jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,687
- 1,780
Hivi Dr. Kikwete huwa hajiandai (sijui hawa wakubwa WANAANDALIWA) kabla ya kwenda kuzungumza kama Rais wa nchi?
Mara kadhaa nimeona akijibu maswali au kuchangia issue kama kabambikizwa; hakujua kama itaibuka na hakujiandaa!
Hao washauri na etc wanaolipwa kwa kodi zetu wanafanya nini? Maana sasa inakuwa aibu!
Mfumo wetu wa utendaji katika siasa ndio unatuletea yote hayo, we cheki mawaziri wetu na jinsi wanavyojibu maswali bungeni, na cheki maswali ya nyongeza yanavyowaangusha na kulindwa-lindwa na spika!
Kumbuka ule mdahalo wa JK na waandishi wa habari wateule na maswali mateule na bado alipwaya sana ukilinganisha na midahalo ya wenzake.