Hivi huu ni utu jamani?

Hii ni kielelezo cha wazi kwamba training ya jeshi letu la mgambo inahusisha misuli tu na sio ubongo.
 
Huo ni ynyama na ushenzi na unyanyasaji usio mfano.

Nnnatoa mwito binafsi ya kuwa mkuu wa mkoa awajibike au awajibishwe mara moja na wakuu zake na akikataa kuwajibika wakikataa kumuwajibisha basi wananchi tuingie mitaani kuandamana kushikiza kuwajibishwa kwake.
 
Dar nakuunga mkono. Mimi naomba wana JF wote tuungane kuhusu hili. Si mara ya kwanza hawa askari wa jiji wanafanya hivi!.
 
Dar nakuunga mkono. Mimi naomba wana JF wote tuungane kuhusu hili. Si mara ya kwanza hawa askari wa jiji wanafanya hivi!.

Don't hold your breath! JF hatuna mpango na masuala ya jamii! Ingekuwa UFISADI, SIASA AU SHUTUMA ZA NGONO ungeona ambavyo tungechangamkia. Ndio maana wengi wanafungua thread kwenye Jukwaa la Siasa. Mia tatu kwenye siasa hapa kwako takhriban ishirini! Hatuna interest.
 
Inasikitisha kuona utu wa binadamu unashushwa kwa visingizio kama hivyo,

Hali kama hizi ndizo zinazojenga kisasi na chuki dhidi ya mgambo na wamachinga na mama ntilie.
Halmashauri ya jiji inatakiwa kulitupia au kuingilia kati nidhamu au mafunzo ya mgambo wao na kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali pale wanapokiuka haki za wananchi.
La sivyo hapa watu wanaweza kujichukulia sheria wenyewe ya kulipiza kisasi

Lakini pia najiuliza, kwamba hakuwa hata na bukta au ch*pi ndani? si kawaida ya vijana wa kibongo kuvaa suruali tu, au walizitoa zote?
 
Heshima mbele wanaJambo!! Leo katika pitapita zangu mtandaoni nilikutana na hii kule kwa Michuzi Junior blogspot:

http://michuzijr.blogspot.com/2008/03/sio-sawa-hata-kidogo.html

Kwa kweli nimeshawaona hawa jamaa wakifanya kzi ni hatari na kuna unyanyasaji wa hali ya juu.... Hivi watu wa haki za binadamu mpo humu ndani? KWa sasa ukiwa Dar karibu kila mtu amekuwa touched na hawa jamaa (ndugu, jamaa, rafiki, jirani au hata kuona hadharani) watu wakipigwa eti sababu wanajaribu kutetea vibiashara vyao kidogo, au kutetea gari lake lisivutwe nk nk nk.... Kwa kweli tunahitaji hili kumulikwa kwani pale karibu na St Joseph ukikuta kina Mama Ntilie wapo kwenye kesi ya kutetea vichache vyao inatia hasira, uchungu na wakati mwingine unatamani kupiga watu vichwa pale mahali!!

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu tubariki waTanzania...........
 
Wakuu na mimi niliiposti hii kule kwenye Hoja Nzito sikujua kuwa huku napo ipo... Nahdani Mods wataiondoa ile kule na kuieleta huku....

Kwa kweli mimi nimeshakutwa na hawa jamaa wakifanya mambo yao kwa vijana wa mjini ni unyama usiokuwa na kifani... Eti hawa ndio trained Mgambo kwa kazi mbalimbali, nadhani ningependa nijue hizi training mpya zina faida gani kwa jamii sababu hata kule Kiteto wakati wa kampeni waliokamatwa walikuwa ni "Traind militiamen - MGAMBO"........ Muungwana, tunaomba uweke jicho hapa sababu ni kuumiza baadhi ya wananchi......

Mungu atubariki!!!
 
Don't hold your breath! JF hatuna mpango na masuala ya jamii! Ingekuwa UFISADI, SIASA AU SHUTUMA ZA NGONO ungeona ambavyo tungechangamkia. Ndio maana wengi wanafungua thread kwenye Jukwaa la Siasa. Mia tatu kwenye siasa hapa kwako takhriban ishirini! Hatuna interest.

