Hivi ile Tume ya Waziri Mkuu kwa wahanga wa moto imetoa ripoti?

samesame

Senior Member
Jul 21, 2019
143
323
Waziri Mkuu alitoa siku tano ripoti iwe imetoka. lakn mpaka sasa ni siku 11 na binafs sijasikia taarifa yeyote kuhusu tukio hilo zaid zaid nasikia majeruhi ndio wanazidi kupukutika. toka vifo vya watu 69 had leo wamefikia 99. hizo ni ripoti rasmi za serikali.
Wasi wasi wangu na hili wanaweza lipotezea kama walivyopotezea ripoti ya matukio mengine. swali langu agizo la waziri mkuu limepuuzwa? waziri mkuu akitoa amri hadharani isipotekelezwa kwa muda husika ni kushusha hadhi ya waziri mkuu mbele ya raia. kama waziri mkuu anaweza ongea na utekelezaji ukawa ziro nani atasikilizwa?

Kwa akili zangu ndogo kuna watu walipaswa kujiuzuru kuonyesha uwajibikaji kwa kauli ya waziri mkuu. maana lile ni tangazo kwamba kuna watu hawajafanya wajibu wao kuzuia atahari zile. je ni kwamba hawajijui au dharau?

 
ripoti mpaka ikapitiwe kwanza na mkuu wa yote na isipompendeza haitatoka kabisa
Najaribu kuwaza tuu kuwa ripoti isomeke;
"Uchunguzi wa Tume umebaini kuwa Chama cha Dola kinahusika kwa kuingiza makafara yake kuelekea uchaguzi na tishio la watu kuchukua fomu kumpinga mwenyekigoda"
By; Mwenyekiti wa Tume.
Jee itatoka hadharani?
 
Huenda serikali kuu imetuhumiwa katika hiyo ripoti na ndio maana hawaitoa.

Ni wajibu wa vyombo vya habari kuhoji juu ya jambo hili.
 
Mmesahau eti siku ya ajali waziri mkuu alihoji kwanini ajali itokee mjini kabisa, saa mbili za asubuhi, polisi wapo, zimamoto wapo na ndio wameingia kazini kwahiyo wawajibishwe, kabla hajawachukulia hatua Jiwe akamuwahi, having kuwachukulia hatua huu ni muda wa maombolezo, Jiwe anajua kinachoendelea.
 
Mimi huwa sioni kazi anayofanya huyo PM, alipaswa kuwa bwana mifugo


Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake, Mwalimu Majaliwa yupo vizuri sana, anajua anachokifanya, yupo wise, na anatafakari mambo in advance, siwezi kumlinganisha na yule aliyesema kupambana na matajiri ni kazi ngumu, mara akaruhusu magari kuzidisha uzito wa mizigo the same week yakavunja daraja!
 
Back
Top Bottom