Tuishi nao kwa akili

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
14,375
14,870
Wakuu salaam.

Hebu tujadili hii kauli ya "tuishi nao kwa akili" ilivyokaa.

Mtu kama kafuga na kuishi na nyoka au hata mnyama mkali kama chui, simba nk ukimuuliza ni kwa namna gani ameweza kufuga na kuishi na hao wanyama aghalabu miongoni mwa majibu atakayo kupa ni kwamba; "nawafuga na kuishi nao kwa akili (tahadhari)", kwa jibu hilo inaonyesha wazi kwamba bila kutumia akili bila shaka maisha ya huyo mfugaji yatakuwa hatarini kutokana na hao wanyama.

Tukirudi kwenye msemo unaonukuliwa mara nyingi unaosema kwamba; Tuishi nao (wanawake) kwa akili, je hii sio dharau na udhalilishaji kwa wanawake??-- hii, kwa mawazo yangu, ni sawa na kuwaweka wanawake katika kundi la viumbe hatari mithili ya Nyoka nk. Wanawake ni mama zetu, dada, shangazi nk na hata tunashuhudia mwingine leo hii ni mkuu wa nchi yetu pendwa Bongoland, je naye tuishi naye kwa akili??

Naam, sikatai moja kwa moja kwamba hakuna wanawake wa kuishi nao kwa akili lakini pia tusikatae kwambo wapo pia wanaume wa kuishi nao kwa akili, tena hao ndio wengi zaidi, si ndio hao wamepeleka pesa China!!😏

Mimi nadhani huyo muhenga aliyetunga hiyo kauli siku hiyo aliudhiwa na mkewe ndipo akaamua ku generalise kauli hiyo kwa wanawake wote.
 
Mbona unaumia sna na huo msemo Kwan na wewe ni mwanamke!? Kama ndiyo basi pole dada kwa kufananishwa na wanyama wakali.
 
Mimi mnanichoshaga mnaposema wanawake ni mama zetu, dada zetu sijui shangazi zetu mbona wao hawasemagi wanaume ni baba zetu, kaka zetu wajomba wetu?
 
Mimi mnanichoshaga mnaposema wanawake ni mama zetu, dada zetu sijui shangazi zetu mbona wao hawasemagi wanaume ni baba zetu, kaka zetu wajomba wetu?
wajinga ndiyo wanaopigwa siku zote na misemo ya ovyo
 
Mimi mnanichoshaga mnaposema wanawake ni mama zetu, dada zetu sijui shangazi zetu mbona wao hawasemagi wanaume ni baba zetu, kaka zetu wajomba wetu?
Shida ni kila jambo baya hutupiwa mwanamke hata kama jambo hilohilo afanye mwanaume mfano Mwanamke akiwa mzinifu ataitwa malaya, changudoa nk lakini mwanaume yeye ataitwa Kijogoo au Rijali, shababi nk, hapo utaona jinsi gani wanawake wanavyokandamizwa na jamii ya kiume.
 
Back
Top Bottom