Hivi inawezekanaje kufanya unyama kama huu kwa mtu unayempenda?

recycle Bin

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
3,121
2,000
Kwa mujibu wa mtaalamu wa Psychiatry, magonjwa ya akili miongoni mwa wakina mama walioko kwenye ndoa ni mengi sana na yanawasababishia kufanya mabaya kwa wenzi wao, mfano ndo kama huu hapa:

Picha hii inamuonesha mwanaume mmoja nchini Kenya ajulikanae kwa jina la Dan Shisia Matakhaya, mwenye umri wa miaka 31 na ni Askari polisi nchini humo.

Hakuzaliwa na sura ya kutisha namna hii. Unachokiona ni matokeo ya mabishano kati yake na mke wake.

Siku moja, Matakhaya na mke wake walipishana kuhusu masuala kadhaa ya kifamilia, yeye alichukulia mtafaruko au mapishano hayo kama kitu cha kawaida tu na baadae siku hiyohiyo akaenda kazini. Aliingia zamu ya usiku na kurudi kesho yake majira ya saa kumi na moja na nusu alfajiri.

Kwasababu alifanya kazi usiku kucha, baada ya kurudi nyumbani alienda moja kwa moja kitandani na kulala.

Huo ukawa wakati mzuri kwa mke wake kuja na kumwagia tindikali usoni. Kisha mkewe akakimbia na kuondoka zake. Lakini haikutosha kwa mwanamke huyo kuiharibu sura ya mumewe, akalimwaga pia maji sakafuni na kuunganisha nyaya za umeme ilikusudi mumewe akikanyaga maji yale apigwe shoti ya umeme, na mumewe kweli alikanyaga maji yale na kurushwa na shoti ya umeme.

Alipokuwa akipiga kelele,majirani walikuja wakamkuta ameanguka hajitambui na haelezeki. Majrani wakampeleka hospitalini. Maisha yake yakaokolewa, lakini macho yake yakapofuka kabisa.

Mke wake alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana ili kungoja kesi mahakamani. Matakhaya akamsamehe mke wake kwa yote aliyoyafanya japo akasema hatoweza kuondoa kesi mahakamani dhidi ya mwanamke huyo.

Amekutana naye mara moja mahakamani kisha mwanamke huyo akasema hajui ni kwanini alifanya hayo ya aibu na hatari kweli kweli!

Hapa ndipo utajua muishipo watu wawili na zaidi yawapasa kuomba amani kwa Mwenyezi Mungu, maana mmeingia kwenye hali ya hatari endapo shetani akajipenyeza kwa mmoja wenu.

Matakhaya alisoma sheria na kufuzu Shahada ya suala jinai (criminology). Anajitahidi sasa kila siku kuendana na maisha yake mapya. Ndoto yake ni kuwa kiongozi wa mfano kwenye harakati za kupambana na unyanyasaji majumbani (Domestic violence).

NB: Mkipishana kauli kwenye familia hakikisheni mnatumia muda na akili alikadhali hekima kufikia mwafaka, kuanzisha mtafaruko na kuondoka unarudi huna hata muda wa kuwekana sawa ni jambo la hatari sana wewe baba na wewe mama mkae mkilijua hilo. Inasikitisha sana.
IMG_2894.jpg

IMG_2895.jpg

IMG_2893.jpg
 
Mwamba028

JF-Expert Member
Nov 15, 2013
4,174
2,000
Wanawake tukiamua ni balaa
Watu mkishindwana na hakuna maelewano ndani ya nyumba muachane au mpeane break
Mtu nnaempenda siwezi mdhuru hata kama kaniudhi kiasi gani
shetani yupo na ana nguvu, so muombe sana Mungu, c umesikia mama mwenyewe anasema hajui hata ilikuwaje akafanya vile
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
13,294
2,000
Nina miaka 6 sasa siwaamini tena hawa wadogo zake na Eva/Hawa maana sijui ni maneno gani mengine waliongea na Shetani.
 
Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
8,194
2,000
Wanawake tukiamua ni balaa
Watu mkishindwana na hakuna maelewano ndani ya nyumba muachane au mpeane break
Mtu nnaempenda siwezi mdhuru hata kama kaniudhi kiasi gani
Dada angu....60% ya wanawake walioolewa hawawapend waume zao..waliolewa kwasbabu ya moral insecurities zao tuu na umr kwenda na ugum wa maisha..so akishaona keshapata alichofanya unafkir atamvumilia mumewe asiempenda tena wanalala kitanda ki1 maisha yao yote...si rahis
 
TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,657
2,000
Kwa mujibu wa mtaalamu wa Psychiatry, magonjwa ya akili miongoni mwa wakina mama walioko kwenye ndoa ni mengi sana na yanawasababishia kufanya mabaya kwa wenzi wao, mfano ndo kama huu hapa:

Picha hii inamuonesha mwanaume mmoja nchini Kenya ajulikanae kwa jina la Dan Shisia Matakhaya, mwenye umri wa miaka 31 na ni Askari polisi nchini humo.