You are right FM.

Binafsi nimenotice hicho (hiko?) kitu. JF masuala ya jamii hayana kipaumbele, ila SIASA.....ah, mahala pake. Na kwa wengine kama Mimi ambao hatufancy Siasa huwa tunaachwa nje most of the time. Inasikitisha, but well.............., we live to see.
 
Hapa ndo utashangaa kwanini watu wanaendelea kuchagua CCM ambayo imewafikisha wananchi kwenye utumwa wa namna hii. Zile ajira milioni moja sijui zimeyeyukia wapi, na wafanyakazi wengine ndo wanaendelea kupunguzwa. Jiji la Dar limekuwa n watendaji wabovu siku zote kwani hawa mgambo wanavunja sheria kila siku lakini hawafanywi kitu. Hawa wafanya biashara za mkononi hawana kosa kabisa wanatafuta kula vinginevyo kuna jeshi litatengenezwa ambalo madhara kama ya KENYA KIBERA yatakuja kutukumba na TZ. Hivi jiji halina kitengo cha R&D???????
 
Kwa kweli hii inasikitisha, kitu kikubwa alichokuwa anafanya yule kijana ni kutafuta riziki kwa njia ya halali kabisa. kama wao kweli wanajua sheria kwa nini hawaendi kupambana na MAFISADI ambao wanafisidi nchi na maisha yetu?????.

Hapa kweli ndio utaona matabaka yale ambayo kiongozi wetu muasisi hayati Mwalimu nyerere aliyapiga vita kwa nguvu zote, mafisadi wanaachiwa wanaishi maisha ya kifahari katika MAHEKALU yao kwa gharama ya jasho letu, wale ambao wanatafuta riziki kwa njia ya halali ndio wananyanyasika.

.....kuna mafisadi wengine nasikia wameanza kurudisha fedha zetu walizoiba BOT, kweli mwizi anaiba ikisha anarudisha halafu inakuwa basi kweli hapa nanusa mchezo wa kulindana
 
Zile ajira milioni moja sijui zimeyeyukia wapi, na wafanyakazi wengine ndo wanaendelea kupunguzwa

Mkuu wa kaya alisema ATATOA ajira million moja,
vijana walikuwa wanajadili maana ya hii kauli 'KUTOA AJIRA', waka konclude kuwa kutoa ajira maana yake ni kupunguza ajira (wakati ule wa sakata la machinga kusafishwa posta)

Nafikiri hiyo ndiyo ilikuwa tafsiri sahii ya HE JK kuwa atatoa=kupunguza ajira million 1.
 
Hivi jamani mi naomba niulize? hivi kuna mtu yeyote mwenye takwimu za wamachinga wapo wangapi dar na kwa mwaka wanapungua au kuongezeka kwa silimia ngapi? ukiwatoa mama lishe na wengineo?
Hivi,serikali inashindwa nini kuwajengea masoko au vibanda maalumu hawa jamaa mathalani huko Tandika na kwingineko ambako mwisho wa siku wamachinga wote watakuwa na maeneo ya kufanyia biashara na ushuru watalipa.Kama kwa siku tunaweza kuwalipa watu hewa milioni 152 je tungejenga masoko mangapi?
Cha ajabu serikali yetu badala ya kununua viwanja nje ya mji wakajenge wizara,wenzetu wanazidi kuzijaza wizara kati kati ya mji.Hivi wizara kama ya elimu ile ingekuwa dodoma au hata kule kimara kuna ubaya gani? lazima iwe karibu na ofisi ya Rais? wizara ya usalama wa raia ilyovunjwa kulikuwa na haja gani ya kuchomeka jengo pale katikati palipobana,hivi kule boko hakuna nafasi? au pugu road? matokeo yake tunalalamika msongamano wa magari mjini na zaidi ya hapo tunalalamika wamachinga tukiwaambia waende kigogo sambusa hawataki,wakati wakuu wetu serikalini hawataki kwenda boko.
 
