Hivi jamani kwanini wanawake hamna mapenzi ya kweli?

Jamani wana JF nimekuja hapa kwenu kuwaeleza hili swala na pia kuomba ushauri wenu kutokana na hili sakata lililonikuta la kusalitiwa na mpenzi wangu.

Jana usiku wakati nikiwa nafanya kazi zangu mbali mbali niliamua kuingia katika mtandao wa facebook na kuhack account ya facebook ya mpenzi wangu ili kujua kama kweli ananipenda au napoteza mda wangu tu kumpenda mtu ambaye hapendeki. Niliamua kufanya hivyo baada ya kudanganywa password ya e-mail yake kipindi cha nyuma kwa kisingizio eti aliogopa kunipa e-mail yake kwa sababu eti aliwahi kumpa mpenzi wake wa nyuma e-mail yake na matokeo yake mpenzi wake akawa anaitumia e-mail yake kwa kumtuhumu makosa ambayo hajayatenda kwa hiyo aliogopa pengine na mimi ningemfanyia hivyo. Kwa jinsi nilivyompenda niliamua kumsamehe na kuendelea na uhusiano wetu kama kawaida.

Sasa baada ya kufanikiwa kuhack katika account yake ya facebook nilianza moja kwa moja kwa kukagua profile yake, kutizama picha zake na mwishoni niliingia katika inbox yake na kuanza kusoma message zake. Jamani message nilizozikuta huko sitaki hata kusema. I wish kama ningekuwa na uwezo ningewawekea hapa ili na nyinyi mzione. Nilipomueleza na kumtaka aniambie ni kwa nini ameamu kunifanyia hivyo na kuamua kunisaliti na wanaume wengine tena wa facebook akanijibu na kuniambia kuwa eti alifanya vile kwa sababu eti wanaume wote wapo kuumiza tu ila hakumaanisha kila alichokuwa anasema katika message za facebook pia akaniambia kuwa japo aliumizwa ila alipokutana na mimi alinipa moyo wake wote cuz alinipenda sana na aliamini kuwa niko tofauti na wanaume wengine ila kiukweli hana mwanaume mwingine zaidi yangu.

Kitu kingine nilichogundua ni kuwa huyo mpenzi wangu ana e-mail address ila mimi aliniambia e-mail address yake mmoja tu. Mimi nilihisi kuwa anazo mbili na baada ya kugundua hivyo nilimuuliza kuwa e-mail address ........ ni ya kwako??? akaniambia hapana na ya kwake ni hiyo aliyonipa kumbe hiyo e-mail ambayo alinificha ndiyo hiyo ambayo anaitumia facebook. Sasa leo baada ya kugundua hilo nilipomuuliza kwa nini alinidanganya kipindi kile alikana kabisa kuwa hakusema hivyo.

Kwa jinsi nilivyo kasirika na kuumia moyoni nimeamua kuchana naye ingawa kiukweli nilimpenda sana msichana huyu, nilimpa kitu kitu alichohitaji, nilimpa mapenzi yangu yote, nilimpa hata vile visivyohadithika lakini bado mtoto wa kike haonyeshi kuridhika kila mwanaume anataka awe wake. kama nilivyosema hapo mimi nimeamua kuchana na nimeshamtakia wazi ila yeye bado ananiomba msamaha anasema eti hawezi kuishi bila mimi. Nifanyeje jamani?
Pole sana
 
Mambo mengine ni kujitakia presha kama siyo BP..achana na email mimi hata simu ya mpenzi wangu imekaa hapo pembeni siigusi na yes ana marafiki wa kike, ma-X sijui Y na kadhalika..sasa nikianza kufuatilia kila kitu nitakuwa ana amani kweli ya roho? na yeye vivyo hivyo kwangu, ni kuwa na imani mtu anakupenda na kuheshimiana.

Pole kwa uliyoyakuta..kama umeamua kumuacha basi usiumie roho mana ni uamuzi uliodhamiria.
Hahaha
 
Wewe achana nae huyo! Utakufa kwa presha bure! Hata mimi nakwambia ukweli toka moyoni nimeumizwa wiki hii hii! Huweziamini nimekonda kwa siku2 tu! Kula kwa taabu mawazo kibaao mwenzako anajirusha tu! Piga chini!
 
Jamani wana JF nimekuja hapa kwenu kuwaeleza hili swala na pia kuomba ushauri wenu kutokana na hili sakata lililonikuta la kusalitiwa na mpenzi wangu.

Jana usiku wakati nikiwa nafanya kazi zangu mbali mbali niliamua kuingia katika mtandao wa facebook na kuhack account ya facebook ya mpenzi wangu ili kujua kama kweli ananipenda au napoteza mda wangu tu kumpenda mtu ambaye hapendeki. Niliamua kufanya hivyo baada ya kudanganywa password ya e-mail yake kipindi cha nyuma kwa kisingizio eti aliogopa kunipa e-mail yake kwa sababu eti aliwahi kumpa mpenzi wake wa nyuma e-mail yake na matokeo yake mpenzi wake akawa anaitumia e-mail yake kwa kumtuhumu makosa ambayo hajayatenda kwa hiyo aliogopa pengine na mimi ningemfanyia hivyo. Kwa jinsi nilivyompenda niliamua kumsamehe na kuendelea na uhusiano wetu kama kawaida.

Sasa baada ya kufanikiwa kuhack katika account yake ya facebook nilianza moja kwa moja kwa kukagua profile yake, kutizama picha zake na mwishoni niliingia katika inbox yake na kuanza kusoma message zake. Jamani message nilizozikuta huko sitaki hata kusema. I wish kama ningekuwa na uwezo ningewawekea hapa ili na nyinyi mzione. Nilipomueleza na kumtaka aniambie ni kwa nini ameamu kunifanyia hivyo na kuamua kunisaliti na wanaume wengine tena wa facebook akanijibu na kuniambia kuwa eti alifanya vile kwa sababu eti wanaume wote wapo kuumiza tu ila hakumaanisha kila alichokuwa anasema katika message za facebook pia akaniambia kuwa japo aliumizwa ila alipokutana na mimi alinipa moyo wake wote cuz alinipenda sana na aliamini kuwa niko tofauti na wanaume wengine ila kiukweli hana mwanaume mwingine zaidi yangu.

Kitu kingine nilichogundua ni kuwa huyo mpenzi wangu ana e-mail address ila mimi aliniambia e-mail address yake mmoja tu. Mimi nilihisi kuwa anazo mbili na baada ya kugundua hivyo nilimuuliza kuwa e-mail address ........ ni ya kwako??? akaniambia hapana na ya kwake ni hiyo aliyonipa kumbe hiyo e-mail ambayo alinificha ndiyo hiyo ambayo anaitumia facebook. Sasa leo baada ya kugundua hilo nilipomuuliza kwa nini alinidanganya kipindi kile alikana kabisa kuwa hakusema hivyo.

Kwa jinsi nilivyo kasirika na kuumia moyoni nimeamua kuchana naye ingawa kiukweli nilimpenda sana msichana huyu, nilimpa kitu kitu alichohitaji, nilimpa mapenzi yangu yote, nilimpa hata vile visivyohadithika lakini bado mtoto wa kike haonyeshi kuridhika kila mwanaume anataka awe wake. kama nilivyosema hapo mimi nimeamua kuchana na nimeshamtakia wazi ila yeye bado ananiomba msamaha anasema eti hawezi kuishi bila mimi. Nifanyeje jamani?
Hata mama yako au mamayo dume?
 
Back
Top Bottom