Hakuzaliwa na sura ya kutisha namna hii. Unachokiona ni matokeo ya mabishano kati yake na mke wake.

Siku moja, Matakhaya na mke wake walipishana kuhusu masuala kadhaa ya kifamilia, yeye alichukulia mtafaruko au mapishano hayo kama kitu cha kawaida tu na baadae siku hiyohiyo akaenda kazini. Aliingia zamu ya usiku na kurudi kesho yake majira ya saa kumi na moja na nusu alfajiri.

Kwasababu alifanya kazi usiku kucha, baada ya kurudi nyumbani alienda moja kwa moja kitandani na kulala.

Huo ukawa wakati mzuri kwa mke wake kuja na kumwagia tindikali usoni. Kisha mkewe akakimbia na kuondoka zake. Lakini haikutosha kwa mwanamke huyo kuiharibu sura ya mumewe, akalimwaga pia maji sakafuni na kuunganisha nyaya za umeme ilikusudi mumewe akikanyaga maji yale apigwe shoti ya umeme, na mumewe kweli alikanyaga maji yale na kurushwa na shoti ya umeme.

Alipokuwa akipiga kelele,majirani walikuja wakamkuta ameanguka hajitambui na haelezeki. Majrani wakampeleka hospitalini. Maisha yake yakaokolewa, lakini macho yake yakapofuka kabisa.

Mke wake alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana ili kungoja kesi mahakamani. Matakhaya akamsamehe mke wake kwa yote aliyoyafanya japo akasema hatoweza kuondoa kesi mahakamani dhidi ya mwanamke huyo.

Amekutana naye mara moja mahakamani kisha mwanamke huyo akasema hajui ni kwanini alifanya hayo ya aibu na hatari kweli kweli!

Hapa ndipo utajua muishipo watu wawili na zaidi yawapasa kuomba amani kwa Mwenyezi Mungu, maana mmeingia kwenye hali ya hatari endapo shetani akajipenyeza kwa mmoja wenu.

Matakhaya alisoma sheria na kufuzu Shahada ya suala jinai (criminology). Anajitahidi sasa kila siku kuendana na maisha yake mapya. Ndoto yake ni kuwa kiongozi wa mfano kwenye harakati za kupambana na unyanyasaji majumbani (Domestic violence).

NB: Mkipishana kauli kwenye familia hakikisheni mnatumia muda na akili alikadhali hekima kufikia mwafaka, kuanzisha mtafaruko na kuondoka unarudi huna hata muda wa kuwekana sawa ni jambo la hatari sana wewe baba na wewe mama mkae mkilijua hilo. Inasikitisha sana.
View attachment 1675401
View attachment 1675402
View attachment 1675403
Women are soo dangerous. Nawaogopa sana hawa viumbe kiasi natathmin kila atua zake.
 
pisi jacky

Member
Oct 21, 2020
32
150
~ Mke ni baraka
~ Mke ni mlango wa mafanikio
~ Mke anakuletea watoto unaheshimika kama mwanaume
~ Unapokwama mke anasimama usifedheheke
~ Linapokupata jambo la aibu na fedheha mke anakuwa kama mtandio kukufunika ile aibu ikuondoke

Lakin narudia tena lakini jikague kabla hujaoa. Jiangalie ulikopita, vivuli vya tulikopita hutufwata tuendapo.

Kama unaona kuna mahali uliharibu kupitiliza na hujasolve zile tofauti mara mia usioe, kaa tu kama alivyokuwa marehemu Ruge. Maana huyo unayesema she is the right one she might be your death sentence.

Ndoa ni njema na nzuri lakini sio kila mmoja wetu ataoa au kuolewa.

NB: Namuhurumia sana mwamba kwenye picha lazima akikaa anasema labda ningemuoaga flani haya yasingenikuta but too late

7AE05470-3C41-430C-A9B7-494A2E8493BE.jpeg

Kusoma kilichomsibu jamaa ingia >>> Hivi inawezekanaje kufanya unyama kama huu kwa mtu unayempenda?

Dear men jifunzeni kumtaja Mungu, ombeni sana kabla hamjaoa na waswahili husema mchagua Nazi huangukia koroma.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom