Hivi Hazina wanamuogopa DG wa PPF? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Hazina wanamuogopa DG wa PPF?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by mchukiaufisadi, Sep 21, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  PPF ni shirika la Umma kwa ajili ya kukusanya michango ya wanachama wake, kuiwekeza na kisha kuwalipa kwa usahihi wastaafu. Kumekuwa na matukio mbalimbali ya ukosefu wa uadilifu ndani ya huu mfuko hasa baada ya ERIO William kupewa wadhifa huo na mjomba wake William Mkapa bila aibu.

  1. Wafanyakazi wa mashirika ya umma inatakiwa wewe wale wa masharti ya kudumu na pensioni. Kabla ya 2003, ndivyo walivyokuwa.
  2. Mwaka 2003 waliamua kubadili ajira zao na kuwa za mikataba. Kwa uhalisia wa taratibu, mfanyakazi wa ajira ya mkataba mfupi hulipwa gratuity pale anapoondoka kazini mkataba ukiisha. Huyu hastahili kuchangiwa michango ya pensioni (15% kwa mwezi)
  3. kwa kuwa Hazina wamelala, huku wakijua wanapuuza Waraka wa UTUMISHI waliendelea kujilipia gratuity 25% na pension 15% hadi leo.
  4. Mwaka 2008, wakajilipa kila mmoja gratuty ya 25% kwa miaka mitatu, group endowment 47% ya mishahara yao wakati huohuo wanaendelea kuchangiwa pension.
  5. Mwaka 2010 DG alijilipa gratuity 25% na Endowment 47% ya mishahara ya miaka yote.  Hili limefanyika wakati Hazina wamegoma kusaini mkataba wa PPF wa Hali bora maana umejaa ufisadi na uizi kwa wanachama.
  6. Mwaka 2011, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ya Mh. Zitto Kabwe, iliagiza wakurugenzi wa PPF wasilipwe Group endowment mpaka CAG afanye ukaguzi, kwa dharau kubwa, DG Erio kawalipa na wanaendelea na kazi.
  7. Baada ya kuona malengo yao ya kujichukulia malipo ya group endowment kabla ya kustaafu yamefanikiwa, wamejirudisha kwenye ajira ya kudumu mwaka huu.

  Hivi kweli Msajili wa Hazina anafaida gani kwa umma? Kama wanaweza jiamulia mambo makubwa kama haya bila ya yeye kujua, bado Waziri wa fedha anamuhitaji?

  Hivi ni sahihi mtu mmoja ambaye mshahara wake ni mkubwa (appro 10M) kwa mwezi achangiwe na PPF karibu 87% ya milion kumi kila mwezi kutokana na fedha za wavuja jasho?

  Naomba kuwasilisha kwa Great Thinkers tu. Kama sio Great Thinker please usichangie.

  ============
  Moderator's comment:

  Tumeifunga hoja hii kutokana na wachangiaji kuingiza masuala binafsi, hata hivyo mamlaka husika wakiwemo PCCB na POAC zimetumiwa nakala ya mjadala huu.

  JF isitumike kama attacking tool, tunatoa ushirikiano pale lugha ya uwasilishaji inapokuwa ya kiungwana.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu... pension funds are very powerful, especially under the current government
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,978
  Trophy Points: 280
  Dg ni mtu wa Kikwetee. Mind you!!!!!!!!!!!!!
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Majungu si mtaji!
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  So what? Even Lowassa was.
   
 6. n

  nambala New Member

  #6
  Sep 22, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeyasoma maandishi ya ndugu yangu,nimejiridhisha kwamba mwandishi ni sawa na fungu la kukosa,amewasilisha kilio cha malalamiko kupata huruma asiyostahili,akijazilisha hoja zake kwa maneno mengi yasiyokuwa na chembe ya ukweli,mimi ntamjibu hoja kwa hoja,nikitumia uzoefu wangu katika uhudumu wa mifuko mbalimbali ya jamii nchini na nje ya nchi yetu,KWANZA-ni kweli kwamba,wafanyakazi wa mashirika ya umma wanapaswa kuwa chini ya masharti ya kudumu na pensionable,na katika hoja hii,ni vema nikamfahamisha mwandishi na wadau wa fikra pevu kwamba,dai la mwandishi lilishatekelezwa mda kitambo yapata mwaka wa pili sasa,na hii ni baada ya sheria inayounda mashirika ya umma kwa mfuko wa ppf kubadilishwa na kurudi kwenye utaratibu wake wa awali kama ilivyokuwa mpaka mwaka 2003,kuileta hapa kama hoja mpya,ni kuvia fikra na kutaka kuaminisha umma wa wanafikra vitu vya uongo na uzushi kwenye jambo linalohitaji majibu ya fact badala ya maoni binafsi ya mwandishi au mlalamikaji.-kwa sasa nadiliki kuliita dai hili la mwandishi mlalamikaji kama dai lisilo na mashiko.

  Mbili:-hoja au dai la pili la mwandishi ni dai mufilisi,mwandishi anashindwa kujua kwamba,hoja au nia ya malipo ya gratuity,sii hoja ya mtu binafsi kuja nayo mfukoni,maamuzi yote ya malipo katika ajira za ppf kama tunavyotaraji kuwa katika mifuko mingine ya jamii huamuliwa na bodi ya mfuko wa ppf,sii busara wala hekima,kutoa zigo la tuhuma kwa mtu,katika maamuzi ambayo yeye ni mjumbe tu,ikumbukwe kwamba bodi ya ppf,inaundwa na watu wengi na wenye uwezo na uzoefu katika nyanja mbalimbali,tena wakitoka maeneo mbalimbali ya kikazi,ikiwemo uwakilishi wa muhimili wa bunge,wizara ya fedha na taasisi nyingine za kiserikali,dg wa ppf,anakuwa sehemu tu ya wajumbe,na inapolazimu mambo mengine huamliwa atoke nje ya kikao husika ili wajumbe wa bodi wawe huru zaidi katika kujadili afya ya mfuko wa ppf,ikiwemo malipo ya wafanyakazi wanaomaliza mikataba yao ya mda mfupi na mrefu,ushahidi upo wazi,ppf imekuwa mstari wa mbele kuwalipa mafao wafanyakazi wake pindi wanapofikia tamati ya mikataba yao ya utumishi kwa wakati muafaka,na ndio maana hakuna mahala ppf imewahi kulalamikiwa na wafanyaklazi wanaomaliza mikataba yao kuwa eti hawajalipwa inavyostahili,haya ni maneno na maono binafsi ya mwandishi au mlalamikaji huyu,nadiriki kuyaita majungu ya ofisini,ambayo kwa tanzania ni sehemu ya maish-itoshe tu kusema mwandishi au mlalamikaji ana hoja dhaifu,anajaribu kupaza sauti isikike.

  HOJ YA TATU-nianze tu kwa kusema hasidi hakosi sababu kama msemo wa kiswahili unavyotufunza,ni kejeli na uwongo wa mchana kweupe kusema eti hazina imelala,na kufumbia macho kupuuzwa kwa waraka wa utumishi-kwa taarifa tu,ppf-kama nilivyosema awali inaundwa na bodi,dg ni mjumbe,hazina ni mdau wa bodi,bunge lina uwakilishi katika bodi hii,wizara ya fedha ina uwakilishi,kwa pamoja wajumbe wa bodi walijiridhisha na kuidhinisha malipo ambayo ndugu yangu anayalalamikia,katika maamuzi yanayomgusa dg,bodi humuondoa nje kikao mkurugenzi ili kuwa huru kujadili jambo linalohusu maslahi yake kwa uhuru,wanabodi walijiridhisha wakaidhinisha malipo,nimwombe mwandishi awe muungwana kukubaliana na maazimio ya bodi ya mfuko badala ya kumalizia kinyongo chake kwa ndugu dg,bodi ilipitisha malipo ya watumishi,haiojalishi watakuja wa majina gani,leo ni erio,kesho atakuja saiboki,au atakuja manka,ni vema wanafikra pevu,tufunzane kujadili mifumo kuliko kujadili watu.maana kwa maazimio ya bodi ya ppf,hata mwandishi wa malalamiko haya akipata nafasi ya erio kuwa dg,atalipwa kwa maelekezo haya ya bodi,narudia kumshauri,aandike hoja mantiki na sii hoja nyongo.

  HOJA YA NNE,-Hapa nimsaidie mwandishi,kumchangia mtumishi asilimia au gawio kat ika pension yake ,ni haki ya msingi kwa mwajiriwa,naamini iwe ppf au katika eneo lingine la ajira,haijalishi ni kiwango gani cha mshahara mtumishi analipwa,katika hili,mwandishi ameonyesha kinyongo cha kupitiliza kwa anaowatuhumu,narudia kumpa ushauri wa bure,mwandishi,malipo ya ppf-yanamlenga mtumishi katika ngazi fulani,ama dg,au mkurugenzi au mkuu wa kitengo,hayalengi jina la mtu,hata kama ni yeye ataaji
   
 7. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MKUU JINSI ULIVYOJIBU NAHISI KAMA WEWE NDO MHUSIKA HASWAAAAAAAAAAAAAA.
  Sasa si mkae ofisini kweny myamalize hayo?
   
