Hivi ICC ni kwa ajili ya viongozi wa Africa Pekee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ICC ni kwa ajili ya viongozi wa Africa Pekee

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Izack Mwanahapa, Dec 5, 2011.

 1. Izack Mwanahapa

  Izack Mwanahapa JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 497
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Toka nimeanza kusikia kitu kinaitwa mahakama ya ICC na Mtu anaitwa Moreno Okampo kesi nyingi ni kuhusu viongozi wa Africa tu. Au mahakama hii inatumika kama mkono wa Europ kuwaadhibu viongozi wa Africa wanaoonekana kuingilia maslahia yao?
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  hivi mtu kama Raulent Gbagbo alikuwa anaingilia maslahi gani kwa EU?
   
 3. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,807
  Likes Received: 2,581
  Trophy Points: 280
  Slobodan Milosevic?
   
 4. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,324
  Likes Received: 10,483
  Trophy Points: 280
  augusto pinochet
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  hivi jitu kama mkapa likipelekwa icc kwa mauaji ya zanzibar?na aliyefanya mauaji ya arusha je?
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  BUSH akishakamatwa na kufikishwa ICC ndipo nitaamini haina ubaguzi!
   
 7. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Exactly tuliundiwa sisi waafrika kutokana na laana ya viongozi wetu wanaoanguka na peni pasipo kujiuliza wala kuhoji wanachokisaini. Mi naambiwa kuwa wale wazungu walianza kuuleta Afrika mswada wa sheria ya kupitisha sheria za ICC na bila hiyana viongozi wetu mabwege wakaanguka na peni (wakasaini) bila hata ya kuhoji kwa ile kasumba kuwa kila kinachoasisiwa na mzungu ni cha kutoka kwa mungu, wazungu walipourudisha kwao kila nchi ikaingiza kipengele kinachosema raia wao kwa kosa lolote hawatapelekwa mahakama ya ICC mpaka mahaka au sheria za nchi zao kama zitaruhusu kufanya hivyo
   
 8. libent

  libent JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  viongozi wa kiafrika wanatakiwa kujifunza kutoka kwa wenzao wa ulaya, nchi za ulaya mambo mengi yako open hawatawali kwa mabavu hawang'ang'anii madaraka muda wao unapoishi wanaondoka madarakani by the way ICC ni mahakama ya dunia ambayo iko kwenye mpango wa New World Order
   
 9. Izack Mwanahapa

  Izack Mwanahapa JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 497
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kuna makampuni mengi sana ya ufaransa yanayoendesha unyonyaji katika nchi ya Gbagbo ndio maana wafaransa walipigana kufa na kupona ili kumng'oa Gbagbo ili wamweke Watara ambaye inasemekana ni kibaraka wao na ifact amekaa sana ufaransa even his wife ni mfaransa.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Slobodan milosevich na wazungu wengine walioshitakiwa kutokana na vita vya Balkan (Yugoslavia ya zamani etc) walifikishwa katika mahakama nyingine maalum iliyoundwa na UN ambayo makazi yake ni huko huko The Hague.
  Hiyo mahakama ilipewa muda wa kumaliza kazi zake, na si hii ya ICC iliyoundwa ya kudumu. Mahakama nyingine maalum za makosa ya jinai zilizoundwa na UN ni pamoja na hii ilyoko Arusha kuhusu watuhumiwa wa Rwanda, ile ya Sierra Leone na nyingine ya Cambodia.

  Hii ya kudumu ya ICC ndiyo ambayo tangu iundwe na kuanza kazi 2002, watuhumiwa wake wote 28 (Gbagbo ni wa 28) wametoka bara la Afrika.
   
