Hivi inakuwaje Mji wa Nazareth Israel waislamu ni wengi lakini hawana ugomvi na Wayahudi Kama wapalestina

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Mji wa Nazareth Israel ndio Mji mkubwa ndani ya Israel wenye waarabu waislamu wengi. Waislamu katika mji huo Ni asilimia 70 ya wakazi wote wa mji huo. Misikiti ipo mingi na hawana ugomvi na Wayahudi huishi nao kwa amani na utulivu. Huwezi kuta mwarabu muislamu akimsema vibaya myahudi Wala Huwezi kukuta myahudi akimsema vibaya mwarabu muislamu. Wanaishi kwa amani na upendo Sana

Swali langu hivi waarabu waislamu wapalestina kwa nini hawaelewani na Wayahudi na wanawachukia tofauti na wa Nazareth?
 
Palestine ni nchi iko chini ya Israel. Ni occupied territory wao wanapiginia haki ya nchi yao kuwa huru.
Waraabu walioko Nazareth ndani ya Israel ni raia wa Israel .
Ni vitu viwili tofauti.
Lakini sio kweli kama huko Nazareth warabu wana haki sawa na Wayahudi. Kwanza marufuku kuoa myahudi
 
sio kweli kama huko Nazareth warabu wana haki sawa na Wayahudi. Kwanza marufuku kuoa myahudi
Dini ya kiyahudi haitaki muumini nje ya Wayahudi sababu kubwa ni za kdini hata sisi waswahili haturuhusiwi kuolewa au kuoa myahudi sababu sio Wayahudi.
Wako Kama wahindi hawahitaji asiye muhindi kujiunga na dini yao Wala kuoana nao
Ninaposema wako sawa hawabaguani popote iwe kwenye Shule ,vyuo ,mahotelini au sehemu za starehe au sherehe ,misiba nk kwenye kusali na kuoana kila mtu kivyake Lakini kwenye maisha ya kawaida wako Pamoja iwe kwenye vyama vya siasa,kugombea nk wako pamoja
 
Palestine ni nchi iko chini ya Israel. Ni occupied territory wao wanapiginia haki ya nchi yao kuwa huru.
Waraabu walioko Nazareth ndani ya Israel ni raia wa Israel .
Ni vitu viwili tofauti.
Lakini sio kweli kama huko Nazareth warabu wana haki sawa na Wayahudi. Kwanza marufuku kuoa myahudi
Ni kama mkiristu wa bara kumuoa mwanamke wa Zanzibar. Ushnzy mtupu
 
mgogoro wa palestina unachochewa zaidi na mataifa ya nje kupita hata wapalestina wenyewe, na palestina huu mgogoro ni advantage kwao ya kupata misaada kutoka mataifa ya kiarabu na ulaya,, hawawez kukubali uishe
 
Mji wa Nazareth Israel ndio Mji mkubwa ndani ya Israel wenye waarabu waislamu wengi. Waislamu katika mji huo Ni asilimia 70 ya wakazi wote wa mji huo. Misikiti ipo mingi na hawana ugomvi na Wayahudi huishi nao kwa amani na utulivu. Huwezi kuta mwarabu muislamu akimsema vibaya myahudi Wala Huwezi kukuta myahudi akimsema vibaya mwarabu muislamu. Wanaishi kwa amani na upendo Sana

Swali langu hivi waarabu waislamu wapalestina kwa nini hawaelewani na Wayahudi na wanawachukia tofauti na wa Nazareth?
Mbona ile Israel yenyewe inasemekana kuwa sio mahali pake. Kuna ushahidi kuwa Israel ilikuwapo Africa na ilikuwa bonge la nchi ikipakana na Misri, Ethiopia, Libya. Baadhi ya ma-DIASPORA wanaokaa nje wanahistoria za mababu zao zikikubaliana kuwa wao ni wayahudi tena walitoka kwenye kingdom za Afrika.
 
Palestina ina mkono wa Iran,

Iran hataki pelestina na Israel wawe Nchi moja,wakati palestina ni km wilaya ya bagamoyo tu
Ikumbukwe eneo lote la Israel kiasili ni la Wapalestina mpaka waliponyan'ganywa mwaka 1948,na Marekani kupitia mgongo wa UN
 
Mji wa Nazareth Israel ndio Mji mkubwa ndani ya Israel wenye waarabu waislamu wengi. Waislamu katika mji huo Ni asilimia 70 ya wakazi wote wa mji huo. Misikiti ipo mingi na hawana ugomvi na Wayahudi huishi nao kwa amani na utulivu. Huwezi kuta mwarabu muislamu akimsema vibaya myahudi Wala Huwezi kukuta myahudi akimsema vibaya mwarabu muislamu. Wanaishi kwa amani na upendo Sana

Swali langu hivi waarabu waislamu wapalestina kwa nini hawaelewani na Wayahudi na wanawachukia tofauti na wa Nazareth?
Umewezaje kujua kuwa Nazareth kuna muslims wengi , ukashindwa kujua shida iliyopo katika ya Palestine na Israel?
 
Wapalestina sio wote wenye ugomvi na Israel. Kuna wapalestina wengi wanatoka Gaza na ukingo wa magharibi kwenda kufanya kazi Israel kwa Amani kabisa.Wenye ugomvi na israel ni vikundi Vya wanamgomba Vya hamas na Islamic jihad. Tena hao wanachochewa na Iran vinginevyo amani ingeshapatikana!
 
Uwelewa wako ni mdogo ndugu na kama kitu hujui bora ukakaa kimia kuliko kuonekana kituko mbele za watu.
Kwanza tambua ule mgogoro sio wa kidini bali ni wakugombania ardhi kati ya Israel na palestina.
Israel ni taifa lenye raia wa dini tofauti huku dini ya kiyahudi ikiwa ndio kubwa ikifatiwa na uislam na kwa asilimia ndogo sana ya wakristo na dini nyingine. Kwa hiyo waislam anao waongelea mtoa mada ni raia wa Israel na si wapalestina, na wapo ndani ya vitengo mbali mbali vya usalama na wanahusika katika ukandamizaji unao fanywa na Israel dhidi ya wapalestina.
Alafu kingine kama unadhani raia wote wa palestina ni waislamu basi ninakusikitia sana maana kuna wakirsito wa kipalestina zaidi ya milion moja na nusu ambao ni asilimia 20 ya wapalestina wote, na asilimia 80 ni waislam kwa hiyo kama unadhani ukandamizaji na mauaji yanayo fanywa na taifa teule kutoka kwa mungu wenu dhidi ya wapalestina ni waislam tu ndio wanao teseka, basi kuanzia leo tambua ya kwamba kuna wakrisito wenzenu maelfu kwa maelfu wanateseka kwa sababu ya ukandamizaji unaofanywa na taifa teule.
 
Mbona ile Israel yenyewe inasemekana kuwa sio mahali pake. Kuna ushahidi kuwa Israel ilikuwapo Africa na ilikuwa bonge la nchi ikipakana na Misri, Ethiopia, Libya. Baadhi ya ma-DIASPORA wanaokaa nje wanahistoria za mababu zao zikikubaliana kuwa wao ni wayahudi tena walitoka kwenye kingdom za Afrika.
uganda
 
Back
Top Bottom