 8. M

  Ma Tuma Senior Member

  #8
  Sep 22, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yamerukwa mavi umekanyagwa uharo.
   
 9. n

  nambala New Member

  #9
  Sep 24, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BUBE- mimi sii muhusika, nimemjibu kama mdau wa utumishi katika mifuko ya hifadhi, hapa kwenye social media ni mahala pa kufunzana, ni mahala ambapo mtu anapata shule au darasa la bure na wakati mwingine wengi wetu tumefaulu hata usaili wa kazi sababu ya mafundisho ya hapa jf, sii kazi tu, hata mafundisho ya jinsi ya kukaa katika jamii.

  Eneo hili fikra pevu ni eneo nyeti sana, ni vema kulinda heshima yake, tusiligeuze kuwa jamvi la wapiga soga za upotoshaji kwa intrest binafsi, isiwe mahala pa mtu kuja kumalizia hasira na nyongo yake ya ofisini, tusipafanye mahala hapa pa kuja kuondolea stress.

  Mdau mchukia ufisadi ame kuja na upotoshaji kwenye mambo ya msingi, maana hata sheria za mifuko yote nchini zipo wazi, asome nssf, lapf, ppf, gepf, pspf, asome mlinganisho wa kanuni na taratibu zake, halafu apate majibu ya hii topic yake.

  Huu ni umaskini wa akili ambao mwanafikra pevu mwenzetu anayeheshimika duniani baba wa taifa mwlimu nyerere aliupinga waziwazi, kwamba umaskini wa akili ni umaskini mbaya kuliko wote duniani,kumjadili mtu kwa nyongo na kuacha kujadili issues. Ni kutowatendea haki wanaotusoma, simjui huyu mtu anaitwa Erio, bali nafahamu sheria za ma-dg wa mifuko ya hifadhi hivyo kama anauchukia ufisadi kweli ni vema atuhamasishe wanafikra pevu kuupinga mfumo unaowapa haki ya kulipwa hayo anayoyalalamikia kuliko kujadili kumchukia mtu.

  Maana kwa taratibu za mfumo wa ppf, hata akitoka Erio ambaye ni dg, akaja mchukia ufisadi kuwa dg wa ppf, taratibu zinampa haki ya kulipwa haya anayoyaandika hapa kwa kuyapinga, unless muhusika awe na maslahi binafsi ya chuki na huyo Erio, lakini kama kweli ni mpambanaji wa kweli dhidi ya ufisadi, apambane kuondoa sheria zinazoruhusu malipo, nami nambala nipo tayari kumuunga mkono. Vinginevyo tutatukana watu hapa bure, wenye akili watatupuuza.

  NAMBALA
   
 10. M

  MUSHONO New Member

  #10
  Sep 24, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  oya mchukia ufisadi kama umefukuzwa kazi ppf , tafuta kwingine,mambo ya majungu kama haya sii inshu wala nini,mimi ni mpinga majungu kwa sana yani,au mshikaji dg alikuchukulia mkeo nini,maana unachana mistari ambayo ni full kinyongo yani,tafuta inshu kwingine bwana,majungu yatakubakiza masikini wakati wadau wanasonga hatua mbele.
   
 11. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Mwisho waelewa tuta okota chembechembe za madini kwenye hili tope zito. Inaelekea kunakitu kinacho hitaji uchunguzi wa kina. Ningepata picha nzuri endapo mtu mwengine haswa wadau wakongwe wenye nafasi hiyo ya kufanya huo uchunguzi waliangalie kwa undani swala hili. Kwenye ''majungu/umbea'' katikati yake njia ya ukweli hupatikana.

  Kemea ufujaji wa pesa za walalahoi waa TZ popote paale ulipo bili kuweka mbele kujuana wa ubinafsi wala majungu.
   
 12. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  NAPENDA KUKUJIBU KAMA IFUATAVYO:

  PENYE RED:

  Erio aliingia madarakani kwa hila ambazo zilifanikishwa na mjomba wake Mkapa.

