Hivi inakuaje mtu unakua hivi?

Hivi inakuaje mtu unakua hivi?

Salaam wanandugu naomba kuuliza,hivi hivi vitu vinasababishwa na nini?!!!

Chuki;Utakuta mtu anakua na chuki mbaya kwa binadamu mwenziwe bila sababu za msingi!Yaani anakuchukia tuu!hujamfanya lolote lile baya au zuri.
Mwingine hata kuongea hamjawahi ila anakuchia tu,mfano hata humu wapo anachukia fake I'd [emoji3] na ugomvi anamuanzishia kisa hakuna au walipishana kidogo!!

Unafiki sijui haswa tatizo ni nini ila kuna watu wanaona raha wenzao wakigombana au kutofautiana.Atafanya kila njia awachonganishe mzozane,msutane mradi yeye nafsi yake iridhike tu

Uchoyo;Kuna mijitu michoyo hapa duniani...mpk shetani anawashangaa..!.
Mtu mchoyo mpaka anaficha chakula uvunguni mwa kitanda au chooni mradi tu asigawe sijui hii hali inasababishwa na kitu gani?au kama ugonjwa sijajua tiba ni nini?
Ila wachoyo kwa kuombaaa...balaa!

Roho mbaya;Hawa ndo mwisho wa matatizo kuna watu wana mioyo migumu jamanii!!!kama wadudu...yaani atahakikisha anafanya fitna zote ili usifanikiwe au ukiwa na mafanikio kidogo yeye ananuna au hakusemeshi
Anatamani awe yy tu mwenye kufanikiwa baas wengine mumsujudie...!!!Sasa sijajua huu ni ugonjwa huu tiba ni nini ...!!!!Mtu anakua na roho nyeusi mpk anatamani kuona wenziwe wakiwa kama yeye maskini!!.

NB;Sisemi Mimi ni mkamilifu ila vingine vinazidi jamanii!
Kama ni ugonjwa basi hali ni mbaya sana!


My own brand!!
Woyoooo... Brand katika uboraa[emoji9]

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Umefurahii.

Bora kauliza, mastaajabu ya dunia hii mengi. Nishakutana na bibie mmoja Mmarekani mweusi ananisema kwamba eti mimi ananimind ila mpole mpole sana, kashazoea kupelekeshwa pelekeshwa kijeshi jeshi na kigomvi gomvi.

Mtu anaweza kukufanyia kisirani makusudi, eti kwa sababu anakupenda.

Nikasema wanaovuma wa Mara, kumbe hata huku Marekani wapo.
 
Umefurahii.

Bora kauliza, mastaajabu ya dunia hii mengi. Nishakutana na bibie mmoja Mmarekani mweusi ananisema kwamba eti mimi ananimind ila mpole mpole sana, kashazoea kupelekeshwa pelekeshwa kijeshi jeshi na kigomvi gomvi.

Mtu anaweza kukufanyia kisirani makusudi, etikwa sababu anakupenda.

Nikasema wanaovuma wa Mara, kumbe hata huku Marekani wapo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kashazoea kuwapata wa kumpeleka kijeshi jeshi
 
mi nadhani chuki inatokana na hasira, sasa hapo ni kwa muda gani unakaa na hasira ndo tatizo. mfano mie ninapokua na hasira nachukia kiasi cha kujiapiza vitu vingi vya kisasi ila kiuhalisia huwa hasira zangu hazidumu siku na zikiisha nasahau yote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom