Hivi hiki ni kitenzi kishirikishi?

jesacho

Senior Member
Mar 2, 2015
115
13
wanafunzi WALIKUWA shambani.

naomba kujua kama kweli neno WALIKUWA ni kitenzi kishirikishi au la
 
wanafunzi WALIKUWA shambani.

naomba kujua kama kweli neno WALIKUWA ni kitenzi kishirikishi au la
wanafunzi walikuwa wanalima shambani
-walikuwa --> kitenzi kisaidizi
-wanalima --> kitenzi kikuu
~ kitenzi kishirikishi ni "kama" "na" na mengineyo, yaani haioneshi kitendo.
 
sasa ukisema kitenzi kisaidizi ni lazima kuwe na kitenzi kikuu ....mbona hakuna kitenzi kikuu hapo ...nikitenzi kisaidizi kivip
 
sasa ukisema kitenzi kisaidizi ni lazima kuwe na kitenzi kikuu ....mbona hakuna kitenzi kikuu hapo ...nikitenzi kisaidizi kivip
wewe ndo hujaiweka sentesi yako vizuri, sababu mtu atakuuliza walikuwa wanafanya nini hawawezi kuwa huko bila sababu, utajibu walikuwa wamekaa/wanalima nk, hapo ndipo kinapoingia kitenzi kikuu
 
wanafunzi WALIKUWA shambani.

naomba kujua kama kweli neno WALIKUWA ni kitenzi kishirikishi au la
Wanafunzi WALIKUWA shambani. Neno walikuwa ni kitenzi kikuu.

Tatizo ninaloliona hapa watu mnakariri neno kuwa hutumika Kama aina fulan, ukitumia kanuni hyo utachizi, ila ili ujue neno fulani limetumika Kama aina fulani shughulika na sentensi husika.
 
wanafunzi walikuwa wanalima shambani
-walikuwa --> kitenzi kisaidizi
-wanalima --> kitenzi kikuu
~ kitenzi kishirikishi ni "kama" "na" na mengineyo, yaani haioneshi kitendo.
Mbona umetunga sentensi yako?? Yeye ameuliza "wanafunzi walikuwa shambani"

"Walikuwa" ni aina gani ya maneno?
 
Wanafunzi WALIKUWA shambani. Neno walikuwa ni kitenzi kikuu.

Tatizo ninaloliona hapa watu mnakariri neno kuwa hutumika Kama aina fulan, ukitumia kanuni hyo utachizi, ila ili ujue neno fulani limetumika Kama aina fulani shughulika na sentensi husika.
Wewe kama ni mwl lazma watoto wafeli, mimi sio mwalimu lakini najuwa umekosea
 
Kitenzi kitenzini...
Kitenzi kikuu ni Messi..kitenzi kisaidizi ni Neymar..na kitenzi kishirikishi mtamalizia wenyeweeeeee...
 
Ni kitenzi kishirikishi .Kwa kawaida sarufi haina formula maalum
mf:mtoto alikuwa nyumbani-hapo inaonyesha(t)
2:Mtoto alikuwa anataka kucheza-hapo ni(Ts)+(Ts)
3:Mtoto anacheza(T)
 
ni kitenzi kishirikishi maana aina hii huonyesha uyakinishi au kinyume chake, kwa hiyo neno Alikuwa limeonyesha kukubali kinyume cha Hakuwa ambacho ni kishirikishi kinachokanusha
Yaap. Ni kitenzi kishirikishi; kingefuatana na kitenzi Kikuyu ndio kingekuwa kitenzi kisaidizi. Upande wa sentensi IPO sawa.
 
Ni kitenzi KISAIDIZI.
Sentensi hiyo haijakamilika kwa sababu sifa kuu ya sentensi ni lazima itoe taarifa kamili.
Unaposema "wanafunzi walikuwa shambani" sentensi haijakamilika, wapaswa kukamilisha walichokuwa wanafanya huko shambani ambacho ndo kitakuwa kitenzi kikuu.
 
daah!

inasikitisha sana watu hawajui kiswahili.

kitenzi kisaidizi kikiwepo lazima na kitenzi kikuu kiwepo!

mfano wa vitenzi vishirikishi:

mtoto yu mgonjwa.
embe li bichi.
hapa pa pachafu.
juma ndiye mtoto.
nguo si chafu.
mimi ni mkubwa.
mti u mkavu.
kisahani ki kisafi.
nguo i mpya.

au,

juma alikuwa mkulima.

mtoto anaonekana mjinga.

siku zote;

kitenzi kishirikishi kinafuatwa na nomino.

kitenzi kisaidizi kinafuatwa na kitenzi kikuu

mfano:

baba alikuwa angali analisha.
alikuwa=kitenzi kisaidizi.
angali=kitenzi kisaidizi.
analisha=kitenzi kikuu.

au,

baba alikuwa angali malishoni.
alikuwa=kitenzi kishirikishi.
angali=kitenzi kishirikishi.
malishoni=nomino.

au,

baba alikuwa mkulima.
alikuwa=kitenzi kishirikishi.
mkulima=nomino.

au,

baba alikuwa analima.
alikuwa=kitenzi kisaidizi.
analima=kitenzi kikuu.

NB:KITENZI KISAIDIZI HUTOKEA PALE TU AMBAPO KITENZI KIKUU KINAHITAJI USAIDIZI.

NOMINO HAZIHITAJI USAIDIZI WA KITENZI KISAIDIZI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom