Hivi jamani kwanini wanawake hamna mapenzi ya kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi jamani kwanini wanawake hamna mapenzi ya kweli?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Michael Amon, Jan 25, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Jamani wana JF nimekuja hapa kwenu kuwaeleza hili swala na pia kuomba ushauri wenu kutokana na hili sakata lililonikuta la kusalitiwa na mpenzi wangu.

  Jana usiku wakati nikiwa nafanya kazi zangu mbali mbali niliamua kuingia katika mtandao wa facebook na kuhack account ya facebook ya mpenzi wangu ili kujua kama kweli ananipenda au napoteza mda wangu tu kumpenda mtu ambaye hapendeki. Niliamua kufanya hivyo baada ya kudanganywa password ya e-mail yake kipindi cha nyuma kwa kisingizio eti aliogopa kunipa e-mail yake kwa sababu eti aliwahi kumpa mpenzi wake wa nyuma e-mail yake na matokeo yake mpenzi wake akawa anaitumia e-mail yake kwa kumtuhumu makosa ambayo hajayatenda kwa hiyo aliogopa pengine na mimi ningemfanyia hivyo. Kwa jinsi nilivyompenda niliamua kumsamehe na kuendelea na uhusiano wetu kama kawaida.

  Sasa baada ya kufanikiwa kuhack katika account yake ya facebook nilianza moja kwa moja kwa kukagua profile yake, kutizama picha zake na mwishoni niliingia katika inbox yake na kuanza kusoma message zake. Jamani message nilizozikuta huko sitaki hata kusema. I wish kama ningekuwa na uwezo ningewawekea hapa ili na nyinyi mzione. Nilipomueleza na kumtaka aniambie ni kwa nini ameamu kunifanyia hivyo na kuamua kunisaliti na wanaume wengine tena wa facebook akanijibu na kuniambia kuwa eti alifanya vile kwa sababu eti wanaume wote wapo kuumiza tu ila hakumaanisha kila alichokuwa anasema katika message za facebook pia akaniambia kuwa japo aliumizwa ila alipokutana na mimi alinipa moyo wake wote cuz alinipenda sana na aliamini kuwa niko tofauti na wanaume wengine ila kiukweli hana mwanaume mwingine zaidi yangu.

  Kitu kingine nilichogundua ni kuwa huyo mpenzi wangu ana e-mail address ila mimi aliniambia e-mail address yake mmoja tu. Mimi nilihisi kuwa anazo mbili na baada ya kugundua hivyo nilimuuliza kuwa e-mail address ........ ni ya kwako??? akaniambia hapana na ya kwake ni hiyo aliyonipa kumbe hiyo e-mail ambayo alinificha ndiyo hiyo ambayo anaitumia facebook. Sasa leo baada ya kugundua hilo nilipomuuliza kwa nini alinidanganya kipindi kile alikana kabisa kuwa hakusema hivyo.

  Kwa jinsi nilivyo kasirika na kuumia moyoni nimeamua kuchana naye ingawa kiukweli nilimpenda sana msichana huyu, nilimpa kitu kitu alichohitaji, nilimpa mapenzi yangu yote, nilimpa hata vile visivyohadithika lakini bado mtoto wa kike haonyeshi kuridhika kila mwanaume anataka awe wake. kama nilivyosema hapo mimi nimeamua kuchana na nimeshamtakia wazi ila yeye bado ananiomba msamaha anasema eti hawezi kuishi bila mimi. Nifanyeje jamani?
   
 2. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Forget about the past and keep looking forward,makosa katika maisha ni kama maandishi ya kalamu ya wino,ukikosea huwezi ku-erase maandishi ila unaweza ku-cancel tu kwa mstari mmoja wa wino.Huo mstari mmoja wa wino ndio mpenzi wako mpya.Lakini kumbuka kwamba licha ya huo mstari mmoja ku-cancel yale maandishi bado yataendelea kuonekana tu nikimaanisha hata ukimpata mwenza mpya lakini bado kivuli cha mpenzi wa zamani kipo.
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Usemayo ni kweli kabisa mkuu. Nashukuru kwa ushauri wako
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,586
  Likes Received: 762
  Trophy Points: 280
  Hivi, in case tukikagua emails zako, inbox zako zote JF, FB sijui twitter; hatutakuta umeflirt na mtu, kiutani au hata seriously?
   
 5. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,791
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  yaani kuflirt na wanaume wengine ndio kisa cha kumuacha?
  mie hata nikiolewa sitaacha kuflirt,unless umenikuta kitandani na mtu tunafanya mapenzi ndio nitakuelewa ukisema unaniacha sio upuuzi wa kusoma messages...............................

  unahack vipi account facebook embu nifundishe nataka kuhack account ya mtu lol,am serious lol
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,061
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Mambo mengine ni kujitakia presha kama siyo BP..achana na email mimi hata simu ya mpenzi wangu imekaa hapo pembeni siigusi na yes ana marafiki wa kike, ma-X sijui Y na kadhalika..sasa nikianza kufuatilia kila kitu nitakuwa ana amani kweli ya roho? na yeye vivyo hivyo kwangu, ni kuwa na imani mtu anakupenda na kuheshimiana.

  Pole kwa uliyoyakuta..kama umeamua kumuacha basi usiumie roho mana ni uamuzi uliodhamiria.
   
 7. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Neema!!!! umeniacha hoi hapo! hahahaha
   
 8. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,589
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wewe achana nae huyo! Utakufa kwa presha bure! Hata mimi nakwambia ukweli toka moyoni nimeumizwa wiki hii hii! Huweziamini nimekonda kwa siku2 tu! Kula kwa taabu mawazo kibaao mwenzako anajirusha tu! Piga chini!
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Huwezi kukuta
   
 10. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Asante sana kwa ushauri wako. na wewe pia pole kwa yaliyokukuta
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Mwanzoni sikuwa na lengo la kukagua kitu chochote kuhusu yeye. Yani tokea tumeanza uhusiano mpaka sasa sijawahi kusoma msg yake hata moja katika simu yake lakini baada ya kunidanganya password ya e-mail yake nikahisi kuna kitu ananificha nikaona bora nifuatilie nijue kinachoendelea
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Sasa huyo ni WANAWAKE au MWANAMKE?

  Nwy pole kama wewe nae hujawahi kuflirt na watu wengine wakati ukiwa kwenye mahusiano nae.
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  kama kuflirt ndio tabia yako na mpenzi wako anaipenda its ok. Lakini mimi sina tabia hiyo na wala sipendi mpenzi wangu awe na tabi hiyo. umenielewa???
   
 14. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,589
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  powa mkuu! Mi ni msemakweli daima!
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mwanaume. Asante Lizzy
   
 16. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 5,778
  Likes Received: 2,162
  Trophy Points: 280
  Pole sn ndugu yangu..dah nadhani nami niko kwnye kundi km lako tu. BTW alichomaanisha Lizzy co kukuuliza km ww ni HE au SHE,anamaanisha umegeneralize wanawake wote ilhali huyo ni mmoja tu...that means ungeweka exception.
   
 17. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kichwa ngumu na kukaza shingo dhidi ya wanaume kunawa-cost wanawake wengi.Najua Wanawake mtalipinga hili lakini.....SIRI SIRINI.
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,134
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  kwani wanamme wote wana mapenzi ya kweli?

  Wahenga walisema'kwenye msafara wa mamba na kenge wako'

  Tafakari, chukua hatua, haki mapenziiiii!
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu. Nimekuelewa
   
 20. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,617
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa ushauri wako mkuu. Nimekuelewa
   
Loading...