Nimepata taarifa kuwa kijana huyu kajivua nguo, je ni kweli, manake othewise kaumiza sana hisia zetu
 
huwa naajiuliza sana, hivi hawa mgambo wanapata wapi hiyo jeuri ya kutenda unyama huu? mi naona kuna umuhimu wa kupitia upya hizi taratibu za kuwapata vijana kwaajili ya kujiunga na jeshi hili. vitu kama elimu, akili ya mtu na maisha yake kwa kipindi kilichopita vinapaswa kuangaliwa kwa umakini wa hali ya juu sana vinginevyo tusijeulizana nani aliweka jiwe hadi tukajikwaa mambo yatakavyop kuwa kama kenya, haiingii akilini mtu mzima mwenye akili timamu tena mtanzania akatenda unyama kama huu. hawajamaa ni akam wameagizwaau kuna sheria yao inayowalinda kufanya mambo ya kihuni kama haya. KAMA VIPI HIKI KIKOSI KIFUTWE KABISA.
 
Mimi ninaona tukianza kuujadili huu uvundo, historia yake itakuwa ndefu kidogo.Lakini nawaomba nigusie kidogo wana JF wengine watanisaidia kunirekebisha endapo nitakuwa nimekosea.
Ni takriban miongo minne tangu tuupate uhuru wetu. Wakati tunapata huo uhuru wetu kulikuwa na mwamko mkubwa wa vyama vya ushirika na ninaweza kusema vilikuwa vinaendeshwa kwa umakini na uaminifu mkubwa. Vyama hivi vilikuwa ndio chachu kubwa kabisa ya kumuondoa mkoloni. Pamoja na hayo wakulima walipata pembejeo,mafao kutokana na kilimo chao pamoja na misaada mingi na hata hao mafisadi mnaowasikia leo kama sio hivyo vyama vya ushirika kuwasomesha sijui wangekuwa wapi.

Mwl.Nyerere wakati huo aliyaona hapa sitaki kumkosoa muasisi wetu Mungu amuweke mahali pema peponi.Mwl. alikuwa na mtazamo tofauti aliona endapo vyama hivi vikiendelea ukabila utashamiri kwa kasi kwani wakati huo nchi ilikuwa changa sana na akaamua kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa hivi vyama viwe vinasimamiwa na kuratibiwa na serikali.
Hapa sasa ndipo ufisadi ulipoanza rasmi kwa sababu wale ambao Mwl. aliwaamini kwamba wangemfanyia kazi ndio wakaanza kuvifilisi vyama vyetu vya ushirika mpaka vikakosa muelekeo na wakulima nao wakapoteza imani yao pamoja na uzalishaji kuzorota.
Umaskini uliokithiri ukawa umevikumba vijiji vyetu na badala yake wao wakawa ndio wazalishaji wakuu wa mazao ya vyakula mijini pamoja na mambo mengi. Kama ukisoma Vitabu Vya Issa Shivji From Peasant....... to.....Sikumbuki vizuri utakubaliana nami.
Sasa vijana wetu huko vijijini nao wakakosa kabisa muelekeo kutokana na uduni wa maisha ulivyokuwa umekithiri pamoja na kuporomoka kwa elimu. Kutokana na kutokuwa na mzunguko wa hela wenye uhakika kama uluvyokuwa wakati ule enzi ya vyama vya ushirika visivyokuwa na mafisadi. Vijana wakaona njia ya pekee ya kujikwamua na umaskini wao ni kuja mijini hususan Dar es salaam. Sasa hali ikaendelea hivi miaka na miaka mpaka sasa hawa viongozi wetu wameshindwa kuidhibiti na matokeo yake ni matumizi ya nguvu kwa kutumia mgambo wa jiji. Mimi nasema hata hao mgambo wenyewe ni njaa tupu hawakutakiwa kuja mijini. Na ndio maana misemo ya tutabanana hapahapa si migeni kuisikia masikiono mwetu.
Sasa hoja yangu ni kwamba kama serikali inataka kukabiliana na suala la umachinga kwanza ianze kujisafisha yenyewe kutokana na uvundo uliopo manake hauna ubani huo au pafyumu kwa lugha nyepesi, pili iboreshe kilimo hasa vijijini pamoja na vyama vya ushirika vitakavyosimamiwa na wananchi wenyewe,Tatu sekta ya madini sio chanzo cha kuondoa umaskini viongozi wetu walikurupuka ila kilimo ndio uti wa mgongo kama uongo kamuulize fisadi au msomi yeyote kasomeshwa na hela za nani achana na vijana kama sisi wa siku hizi uliza wale wazee wetu, Maisha bora kwa kila mtanzania hayaji kwa kuvuana nguo hadharani na kudhalilishana bali yanakuja kwa nia na vitendo thabiti vitakavyowashirikisha wananchi wetu katika maamuzi mabalimbali ya serikali kuanzia chini mpaka juu bila kujali rangi,itikadi,dini na ukabila,mwisho Tanzania sio nchi maskini ila ni sisi wenyewe ndio tunauendekeza umaskini kutokana na fikra tunazojengewa na hawa mafisadi.
LAKINI YOTE HAYA YANA MWISHO.
 