 11. T

  Thesi JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Una uhakika yanaendesha unyonyaji. Au yanafanya biashara. Ukweli ni kuwa ICC imeundwa kuwahukumu waovu na wauaji. Afrika ndiko uovu na mauaji ni mambo ya aibu ni kawaida kabisa. Na nsio maana wewe huwezi kuona uovu huo kwa kuwa umeuzoea unakuja tu kuzishutumu nchi za maghariibi kuleta ICC. walete na ICC zingine tatu. Hii moja haitoshi kwa maovu tunayotenda waafrika. Kwani Milosevic ni mwafrika? Wale wakambodia wanaohukumiwa pia waafrika. Wauwe watu, wabake wanawake na mwisho waachwe kuwa viongozi. Hongera nchi za magharibi kuona umuhimu wa kuweka ICC kuwahukumu wababe wa Afrika. Unataka kuniambia Gbagbo hana makosa? Kauwa wangapi? Bashir hana Makosa? Kawatekeza wangapi?
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hivi kwa mawazo yako mazuri tu unaona alivyo fanya gagbo ni sawa? maana naona watu tunataka kupotosha mambo? au tuseme tanzania tunavyo fanya uchaguzi baada ya miaka mitano , tunafanya kilicho sawa au sicho? maana utasema tunafanya hivyo kulinda maslahi wa nchi za ulaya? je leo hii niki laumu polisi wetu kwa kupiga watu au kuchukua sheria mkononi utasema nimetumwa na ufaransa au ndivyo haki zangu zinatakiwa ziwe?
  wewe mwenyewe ni shahidi wa nchi nyingi za kiafrika ambapo uchaguzi ukifanyika kunakuwa hakuna haki, sasa watu wakipiganisa hiyo haki ni kwa sababu ya huyo mfaransa au ni haki yao?
   
 13. L

  Luiz JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bila ICC viongozi wa africa wangekuwa madikteta kwa hiyo naunga mkono hii mahakama ya ICC.
   
 14. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2014
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,439
  Likes Received: 14,098
  Trophy Points: 280
  HAWA JAMAA WALIKOMALIA ISHU YA KENYA MPAKA UHURU NA RUTO WAKAPATA KESI, tunashuhudia mauaji makubwa tena ya wanawake na watoto,hatumsikii obama,cameroon, na wengine, naunga mkono kujitoa icc
   
 15. R

  RockSpider JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2014
  Joined: Feb 16, 2014
  Messages: 6,875
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Crime kubwa against Humanity huratibiwa na kutekelezwa na mataifa ya kibeberu USA et al ... Kwa yale yaliyotokea Libya, Misri, Fallujah Iraq, Afghanistan, Congo na sasa West Africa wanakilimbitwa kwa EBOLA... Bush, Obama, Netanyahu, Cameroon et al wangetakiwa washtakiwe kwenye hiyo mahakama!!!... kwa hali ilivyo sasa ni uwazi usiopingika kuwa ICC imewekwa kama fimbo ya kuwatandika viongozi wote wa Kiafrika wenye kukataa sera zao za kukwapua rasilimali zetu... Mnakumbuka kuwa ile kesi ya Charles Taylor ilisitishwa kuonyeshwa baada ya Taylor kutamka kuwa alipelekwa mahakamani pale kwa kuwa alikataa mikata ya kishenzi ya mrabaha wa 3% kwenye almasi za Waliberia, alienda mbali zaidi baada ya kusema kuwa Yule Mwana mama Johnson ni USA Puppet aka Economic Hit Men aliendaliwa Harvard ... Mpaka leo dunia haikuwahi kujua kilichoendelea maana maamuzi yalifanyika ndani kwa ndani kwa maslahi ya watu wa magharibi ...Africa bado sanaaaa....
   
 16. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2014
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Wala Assad haimuhusu. Au wale hamas wanaorusha makonbora
   
 17. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2014
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,098
  Likes Received: 11,246
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kusaini hawakujua hili?? Wacha wakanyongwe
   
 18. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2015
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Viongozi wa nchi za kiafrika wanalalamika sana kuwa mahakama hii ipo kwa ajili viongozi wa kiafrika,kwa upande wangu hapana isipokuwa ni kwasababu viongozi wa nchi zetu wamekuwa wakituumiza sisi wanaotuongoza,mabomu,jela bila sababu na aina nyingine za mateso,je pasipokuwapo na hayo niliyoyataja watakamatwa viongozi wetu?jibu ni hapana,muda wa uongozi umekwisha wewe unataka kuendelea kwa kuvunja katiba,unataka chama chako kishinde tu hata ukishidwa ni lazima chama chako kiwepo madarakani na kutumia nguvu kupita kiasi, je machafuko yakitokea ni nani akamatwe?
  Naomba tuliangalie na tujadili ili liwe wazi kuwa tunajitakia wenyewe au la nini mawazo yako juu ya uongozi wa nchi za Afrika na mahakama ya ICC uholazi.
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2015
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  sidhani kama ni kwa ajiri ya Africa tu, mbona hawajatoa hati ya kumkamata abubakari shekau mpaka sasa
   
 20. engwe1980

  engwe1980 Member

  #20
  Mar 18, 2015
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bush angekuwa wa kwanza kupelekwa the Hegue kwa mauaji katika nchi mbalimbali
   
Loading...