Aina za viongozi wanaongoza nchi za Afrika ni ya kutilia mashaka

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,749
Kitu pekee ambacho kinatambulisha mwelekeo wa Nchi kimaendeleo ni aina ya viongozi wanaongoza na aina ya wanasiasa waliopo.

Nchi ambayo viongozi wake wanaongozwa Kwa mashinikizo ya organization za Ulaya, zenye nia ovu na Afrika na wanasiasa wake ni vibaraka wa organization hizo, watu wake wataendelea kuishi kwenye Maisha ya kitumwa milele.

Tatizo la Nchi nyingi Africa sio kushindwa kuondoa vyama tawala madarakani, maana Kuna Nchi nyingi zimetoa vyama tawala mara nyingi madarakani, lakini hali zao ni Mbaya kuliko ilivyo kuwa awali. Wananchi wake Bado wanalia Kwa mateso na taabu zinazotokana na kukosekana Kwa mifumo rafiki Kwa maendeleo yao.

Tatizo la Nchi nyingi za Kiafrika ni fikra na mifumo pandikizi juu ya Siasa, dini, uchumi na utamaduni ambayo inatumiwa na mataifa ya Ulaya na Amerika kuendelea kuzifanya Nchi nyingi za Afrika kuwa watumwa kwao, Kwa kuwatumia viongozi wetu kama bwana jera anavyotumia nyampara kuthibiti wafungwa wenzake. Kwa kuwatumi wanasiasa, dini n.k

Afrika tunahitaji viongozi wanaoweza kututoa kwenye mifumo hiyo ambayo inatumika kutufanya tuendelee kuishi Maisha ya kitumwa. Tunahitaji viongozi waliotayari kufa Kwa ajili ya kubomoa misingi hiyo. Maana ni mifumo inayolindwa Kwa gharama kubwa mno na mikakati mizito. Ni mifumo ambayo ndio imeshikilia maslahi ya Ulaya na Amerika kwenye Nchi nyingi za Africa. Ndiyo maana Sio rahisi kwa kiongozi atakayethubutu kukiuka au kuivunja misingi yao wasimthibiti au kumuondoa Kwa namna yoyote.

Tukitaka Nchi zetu na Africa ikombolewe, sio kuwaza namna ya kuondoa vyama tawala madarakani, maana hakuna chama ambacho watu wake wote ni wema au ni wabaya.

Shetani hawezi kuwa malaika Kwa Sababu tu yupo Kanisani au msikini. Hata Yuda usalti na tamaa ya fedha haikumtoka Kwa Sababu tu ni miongoni mwa wanafunzi wa Yesu.

Hatupaswi kuangalia vyama tu, bali tunapaswa kuangalia watu ambao wanaweza kuwa tayari kubomoa mifumo ya hovyo katika Nchi zetu na kuwaunga mkono kwa gharama zozote bila kujari ufuasi wa vyama.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom