Hivi huu udwanzi wa 'Cover' kauleta nani?

Mbn hata wasanii wakubwa wanaotunga nymb zao hufanya cover z wasanii wengine m nafkiri nimapenzi tu
 
Naona vijana wanaibuka kwa kasi kutengeneza kava badala ya kuutumia mda huo kutengeneza hits zao, huu ni uduanzi, kama kweli nyie ni wasanii si mtengeneze hits zenu? Yaani unakaa unaskilizia staa fulani atoe wimbo ili 'usafirie nyota' yake upitie mgongo wake, dah vijana wa sikuhizi wanapenda dezodezo, hii spidi ya kava naiona kabisa itafikia wakati redioni kava zinakuwa nyingi kuliko nyimbo original. Mi nnavyoelewa kava zilikuwepo tangu enzi hizo, ila zilikuwa zina maana kubwa, hasa ilikuwa ni kwa ajili ya kuwaenzi ma'legend', mfano Brandy na Ray J walivyofanya another day in paradise ya Phil Collins, Jide alivyofanya Muhogo wa Jang'ombe ya Bi Kidude, Mr. Paul alivyofanya Zuwena ya Marijani, n.k, na nnavyoelewa hizi kava zilikuwa zinafanyika baada ya wimbo original kuwa umeshatoka miaka mingi, hiyo ina make sense, but hii ya kutoka baada ya mwezi mmoja hata hainiingii akilini. Halafu cha ajabu media zinasapoti huu ujinga, hapo ndo naamini kwamba media zinachangia kuua mziki. Nyie wasanii na Media acheni huu uduanzi aisee!
Huo udwanzi wa cover watakuwa wameuleta wadwanzi tu.
 
Mbona cover ni kitu cha kawaida huku bongo ndo tumesikia now.
Kasikilize cover ya helo wa Adele akiuimba JOE THOMAS
 
All of me - John Legend, reggae cover ya Iyah Cure ni nzuri sana.
 
nami nampango wa kuandaa cover za nyimbo ambazo kombA alimuimbia bb wa taifa pale taifa wakat wa kumuaga
 
Kuna Cover na Parody....ila huku kwetu (bongo) naona kama hakuna utaratibu maalumu, matokeo yake kila anayeibuka anafanya kile anachotamani.

Sijui sheria zetu za haki miliki zinasemaje ila nijuavyo kufanya Cover mtu unahitaji kufanya makubaliano maalum na wanaomiliki haki za wimbo husika....eidha kwa malipo au bure...ni juu yenu.

Tofauti na Parody ambayo hufanywa kwa lengo la kutania/kuchekesha kwa kutumia mirindimo, melody inayofanania ila lyrics ni za kwako...na kwa maeneo mengi huwa sio lazima kupata ruhusa ya mwenye haki miliki ya wimbo.
 
Kwani inatakiwa original ukae muda gani ndio ifanyike COVER,ili isiwe "udwanzi" ?????????
 
Yule jamaa alieshinda milioni 50 Kule BSS alafu hela yake yote akaenda kununua motokaa yeye kagoma kabisa kutoa nyimbo zake kila siku anadondosha Cover tu naona hivi karibuni ataweka na housing kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom