Hakuna utu au ubinadamu bila dini

Hakuna utu au ubinadamu bila dini

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
929
Reaction score
1,500
Habari ndugu zangu. Wakubwa shkamoo......
Ushawahi kujiuliza maisha yangekuwaje bila Dini?

Leo nimewaza nikawazua na kuangalia mifano iliyohai kuhusu uhusiano uliopo kati ya mtu kuwa na roho ya utu au ubinadamu na Dini. Baada ya uchunguzi wa kina nimegundua bila Dini ubinadamu na utu vita toweka kabisa Duniani na hatutakuwa na tofauti na wanyama .

utu ni ile hali ya kutenda jambo kwa mwingine bila ya kutegemea malipo yoyote kutoka kwake. Hivyo ni jumla ya tabia njema anazopasa kuzionyesha mtu kwa jamii (hulka ya matendo mema). Source Wikipedia

Sasa Kwanini nina amini bila Dini ubinadamu au utu vitatoweka ? .

Sababu ya kwanza. Tumaini la maisha baada ya kifo. Bila dini hakuta kuwa na imani ya kuwa na maisha baada ya kifo.
Hii itaachia wengi walioshika dini kufanya maasi wakijua wote sisi mwisho ni kaburini . Bila shaka tungeuwana hovyo sana na kuumizana . Wengi wanaokamatwa kwa mauaji hukamatwa baada ya kuzubaa kutokana na dhamiri zao kuwa kinyume na walichotenda na hii ni sababu ya imani ya kidini. Bila dini hata sheria zisingeweza kuzuia watu Machafuko yangekuwa mengi sana . Mali zingepiganiwa mara 100 kuliko hivi sasa. Dini ikipotea kabisa ndani ya vichwa vyetu magenge ya mapigano yatakuwa mengi kuliko haiti [emoji1122] na nchi nyinginezo na ndio itakuwa namna ya kujilinda na kuweza kuishi kwa nchi nyingi.
Jiulize kwa hasira zako kama sio kuwa mcha Mungu mangapi mabaya ungetendea wengine haswa waliokukasirisha.
Bila ubinadamu na utu unaoletwa na Dini hakuna ulinzi utakaotosha kukulinda .

Sababu nyingine . Matukio mabaya kwenye jamii zilizo acha Dini. Bila kwenda mbali hebu fanya utafiti wako kwa kulinganisha mikoa ambayo dini imetamalaki sana na sehemu ambazo dini haieleweki imekaaje kwenye eneo hilo . Angalia takwimu za matukio kadiri muda unavyokwenda kutoka nchi za magharibi ata Asia kadiri wanavyozidi kuziacha dini matukio yanaongezeka au yanapungua?. Pia pitia historia kabla hizi dini mbili Ukristo na Uislamu kushika sana Dunia hali ilikuwaje . Mara nyingi vita kupinduana kwa mauaji vilishamiri kuliko hivi sasa na sasa ujuaji unataka kuongezeka tena . Dini zinaanza kuonekana ni ushamba kwa wasomi haina shida wao watapita salama ila ni hatari sana kwa vizazi vijavyo.

Njia salama ya kumwokoa mwanao na tabia hatarishi ni kumnywesha itikadi kali ya Dini.
Ukimwacha aje achague mwenyewe utampoteza kwani bila imani za dini basi hata ushoga na tabia chafu nyinginezo mashiko ya kuzipinga hayatakuwepo .
Maana ukigusia uumbaji tu lazima utagusa Dini. Ukisema tumetokana na sokwe sasa unampangia mtu kuwa unavyotaka wewe ili nini unamzuia asiwe shoga ili nini wakati wote tutaishia kaburini . Bila imani ya maisha baada ya kifo inakuwa sababu nyingine hazina nguvu. Itikadi kali ya dini itamlinda mwanao na kumpa Amani hata anapopitia magumu kiasi gani watu wote wampinge bado ataishi akiamini kuna Mungu.