  1.Elimu: Masters ya sheria, sina tatizo,
  2.Uzoefu: Desk officer TLS up to May 2000, june 2000 PPF Legal Officer na Katibu wa Bodi (hana assistant), 2003-2005 PPF Head of Legal Unit supervising one staff and a secretary, 2005 Sept, Director General PPF, supervising 200 staff and more than 100,000 members. Hapa ndio tatizo hana leadership skills na uzoefu
  3. Katibu wa Hazina by the Mgonja, aliandaa dokezo kwenda kwa Waziri kuwa Mr. Nsemwa anapendekezwa kuendelea kuwa DG PPF kwa kipindi cha pili. Dokezo likiwa mezani kwa Waziri, Erio akajua maana alikuwa aifuatilia sana hiyo nafasi. Akamtumia mama mmoja pale Hazina mwenye cheo kikubwa, akachukua faili na kurudi nalo kwa Mgonja na kumshawishi kuwa nafasi itangazwe ili kumpata DG. Kama mjuavyo, hata Adam wa kale alishawishiwa na Hawa. Tangazo likatolewa.
  4. Interview ilikuwa ifanywe na PWC, badala yake shabiki mkuu wa Erio, Marehemu Elvis Musiba akasimamia ili kuhakikisha aliyekuwa DG wa wakati huo hapiti maana angekuwa threat kwenye hila zao. PWC wanajua vema na hawakufurahishwa na hili ndio maana baada ya kupewa maelekezo kuwa lazima Nsemwa ashindwe kwenye mchujo walikataa kusimamia na kupewa Musiba.
  5. Interview ya pili aliongoza mtu mmoja wa TRA (DF) akafuatiwa na DF wa PPF, erio alikwa wa TATU.
  6. Mapendekezo ya Waziri wa Fedha Mramba (yalikuwa ya shinikizo la .....) yakampendekeza Erio ambaye ni wa tatu kuwa apewe na Mjomba mtu hakutia ajizi akampa.

  TUJIULIZE Baada ya miaka mitano kuisha, mbona interview hazikuitishwa tena? Kama kweli hakuingia kwa hila kwa nini amekuwa mtu wa visasi?

  Mara alipoingia madarakani akapanga kuwaondoa ndani ya miezi mitatu tu ya u-DG Chenza, Mjinja na Osca Sikauka Mwachanga (alikufa na CHARGES bila kuzijibu) hatimaye alifanikiwa maana hao waliobaki hai mmoja aliondoka na wa pili alitengeneza njama.

  NAOMBA UJIBU HAYA MACHACHE ILI NIKUANIKE ZAIDI.
   
 13. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  BW/BI NAMBALA

  NAPENDA KUKUJIBU KAMA IFUATAVYO KWENYE RANGI YA BLUE KWENYE POST YAKO:

  TUJIULIZE Baada ya miaka mitano kuisha, mbona interview hazikuitishwa tena? Kama kweli hakuingia kwa hila kwa nini amekuwa mtu wa visasi?

  Mara alipoingia madarakani akapanga kuwaondoa ndani ya miezi mitatu tu ya u-DG Chenza, Mjinja na Osca Sikauka Mwachanga (alikufa na CHARGES bila kuzijibu) hatimaye alifanikiwa maana hao waliobaki hai mmoja aliondoka na wa pili alitengeneza njama.

  NAOMBA UJIBU HAYA MACHACHE ILI NIKUANIKE ZAIDI.
   
 14. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Re: Mfuko wa PPF kuna ufisadi, wizi na uzinzi, na unyanyasaji wafanyakazi

  [​IMG] By sexon2000 [​IMG]
  (c) muda wake ulipoisha akaja mdada mwingine kutokea bank fulani kwenye kitengo alichobuni na kumpa umeneja. Sasa hivi anatengenezewa mazingira ya kuwa kurugenzi. Huyu mdada hatulii ofisini (pccb wanaweza kagua akaunti yake ya travelling imprest) nje ya nchi kwake ni kama kwenda kariakoo. Kila dg akienda safari nje ya nchi lazima awemo.


  Sasa kapewa ukurugenzi wa Risk bila interview. Erio atajibebea begi lake la huyu sub-single kama kawa. Kweli PPF hakuna utawala Bora, ukurugenzi bila interview? Watu wakichungulia ndani basi wanapewa ukubwa. Toka 1978 hii ni mpya. Erio atasema anataka gender balance and equality kama utetezi.

  Kwa kuwa lilisemwa sana, alitakiwa kuwa na mshipa wa aibu japo kidogo. Angetengeneza interview fake angalau kufunika kidogo.
  . ... nh
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...