wetu mikataba mibovu hotelini?

Je Simbachawene anasema Vyama vya Upinzani vingekaa kimya wakati baadhi ya Mawaziri,wafanyabiasha na watumishi wa Umma wanagawana pesa za Escrow kwenye sandarusi?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya Siasa vikae kimya wakati wakazinwa Nyamongo wanateseka na maji yenye sumu kutoka mgodi wa North Mara,wanapigwa Risasi na wawekezaji?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji kwenye migodi walipojigeuza miungu watu(wasiguswe),walipokuwa wanawahakisha wenyeji kinyama tena usiku wa manane bila fidia?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji hawa walipokuwa wanachimba madini bila kulipa kodi?huku suala la mapato wakilifanya kuwa ni Siri kati yao na Serikali

Je Simbachawene alitaka vyama ya upinzani vikae kimya wakati Twiga wanahamishwa kwenda nje kwa ndege?wanyama wanauwa na wawindaji haramu?

Je Simbachawene alitaka watu wakae kimya huku kuna watumishi wa Umma walikuwa wanakula mishahara hewa?

Je Simbachawene alitaka wapinzani wakae kimya wakati baadhi ya Viongozi wetu wakuu walipoamua kujiuzia mpaka migodi ya madini?

Yaani haya yote,adhabu yake ni kuwazuia wanasiasa wasiseme chochote mpaka wakati wa uchaguzi na wakikaidi Msajili anawafuta katika wigo wa Siasa?

Mambo haya yanatafakarisha sana sana.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kinaitwa Structural Adjustment Programme,

National Economy Recovery Programme.

Etc,mambo ya nchi kujitoa ktk biashara na kuruhusu soko huria na hii ni baada ya uchumi kudorora na mashirika ya umma ku underperform
 
Ukiwa mwanasiasa lazima ujitoe akili kidogo,maana hayo yanafahamika dhahili nani aliharibu,lakini kwa sababu vichwa ni kwa ajili ya kushikilia masikio,macho na nywele inabidi waseme hivyo.
 
Back
Top Bottom