Mwisho tusiache Dini ni ulinzi wa kizazi chetu na vizazi vijavyo.

Wewe unaonaje Dunia bila Dini ingekuwaje?
 
Ingekuwa poa kwani dini zina vitisho vya vitu visivyoonekana. Ni kama utumwa, mf. Kutoa sehemu ya kumi ya pato lako ni utumwa. Omba kwa kutumia mizimu yako na kitabu chako kitakatifu kiwe ni katiba ya nchi. Uwe tu na imani kuwa "usimtendee mtu kitu ambacho hutaki utendewe ".
 
Ni kweli dini zinafundisha maadili, tabia njema, utu na maisha ya kila siku kwa ujumla.
Na kabla ya ujio wa Dini watu walikuwa wanaisha maisha haya haya na kulikuwa na sheria zao pia
Kwa mfano kuna watu huko Amazon wanaitwa Warí hawa wanakula wageni na wenyeji pia
Wanakula wageni kama kitoweo, na wanakula wenyeji wao kwa wao kama watatenda kosa kubwa kama wizi wa mifugo

Kuhusu Utu na Ubinadamu kwa kweli hata sisi ni mashuhuda unakwenda vijijini ndani kabisa hawajui dini na wanaishi kwa mila zao, lakini ukienda kwao wanakukirimu zaidi ya wenye dini zao

Sipingani na wewe ila wapo wenye Utu na Ubinadamu lakini hawana dini
 
Luka 18:

“Watu wawili walipanda
kwenda hekaluni kusali, mmoja alikuwa
Farisayo na mwingine mkusanya kodi.
Yule Farisayo akasimama na kuanza
kusali akisema moyoni, ‘Ee Mungu,
ninakushukuru kwa sababu mimi si kama
watu wengine—wanyang’anyi, wasio
waadilifu, wazinzi—au hata kama
mkusanya kodi huyu. Mimi hufunga
mara mbili kwa juma; ninatoa sehemu ya
kumi ya mapato yangu yote.’ Lakini
yule mkusanya kodi alikuwa amesimama
mbali kidogo na hata hakutaka kutazama
mbinguni, bali alijipigapiga kifuani
akisema, ‘Ee Mungu, nihurumie mimi
mtenda dhambi.’ Ninawaambia, mtu
huyu alishuka kwenda nyumbani akiwa
mwadilifu mbele za Mungu kuliko yule
Farisayo. Kwa sababu kila mtu
anayejiinua atafedheheshwa, lakini yeyote
anayejinyenyekeza atainuliwa.”
 
Habari ndugu zangu. Wakubwa shkamoo......
Ushawahi kujiuliza maisha yangekuwaje bila Dini?

Leo nimewaza nikawazua na kuangalia mifano iliyohai kuhusu uhusiano uliopo kati ya mtu kuwa na roho ya utu au ubinadamu na Dini. Baada ya uchunguzi wa kina nimegundua bila Dini ubinadamu na utu vita toweka kabisa Duniani na hatutakuwa na tofauti na wanyama .

utu ni ile hali ya kutenda jambo kwa mwingine bila ya kutegemea malipo yoyote kutoka kwake. Hivyo ni jumla ya tabia njema anazopasa kuzionyesha mtu kwa jamii (hulka ya matendo mema). Source Wikipedia

Sasa Kwanini nina amini bila Dini ubinadamu au utu vitatoweka ? .

Sababu ya kwanza. Tumaini la maisha baada ya kifo. Bila dini hakuta kuwa na imani ya kuwa na maisha baada ya kifo.
Hii itaachia wengi walioshika dini kufanya maasi wakijua wote sisi mwisho ni kaburini . Bila shaka tungeuwana hovyo sana na kuumizana . Wengi wanaokamatwa kwa mauaji hukamatwa baada ya kuzubaa kutokana na dhamiri zao kuwa kinyume na walichotenda na hii ni sababu ya imani ya kidini. Bila dini hata sheria zisingeweza kuzuia watu Machafuko yangekuwa mengi sana . Mali zingepiganiwa mara 100 kuliko hivi sasa. Dini ikipotea kabisa ndani ya vichwa vyetu magenge ya mapigano yatakuwa mengi kuliko haiti [emoji1122] na nchi nyinginezo na ndio itakuwa namna ya kujilinda na kuweza kuishi kwa nchi nyingi.
Jiulize kwa hasira zako kama sio kuwa mcha Mungu mangapi mabaya ungetendea wengine haswa waliokukasirisha.
Bila ubinadamu na utu unaoletwa na Dini hakuna ulinzi utakaotosha kukulinda .