Huo ni ynyama na ushenzi na unyanyasaji usio mfano.

Nnnatoa mwito binafsi ya kuwa mkuu wa mkoa awajibike au awajibishwe mara moja na wakuu zake na akikataa kuwajibika wakikataa kumuwajibisha basi wananchi tuingie mitaani kuandamana kushikiza kuwajibishwa kwake.

..utakuwa sio "mwenzao" mara moja! jaribu uone!
 
You are right FM.

Binafsi nimenotice hicho (hiko?) kitu. JF masuala ya jamii hayana kipaumbele, ila SIASA.....ah, mahala pake. Na kwa wengine kama Mimi ambao hatufancy Siasa huwa tunaachwa nje most of the time. Inasikitisha, but well.............., we live to see.

..lizy,

..wajumbe wana uhuru wa kuchangia hoja wanazoona zinawavutia na kuwatia hamasa. sasa,mambo ya ufisadi si madogo. lakini hiyo haimaanishi haya mengine hayana maana. ni mtazamo wa mtu tu.

..wewe na fundi mnapochangia hili mnakuwa mko sawa kabisa! na wengine nao wako sawa pia,kwa kutochangia!
 
Pumbavu sana nyie Mgambo,
Nyie Hamna akili kabisa, mnampiga mtu anatafuta riziki kwa jasho yake na mnawaacha Mafisadi wanatanua tu hapo Dar es salaam?
Maskini wewewee, mungelijua mnatumika kama chombo tu, Kama mnaweza kupiga na kushughulikia mambo mbona mnawaacha waliotuibia Fedha zetu Kibao, Kwani hamju yalipo maviwanda ya Patel?, amzijuzi shell za Alex masawe????
Kuweni na akili nyie, tumieni busara zenu kidogo, najua shule yenu sana sana ni darasa la saba ndo maana, ila tumieni hata akili ya kuzaliwa basi
Mimi nina hasira sana wana JF, yaani kuibiwa tunaibiwa na Viongozi, sasa tukipitisha karanga tunauza tunapigwa, hii ndo Tanzania gani sasa

Tehe, tehe, Baba H punguza munkari ndugu yangu- Mgambo wetu hawaingii humu, labda huu ujumbe uutume kwenye magazeti ya KIU na UWAZI ndo watakupata.
 
..lizy,

..wajumbe wana uhuru wa kuchangia hoja wanazoona zinawavutia na kuwatia hamasa. sasa,mambo ya ufisadi si madogo. lakini hiyo haimaanishi haya mengine hayana maana. ni mtazamo wa mtu tu.

..wewe na fundi mnapochangia hili mnakuwa mko sawa kabisa! na wengine nao wako sawa pia,kwa kutochangia!

Nilikuwa nina'state' the obvious. Kila mtu ana haki na uhuru wa kuchangia anapopenda. Kinachonisikitisha ni kuwa hii ni symptomatic kwa jamii yetu. naamini kuwa hatutaweza kuwa na mafanikio ya dhati bila kujali masuala ya jamii. Siasa ni tool tu ya kufanikisha haya. Haya yote yanayotokea sasa hivi ni mfano wa jamii inayoelekea ICU! Lakini hayo ni mawazo yangu tu. hivi vi'petty tyrants' vinatamba kwa sababu wanajua kuwa deep down hatuna mpango nao. Ni kitu ambacho tumekikubali kijamii pamoja na machozi yetu ya mamba.
 
Back
Top Bottom