Baraka zinatoka kwa wazazi, lakini pia baraka huibiwa

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,553
2,992
nimesoma bibilia katika sura/ kitabu cha nyakati nimeona historia ya mtume Yakoubu/ yakubu na eze ambae ni kaka wa yakoubu, bibilia inaonesha kwamba Isaac/ Is-haka baba wa yakubu na aze alikuwa ni mwenye mapenzi na mtoto wa kwanza kutoka kwa mkewe Rebecca ambaye ni eze lakini Rebecca alimpenda sana yakoubu, kipindi cha uzee wa Isaac alimuita mwanawe mkubwa na kumuomba akamuwindie mnyama na kipindi atakaporudi atampa baraka.

Bahati mbaya Rebecca akasikia kuhusu hili naye akamwambia mwanaye mdogo afanye hima kuchukua kondoo na kumuandalia baba yake msosi na divai ili apate baraka ya baba ake ukweli alifanikiwa kuipata na historia inaonesha yakoub ndiye alikuwa kiongozi wa taifa huku kaka yake akiwa msaidizi wake.

Hivyo tunakumbushana kuwa watu tusome lakini bila kusahau kufanya dua na sala kwa wingi kujiombea ili kuepuka kuishi kwenye kiatu kisicho chako.
 
Back
Top Bottom