Sababu nyingine . Matukio mabaya kwenye jamii zilizo acha Dini. Bila kwenda mbali hebu fanya utafiti wako kwa kulinganisha mikoa ambayo dini imetamalaki sana na sehemu ambazo dini haieleweki imekaaje kwenye eneo hilo . Angalia takwimu za matukio kadiri muda unavyokwenda kutoka nchi za magharibi ata Asia kadiri wanavyozidi kuziacha dini matukio yanaongezeka au yanapungua?. Pia pitia historia kabla hizi dini mbili Ukristo na Uislamu kushika sana Dunia hali ilikuwaje . Mara nyingi vita kupinduana kwa mauaji vilishamiri kuliko hivi sasa na sasa ujuaji unataka kuongezeka tena . Dini zinaanza kuonekana ni ushamba kwa wasomi haina shida wao watapita salama ila ni hatari sana kwa vizazi vijavyo.

Njia salama ya kumwokoa mwanao na tabia hatarishi ni kumnywesha itikadi kali ya Dini.
Ukimwacha aje achague mwenyewe utampoteza kwani bila imani za dini basi hata ushoga na tabia chafu nyinginezo mashiko ya kuzipinga hayatakuwepo .
Maana ukigusia uumbaji tu lazima utagusa Dini. Ukisema tumetokana na sokwe sasa unampangia mtu kuwa unavyotaka wewe ili nini unamzuia asiwe shoga ili nini wakati wote tutaishia kaburini . Bila imani ya maisha baada ya kifo inakuwa sababu nyingine hazina nguvu. Itikadi kali ya dini itamlinda mwanao na kumpa Amani hata anapopitia magumu kiasi gani watu wote wampinge bado ataishi akiamini kuna Mungu.

Mwisho tusiache Dini ni ulinzi wa kizazi chetu na vizazi vijavyo.

Wewe unaonaje Dunia bila Dini ingekuwaje?
Dini zilitungwa ili kutawala wanadamu kwa kuwatia hofu na kuachana na maovu - so in this case you are right.
 
Historia inatufunza kwamba vita nyingi , mauaji makubwa , ukatili mkubwa katika historia umefanywa kwa mgongo wa dini na imani.

Hata ukisoma vitabu vitakatifu utakubaliana na mimi kuna mauaji mengi sana kwa mgongo wa dini na imani. Sasa ni juu yako kutumia akili kama dini ndio inasababisha mauaji na ukatili au ukosefi wa dini.
 
Vita vya dini na dini ndio tatizo lakini kwa sasa tumeunganishwa na Dini zilizobeba idadi kubwa sana ya watu tofauti na miaka ya nyuma . DINI ZILIKUWA NYINGI SANA, MFANO NI KILA KABILA TANZANIA NA MILA ZAKE AU DINI YAKE ALAFU KILA MOJA LIJIONE BORA ZAIDI NA UTU UWE NI NDANI TU YA KABILA VITA SI ITAKUWA KILA SIKU.

KADIRI DINI ZINAVYOWEKWA KANDO NDIVYO MAASI YANAZIDI
 
Utu na dini vinaweza kuwa na uhusiano lakini si lazima kwasababu maadili ni asili ya kibinadamu.huruma,upendo haki ni sehemu ya asili ya binadamu na hata hivyo vinaweza kufundishwa kupitia elimu au Jamil
 
Back
Top Bottom