Hivi inawezekanaje kufanya unyama kama huu kwa mtu unayempenda?

Mimi naomba tu kujua yalomkuta jamaa wa kwenye pic tafadhali, aaaarrgh' tusiopo IG mengine yanatupita tu kimya kimya kama upepo..!!
Huyo Bwana Yupo Kenya Alifunga Ndoa Na Mkewe!!
Siku Moja Akipotoka Job Night Shift, Kufika Home Akalala Kupumzika. Huyo Dada Ambaye Ni Mkewe Akamwagia Tindikali



Na Akaenda Kwenye Switch Ya Umeme Akatega Waya Na Kumwaga Maji Chumba Chote Ili Akiamka Apigwe Short
Jamaa Alipomwagiwa Tindikali Sura Ikawa Hivyo
Na Alipigwa Short Majirani Wakamsaidia
 
Mimi naomba tu kujua yalomkuta jamaa wa kwenye pic tafadhali, aaaarrgh' tusiopo IG mengine yanatupita tu kimya kimya kama upepo..!!

Hivi inawezekanaje kufanya unyama kama huu kwa mtu unayempenda?
 
Wanawake tukiamua ni balaa
Watu mkishindwana na hakuna maelewano ndani ya nyumba muachane au mpeane break
Mtu nnaempenda siwezi mdhuru hata kama kaniudhi kiasi gani
Bora kuachana kwa kweli maana hii sio hali ya ubinadamu kabisa alafu alivyojibu sasa kama sio yeye vile.
There's a very thin line between love and hate
Kweli mkuu
Nina miaka 6 sasa siwaamini tena hawa wadogo zake na Eva/Hawa maana sijui ni maneno gani mengine waliongea na Shetani.
na ukiwaamini tu umeisha
 
Hivi inawezekanaje kufanya unyama kama huu kwa mtu unayempenda?
Daah inasikitisha sana, kuna watu wana roho ngumu
 
Huku nakoishi jamaa mmoja ameuliwa siku ya Christmas kisa wivu wa mapenzi. Binti kakuta sijui msg kamtandika jamaa kisu.
Nchi nliopo wanauana kama kuku. Jamaa kamkaba demu mpaka kafa na yeye kajinyonga, mwingine jamaa kaenda kulewa na demu wake baada ya kulewa demu kamwagia dizeli kamchoma moto mpaka kufa. Cases ni nyingi. Mwingine manzi kamfungia jamaa ndani ya nyumba kamwaga petroli kamchoma jamaa....
 
Inasikitisha sana kiukweli
~ Mke ni baraka
~ Mke ni mlango wa mafanikio
~ Mke anakuletea watoto unaheshimika kama mwanaume
~ Unapokwama mke anasimama usifedheheke
~ Linapokupata jambo la aibu na fedheha mke anakuwa kama mtandio kukufunika ile aibu ikuondoke

Lakin narudia tena lakini jikague kabla hujaoa. Jiangalie ulikopita, vivuli vya tulikopita hutufwata tuendapo.

Kama unaona kuna mahali uliharibu kupitiliza na hujasolve zile tofauti mara mia usioe, kaa tu kama alivyokuwa marehemu Ruge. Maana huyo unayesema she is the right one she might be your death sentence.

Ndoa ni njema na nzuri lakini sio kila mmoja wetu ataoa au kuolewa.

NB: Namuhurumia sana mwamba kwenye picha lazima akikaa anasema labda ningemuoaga flani haya yasingenikuta but too late

View attachment 1675935

Kusoma kilichomsibu jamaa ingia >>> Hivi inawezekanaje kufanya unyama kama huu kwa mtu unayempenda?

Dear men jifunzeni kumtaja Mungu, ombeni sana kabla hamjaoa na waswahili husema mchagua Nazi huangukia koroma.
Umemalizia vizuri mno, kosea vyote sio kuoa au kuolewa
 
Back
Top Bottom