ETUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 2,795
- 4,881
Tahadhar: Huu Uzi Una Sauti kubwa mno kama upo very sensitive pita Kulia!
Naona baadhi yetu huenda tumejikuta humu Kwa bahati mbaya Sana,hatuendani na hii platform ambayo imejipambanua kama sehemu yenye watu wenye akili kubwa au maono makubwa Kwa taafsiri isiyo rasmi.
Ukimuona mtu anachangia mada bila kusoma Uzi husika hivi huyu unamuweka kundi gani kama sio Darasa la Tatu B? Hawa ni wapuuzi wakubwa Sana,tena bila aibu anasema kabisa sijasoma huu Uzi au sijasoma wote,sasa kama hujasoma unapata wapi haki ya kuchangia kitu ambacho hukijui? Nyie ndio ambao huwa mnajibu mitihani bila kufuata instruction,Kwa maana nyingine hamjui mnacho fanya.
Yani unachangia mada kutokana na ufahamu wa mtu mwingine na sio wako wewe,je huyo ambaye umeona comment yake Una uwakika gani nae sio Darasa la Tatu B kama wewe? Je Una uwakika nae kaelewa mada au nae hajamaliza kusoma kama wewe? Kama sio upumbavu ni nini?
Humu ndani huwa hatujadili mtu na mara nyingi tunajikuta tunajadili udini,hii ni aibu Sana kwakweli,na hasa ikitokea ima Sheikh au Mchungaji/Padri kafanya makosa kama yeye na sio kama taasisi,lakini tulivyo wapumbavu kama ni Sheikh tutaanza kuutukana Uislamu mwanzo mwisho na kama ni Mchungaji/Padri tutaanza kuutukana Ukristo mwanzo mwisho, kama sio upumbavu ni nini? Kwanini asijadiliwe mtu husika na sio dini yake? Je Uislamu na Ukristo ndio umemtuma huyo mtu kufanya aliyoyafanya?
Kuna wapumbavu wengine ili mada zao zipate wasomaji wengi basi ni lazima Uislamu utukanwe,na kwakuwa watu wengi humu wamelishwa matango Pori kuhusu Uislamu wanajikuta katika upumbavu ule ule wa mtoa mada,ni aibu kwakweli tena Sana,wengine Kwa chuki ambayo imetokana na uelewa mbaya basi huleta hata Maandiko feki ilimradi Tu wazidishe uasi wao dhidi ya Dini ambayo hata haielewi mafundisho yake. Je nikiwaita nyie ni Wapumbavu wakubwa nitakosea?
Na waislamu vile vile tunaingia katika upuuzi huo huo,kwanini uendelee katika mjadala WA kipuuzi,unachoweza kufanya jibu hoja kama kuna ulazima WA kufanya hivyo, lakini ukiona unayejadiliana nae anaendekeza upuuzi cha Busara kwako piga kimya tu. Kuendelea kujadiliana na mtu kama huyo Kwanza ndo mnawafanya wazidi kuleta mada za kipumbavu na vile vile Kitabu chako kinakukataza kufanya mijadala ya kipuuzi.
Matusi yamekuwa sehemu ya jamii forums, kuwa na Utambulisho bandia hakukupi nafasi ya kutukana watu usio wajua,Sana Sana unatupa nafasi ya kujua tunajadiliana na mtu WA namna gani,kauli yako yatosha kujua Tabia zako na maono yako,wajanja watakupuuza mapema Sana, na ambao ni Wapumbavu kama wewe watakusapoti pia.
Unakuta mtu anamtukana mtu Kwa matusi makubwa kabisa akihusisha viungo vya uzazi vya mama yake, Yani hata kutaja hapa naogopa ndio maana nimetumia viungo vya uzazi vya mama yake. Unajiuliza hivi huyu ni mtu wa namna gani,mbona hana ustaarabu,mbona ni mpumbavu namna hii,mpo wengi tu humu. Unafaidika na nini ukitukana,je inakufanya ujisikie vizur? Nikiwaita nyie ni Wapumbavu nakosea?
Kuna nyuzi nyingine sio lazima uchangie,kuna nyingine zipo nje ya uwezo wako na uelewa wako,cha kufanya na ambacho ni cha Busara pita kimya kimya na ujifunze Kwa wachangiaji wengine,nyuzi nyingine huenda haziendani na maadili yako sio vibaya ukapita Kulia utakuwa salama zaidi. Kuliko kutaka kuchangia kila kitu matokeo yake unatuonyesha ulimbukeni wako na upumbavu wako.
Always jitahidi Sana kuchota Busara kutoka Kwa wanajukwaa wengine,hii itakusaidia Sana katika Maisha yako ya kila siku,na Busara ni kuliweka kila Jambo Mahala pake.
Nawapenda Sana!
Ni hayo Tu!