Mpunguze maelekezo kwenye maisha ya watu jamani !! Mambo ya kuzaa , kuolewa na kuoa ni choice za mtu binafsi.
Na nyie mnaozaa na kuoa kwa mkumbo mnashindwa kulea yale yale unakutana na mtoto asubuhi anaenda shule shati ina kifungo kimoja unajiuliza ina maana huyu mzazi weekend nzima hakupata nafasi ya kukagua hata shati ya mtoto ? Mtoto asubuhi mapema mafuta kapaka upande mmoja , nywele zina mchanga wa jana, shingo ina uchafu maana yake mtoto anajiosha kila siku, kitoto kimepauka utasema usiku mmemchimbisha mashimo mtoto.
Au kiatu kimechanika sole ya kiatu yote anaiburuza na ni jumatatu.
Hapa mtakimbilia kusema hali hazifanani tunawajua 😂 jamani ukizaa watoto kumbuka kuwaangalia every inches wale hawakukuandikia barua ya maombi uwazae zilikua ni furaha zako na mihemko, simamia watoto
kuna hali kweli mtoto hata umwangalie vipi atakuchomoka tu wenye watoto hili tunalijua hakuna bingwa wa malezi.
Ila wazazi mmezidi watoto wanatembea ni wachafu , na hawana mahitaji na wazazi wengi msioangalia watoto ndo mnakomaaga watu waolewe na wazae bila kujisikiliza wao "Zaa kila mtoto anakuja na sahani yake" ndo hayo week ijayo vitoto vinafungua shule minywele hiyo , makucha marefu maana yake umemleta mtoto duniani ili umtese.
Wadogo zangu ambao hamjaoa au kuolewa au kuzaa mtu asikupangie chochote kuhusu unavyotakiwa au lini uingie kwenye ndoa au uzae sema na moyo wako kijana /binti angalia hali yako.
Na vyote vikikushinda acha kama huviwezi sio dhambi na sio lazima kuoa au kuolewa au kupata watoto.
Wazazi osheni watoto ni wachafu ni aibu