utandawazi wito ..........wanaogopa dhuluma wengi risiti hawaifadhi.
wadau huwa mimi nashindwa kuelewa utakuta mtu anaenda kutoa PESA kwenye ATM. Akishamaliza anaanza kuzihesabu. Hivi hata kama akizukuta zimepungua/ ongezeka atafanya nini wakati huo Bank inakuwa imeshafungwa.
Na huwa inakera zaidi maeneo ya mikoani yaani umesimama kwenye foleni halafu kila anayeingia anakuwa anafanya kamchezo hako bila kuzingatia kuna foleni kubwa inasubiri huduma.
Sijaelewa na huwa najiuliza bila majibu mtu kuanza kuhesabu pesa baada ya kutoa kwenye ATM.
Naomba wenzangu kama mna mawazo tofauti.
Ukiingia kwenye chumba cha ATM kuna tangazo linasomeka 'HESABU FEDHA ZAKO KABLA HUJAONDOKA'. Kwahiyo waliloliweka ni wajinga?
nimesha shuhudia mtu kaomba hela ikamuhesabia na pesa haikutoka ikatoa risiti kuthibitisha kwamba pesa kesha chukua,mtu atakaye fuata hapo au hata baada ya watu kazaa akapewa pesa zaidi ya ile ailiyoomba
Gosh!!! Kama benki imeshafungwa sasa hapo sijui ndo inakuwaje!!
hivi unaweza uka justify vipi kwamba pesa yako imepungua au imeongezeka once umeshaitoa kwenye mashine na ATM receipt inaonyesha imetoa fedha taslimu
ukikuta zimepungua utamhakikishiaje afisa wa benki kwamba pesa zimepungua kwa ATM na si janja yako
siyo rahisi kihivyo mkuu