Hivi JK alijua anaongea na kundi gani pale Davos?

Hivi Dr. Kikwete huwa hajiandai (sijui hawa wakubwa WANAANDALIWA) kabla ya kwenda kuzungumza kama Rais wa nchi?

Mara kadhaa nimeona akijibu maswali au kuchangia issue kama kabambikizwa; hakujua kama itaibuka na hakujiandaa!

Hao washauri na etc wanaolipwa kwa kodi zetu wanafanya nini? Maana sasa inakuwa aibu!

Mfumo wetu wa utendaji katika siasa ndio unatuletea yote hayo, we cheki mawaziri wetu na jinsi wanavyojibu maswali bungeni, na cheki maswali ya nyongeza yanavyowaangusha na kulindwa-lindwa na spika!
Kumbuka ule mdahalo wa JK na waandishi wa habari wateule na maswali mateule na bado alipwaya sana ukilinganisha na midahalo ya wenzake.
 
Wakuu nimeona videos za JK anaongea kwenye Forum .Kwanza Brown hakumtambulisha kwa staha sana kama alivyo fanya kwa Zuma na Odinga .Najua mtabisha lakini kuna ushahidi wa jinsi alivyo mtambulisha JK kwenye panel .

JK naye kapewa nafasi anaanza kuongea kama anaongea na wazee wa CCM mkoa wa Dar .Jamaa kila mahali ni kuchapia oh Tanzania wakati tunapata uhuru tulikuwa na barabara 3 tu za lami .Akaanza porojo na kuacha maswali ya msingi .Je ni kweli aliona yuko sahihi na kuacha maswali ya msingi ? Ghalfa akacheka mwenyewe watu wamekauka tu ukumbi mzima .Ni kweli hakujua watu wanaongelea pale kitu gani ? I stand to be corrected jamani ila ushahidi upo nitaumwaga hapa soon wa kituko chake cha hadithi za barabara miaka 50 iliyopita .

Mkuu tunasubiri ushahidi huo tushuudie vituko na aibu hiyo unayosema
 
punguzeni hasira, naona contribution nyingi zemekuwa deleted, ila jamaa anatupozea sana.....
 
I can understand him he is frustrated this nations has bg problems than his head can take n think and when he is trying to solves he finds out he has led the nation to more large problems,so he fls hopeless,helpless and confused,

kama vipi changia Kwa kiswahili tu kaka maana hizi lugha ni za wenzetu, hakukua na ulazima wa kukivunjavunja kiingereza hivi
 
Wakuu wote JF .Niko Ethiopia sasa soon nitakuwa bongoland , nimeona hasira zetu kwa kweli mzee wetu katuangusha .Nadhani hakuelewa swali au nini kinaongelewa .Je tufanyeje maana bado foums 4 zinakuja na yeye hana aibu atazuka ili kuonana na wakubwa kwa madai yake ili aendelee kuomba wakati Dunia inajua hafai tena .Tufanyeje next time haya yasitokee .Najua ni tabia zake hawezi kuacha ila sasa tupunguze aibu next time ?
 
Huyu jamaa hadhi yake ni kuwa Mkuu wa Mkoa.. Presidency post ni cheo kikubwa sana kwake hana uwezo. Period

Mkuu I was confused pale alipo anza na barabara 3 wakati wa uhuru .Sikuelewa anataka kusema nini .Hapa pekee nilijua leo bomu kubwa na kweli tumeishia na aibu .Nikashangaa wakati akiongea ghafla kicheko kikuubwa kwenye a very serious issue .Sikuamini na ndiyo maana nimeuliza alidhani anaongea na wazee wa CCM kule Temeke ?Ila Brown anaujua uwezo wake ndiyo maana hata intro yake was so brief na haikuwa ya kuvutia hata kidogo .
 
ameniaibisha sana huyu jk.....wenzangu ofcin wamenishaga sana... naulizwa tu why did you install such a person to be your presindent?? he cannot answer the question aboout education??.....
 
Kwa nini amekubali kushiriki katika 'mjadala' huu n kupinga mjadala wa uchaguzi? Yaelekea JK bingwa wa kusoma yaliyoandikwa na si kujibu maswali yanayojitokeza.
 
hana mtiririko, hana mpangilio, lugha ni shida, na alichoniudhi ni kujibu swali tofait na aliloulizwa...!!!
 
Maana nilimshangaa ana zana kuleta quote za miaka 60 za Prof wake huko sijui Chuo gani alikuwa mie hata simwelewi JK .Hivi kuna ubaya gani kama angeamua kutumia kiswahili akapiga mbwembwe maana ndiyo zako ? Alidhani anaweza kuwakoga watu serious wale walio tumia gharama zao kwenda Davos ? Wale hawakusombwa na malori ili wakamsikilize no .
 
Maana nilimshangaa ana zana kuleta quote za miaka 60 za Prof wake huko sijui Chuo gani alikuwa mie hata simwelewi JK .Hivi kuna ubaya gani kama angeamua kutumia kiswahili akapiga mbwembwe maana ndiyo zako ? Alidhani anaweza kuwakoga watu serious wale walio tumia gharama zao kwenda Davos ? Wale hawakusombwa na malori ili wakamsikilize no .



kama umechunguza kwa makini mle ndani wajumbe wengi wakuwa bize na simu zao wakati anaongea jk.....tofauti na wakat zenawa na zuma wanaongea.....
 
Back
Top Bottom