Hivi hii ni ishara ya kunichoka au?

mke wangu anatabia mbaya hata kama anajua nimetoka kazini nimechoka akiniona tu baada ya muda ni hata kama anajua nimechoka hakuna kupeana pole kwa uchovu yeye atakachofanya ni kuanza kuniuliza maswali ya ajabuajabu mfano leo tunapika nini wakati hela ya chakula nimemuachia sasa sijui nikimjibu pika chochote anaanza kufoka sijui lengo lake nini naombeni ushauri wazee wa jukwaa.



kama unamwachia pesa ndogo,af usikute mwanamke mwenyewe ni mama tuh wa nyumbani

then haumpi kitu chochote cha yeye kujishughulisha nacho,kama biashara au ujasiriamali wa aina yoyote akinunia na kukuuliza maswali ya mkato mkato kama hayo mimi sion kosa lake kbs

tujifunze kuwatunza wake zetu nao watutunze
 
Hapa kuna kitu kimoja naweza kukusaidia ndugu....
Punguza hasira na jazba za uchovu wa kazi...
Kuulizwa nini utakacho kula ni kwa kuwa wewe ndiye mlaji. Ni swali la kawaida sana na ndio maana ukifika hotelini huwa ndio swali la kwanza.

Sasa kwani amerudi hotelini? binafsi hilo swali silipendi kabisa na bahati nzuri siku hizi siulizwi. Mke anatakiwa awe mbunifu afikirie chakula kitakacho mfurahisha mmewe, sio unarudi sa tatu usiku halafu ndo unaulizwa utakula nini.
 
Sasa kwani amerudi hotelini? binafsi hilo swali silipendi kabisa na bahati nzuri siku hizi siulizwi. Mke anatakiwa awe mbunifu afikirie chakula kitakacho mfurahisha mmewe, sio unarudi sa tatu usiku halafu ndo unaulizwa utakula nini.

Mbona ukiulizwa tufanye style gani mimacho huwa yakutoka kama umeongezwa mshahara!!!
Kuna wanaume wengine wapo so selective mkuu...ole wako umpikie furu wakati ye ajisikia kula kibua
 
Back
Top Bottom