Hivi huyu ni mnyama wa aina gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huyu ni mnyama wa aina gani?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kaka Mkubwa, Nov 11, 2009.

 1. Kaka Mkubwa

  Kaka Mkubwa Senior Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka kuona ...kaka kuona!
  Jamani kaka kuona ni mnyama wa aina gani, na ana sifa gani?
  Haya tunayoyasikia kuhusu kaka kuona ni kweli.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Nov 11, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  [​IMG]


  [​IMG]

  [FONT=&quot]Kwa Kiingereza Kakakuona anaitwa Pangolins, Ni mnyama mwenye mwili ulio zungukwa na magambana chakula chake kikuu ni mchwa (anteaters).[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kichwa cha Kakakuona ni kidogo lakini kirefu… Pia mkia wake ni mrefu (broad tails). Ni mnyama asiye na meno na hawana masikio yaliyo yaliyo jitokeza nje… Kiasi ya kwamba unaweza kudhani kuwa hawezi kusikia sauti yoyote, lakini ni mnyama mwenye uwezo mkubwa sana wa kusikia.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ni mnyama mwenye uwezo wa hali ya juu sana kwenye kuhisi harufu, ila si mwenye kuona vizuri (poor sight). [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kakakuona utumia mwili wake wenye magamba magumu kujilinda na maadui na wanyama wakubwa kama Chui, fisi na wadudu kama mchwa (japo ndio chakula chake).[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kakakuona anaulimi mrefu sana ukilinganisha na mwili wake… wakati mwingine ufikia hadi inches 16.[/FONT]
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mweh hata sijui sifa za wanyama
  labda Fidel80 akija atakujibu
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Makubwa haya...Fidel anawajulia sana Wanyama!...
  Mi nilijua mtaalamu ni Rafiki yangu mmoja anaitwa MziziMkavu!

  IPTL IPTL ,DOWANI ,RICHIMOND,tanesco mgao ..UFISADI,EPA,
  nchi nzuriii Tanzania karibuni wasio kwao wenye shida nataabu kukimbizwa na walowezi ..tanzania yawakatibisha ,,,,,,eeehh

   
 5. L

  Lipende Member

  #5
  Nov 11, 2009
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Kwa Kiingereza Kakakuona anaitwa Pangolins, Ni mnyama mwenye mwili ulio zungukwa na magambana chakula chake kikuu ni mchwa (ant eater), na hupatikana karibu au kwenye vichuguu na kipindi cha ukame huranda sana kutafuta vichuguu ili apate chakula.

  Mwili wa kakakuona umefunikwa na magamba magumu, yaliyofunika mgongo wote na ubavuni na sehemu za miguu, magamba hayajafuka sehemu za chini ya mwili wa mnyama pamoja na kichwa. hivyo hujilinda kwa kujizungusha (roll) kama tairi akificha sehemu laini pamoja na kichwa katika kujilindana maadui zake.

  [/FONT][FONT=&quot]Kichwa cha Kakakuona ni kidogo lakini kirefu… Pia mkia wake ni mrefu na mpana (broad tails). Ni mnyama asiye na meno na hawana masikio yaliyo yaliyo jitokeza nje… Kiasi ya kwamba unaweza kudhani kuwa hawezi kusikia sauti yoyote, lakini ni mnyama mwenye uwezo mkubwa sana wa kusikia.[/FONT][FONT=&quot]Ni mnyama mwenye uwezo wa hali ya juu sana kwenye kuhisi harufu, ila si mwenye kuona vizuri (poor sight) kwa ajili hii basi mnyama huyu hutembea kutafuta chakula usiku (noctunal) huweza kutembea mail chake kila usiku na kutumia shimo kama nyumba yake kwa takribani mwezi mmoja.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kakakuona anaulimi mrefu sana ukilinganisha na mwili wake(16") unaomuwezesha kula mchwa kwa kupenyesha ulimi kwenye tunnels za kichuguu kupata mchwa. pia tumbo lililo kama filigisi analotumia kusagia chakula pamoja na mchanaga na vimawe anavyokula, hii ni kwa ajili ya kukosa meno. Kakakuona huishi maisha ya kujitenga au mmoja mmoja( solitary) ingawa pia hutokea dume likawa na jike nyumba moja kwa muda, pia mama hukaa na mtoto wake mpaka miezi minne. mtoto huzaliwa amepauka (pale) na magamba laini ambayo huanza kukomaa ndani ya siku ya pili ya maisha yake. na hutembea na mama yake juu ya mgongo na wakati wa hatari kujiviringisha ndani ya mama yake.

  [/FONT] [FONT=&quot]Mila zilizoenea kuhusu utabiri wa kakakuona
  Huonekana mchana kipindi cha ukame wakati mchwa ni wachache lakini pia mwanzoni mwa mvua kunyesha wakati wa mchwa wengi. kipindi cha ukame atafuata uelekeo wa chakula au maji kwa hisia za eneo lipatikanalo mchwa pia huwa na harufu ile, mchwa ameshindwa kutabiri vita, mavuno au Mvua, lakini pia hutabiri kwa asilimia kadhaa uwepo wa mavuno na mvua ikatokea kuwa kweli.

  Swali? kama an uwezo wa kutabiri kwanini apewe maswali ya kuchagua?( multiple choice)
  Kwanini hupigiwa ngoma akielekea katika vitu wasivyohitaji?

  Adui mkubwa wa Mnyama huyu ni binadamu, kwa ajili ya kazi zake nyingi za kiimani. magamaba yake inasemekana yanatumika katiak kufukuzia uchawi na nguvu za giza ukichanganya na magome ya mti fulani.
  pia inasemekana magamba yake yanatumika kufukuzia wanyama wakali kama simba, fisi na chui karibu ya makazi. pia ukifukia magamba mlangoni kwako, inaleta mvuto kwa akina dada ( dawa ya mapenzi.)

  NB. kakakuona anafanana na myama mwingine anaitwa Muhanga( aardvark). ila huyu hana magamaba na huwa na mwili mkubwa.
  [/FONT]
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  huyo mnyama ni deal la kufa mtu pale kwa Mugabe(Zimbabwe), ukiwa nae we ni milionea.
   
 7. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kumbe ni deal kiasi hicho
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa Wanyamwezi miaka ya zamani alikuwa akionekana, walimchukua ili kutabiri nini kitatokea mbeleni. Walimuwekea vitu kibao kama Silaha, vyakula, maji, nk na akichagua silaha, basi ujuwe vita inakuja. Akichagua chakula basi kuna neema yaja.

  Ila nasikia kuna miaka kadhaa nyuma, alichamchagua Mhindi Mwizi. Inawezekana ndiyo maana tuna MIFISADI ya kutisha Tanzania(JOKE PLEASE).
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Asante sana ndugu Paka Jimmy lakini si unajuwa Utaalamu unazidiana wewe ukijuwa hiki mwengine anajuwa kile Mimi ni Mtaalam wa mambo ya nyota ASTROLOGY, SECURITY FOR COMPUTER, psychology (Saikolojia) na witch doctor (Madawa ya kienyeji) na kidogo hayo mambo ya wanyama kuhusu huyo Kaka kuona ninavyoelewa mimi huwa anatokea kwa nadra sana mijini na kwa imani za Wazee wetu wa kizamani huwa akitokea huyo Kaka kuona huwa wazee wanamuanglia anavyoonekana na husema kuwa akitokea huwa kama huo mwaka akitokea utakuwa na baraka sana ya Mvua na mazao shambani na mambo mengine muhimu kwa wanadamu inategemea katokea mjini gani au sehemu gani ndipo watu husema akitokea hubashiri mema au mabaya inatemegea imani za watu wa huo mji aliyotokea huyo kaka kuona asante sana Paka jimmy leo nimeamuwa kukueleza ujuzi wangu mimi Mzizi Mkavu XPASTER amesema kweli nampongeza kwa maneno yake. http://images.google.com.tr/images?hl=en&rlz=1B3GGGL_enTR352TR352&q=Pangolins&um=1&ie=UTF-8&ei=3mX7SvdF3KCMB6eDmYgF&sa=X&oi=image_result_group&ct=title&resnum=4&ved=0CCAQsAQwAw
   
Loading...