Hivi haya maisha mpaka lini jamani?

Hivi haya maisha mpaka lini jamani?

Mkuu pole sana i can feel hali unayopitia sasa hivi,

Hayo ndo maisha piga moyo konde nyanyuka juu pambana,

Pambana kwa ajili ya kizazi chako pambana kwa ajili ya familia yako,

Usikate tamaa mkuu, kama inawezekana hata habari za kutembea na mi CV achana nayo tafuta njia nyingine ya kukupa mkate iwe halali lakini
 
Mkuu pole sana i can feel hali unayopitia sasa hivi,

Hayo ndo maisha piga moyo konde nyanyuka juu pambana,

Pambana kwa ajili ya kizazi chako pambana kwa ajili ya familia yako,

Usikate tamaa mkuu, kama inawezekana hata habari za kutembea na mi CV achana nayo tafuta njia nyingine ya kukupa mkate iwe halali lakini
Ahsante mkuu kwa kunipa moyo na ushauri wa kujenga kabisa matumaini mapya
 
Unaweza fungua banda la tuition ukawapa madin watoto

Sent from my 1201 using JamiiForums mobile app
 
Wengi wanakufa masikini kwa kusubiri kuajiliwa

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app
 
Wewe umeanzisha mradi gani,maana hata mradi pia kuanzisha ni pesa kama bado hana pesa ya kuanzisha mradi atafanyaje?maana pesa zote yawezekana walitumia kumsomesha wakijua kunasiku atatoka,mradi wako ulionzisha wewe unaweza kumpa kazi?

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
Haaaa haaaa aisee jamaa umenena swala la mradi ni pesa tena
 
Habari za majukumu wana jf wote..
Nina matumaini mu wazima wa afya njema na kwa wale wagonjwa mungu awasaidie muwahi kupona..

Back to the point..
Mimi nikijana wa kiume mwenye umri wa miaka 26
Nina degree moja(B.A education from udsm)
Nimemaliza chuo mwaka 2015
Nilipokuwa mdogo wazazi wangu walinisisitiza sana juu ya elimu na mara kwa mara walinikaripia na hata kunichapa kabisa pindi ninapoleta uzembe shuleni..
Wazazi wangu waliujua sana umuhimu wa elimu japo wao hawakubahatika hata kuingia darasani kwenye maisha yao..
Mamaangu hajui kusoma wala kuandika lakini humdanganyi chochote kuhusu kuyafahamu masomo kwa majina sijui biology sijui geography yote kaisha yakalili.... pia anazijua division zote kuanzia one mpaka zero na points zake.. Bila kusahau comb zote PCM, HGL etc... anazijua..
Wazazi wangu wanaamini elimu ni ufunguo wa maisha na mtu akifanikiwa kusoma automatic atakuwa na maisha bora..
Sasa ni mwaka wa pili tangu nimalize chuo bila mafanikio yoyote ya kupata kazi..
Nimetuma maombi mpaka shule za primary za English medium lakini hata kuitwa tu kwenye usaili imekuwa ni ndoto..
Nafkiri nimetuma maombi karibu shule zote za private za wilaya yangu kuanzia secondary mpaka primary
Nimezunguka sana kutafuta kazi narudia tena Nimezunguka sana lakini sijaambulia chochote..
Lakini cha ajabu watu wanao kuja nyuma yangu kuomba kazi sehemu hizo hizo hupata tena wengi wao hata GPA nimewazidi na masomo ni yale yale kama yangu..
Kuna kipindi namdanganya mama kwamba kuna sehem nimeitwa kwenye interview ili angalau afarijike then naamka asubuhi sana naenda kukaa sehemu tulivu kisha narudi nyumbani jioni...
Nilijaribu kuwauliza wenzangu waliofanikiwa kupata kazi ila majibu yao karibu wote walikuwa na watu wa kuwashika mikono na wengine walihonga kabisa pesa ili wapate kazi..
Kuna kipindi nahisi mawazo yananizidi mpaka naongea pekeangu..
Sina mtu wa kunishika mkono wala pesa ya rushwa kazi ntapata vipi???
Kama kuna boss yoyote atakae soma huu uzi namuomba aache kutoa kazi kwa upendeleo na ubaguzi maana huu mfumo huu unatuumiza sana watoto wa maskini..
Ili upate kazi mpaka utoe hela wakati tunafuta kazi ili tupate pesa tusaidie na sisi wazazi wetu...
Just imagine kama na wewe mtoto wako anateseka kutwa nzima kubeba zege ili atoe saport kwa familia... alafu zinatoka nafasi za kazi ananyimwa ili apewe mtoto wa tajiri alietoa million utajisikiaje?? Hivi ndivo familia za wanyonge zinavoumia na huu mfumo wa pesa na kujuana...
Hali ya kukata tamaa kuna kipindi inakuja lakini najipa moyo kuwa hali hii itapita tu maana mungu anatupenda wote kwa kiwango kimoja na hana upendeleo....
RUSHWA NI ADUI WA HAKI NA INATESA SANA VIJANA WANYONGE WASIO NA UWEZO KIFEDHA WALA NDUGU MABOSI...
ewe boss mpokea rushwa na unaetoa nafasi kwa ndugu zako tu wakati nafasi ni kwa watanzania wote kaa ukijua mungu anakuona na hapendi hivo..


Ahsanteni
Kuna fursa ishajitokeza upande wa 2 kuna mdau anatafta customer/accounts mwnye deploma ama degree Avatar yake sijui anajiita nani tena ukimpata unijuze.

Sent from my SM-J120F using JamiiForums mobile app
 
Usife Moyo mambo itakuja kua nzur tu..halaf we unaona miaka 2 muda mrefu ila tambua wako wenzako kama wewe wana miaka hata 5 No Job.but usijali
Mkuu tuliopitia hii hali tunajua nilikuwa napitia uzi huu actually nimenyong'onyea sana

Wazazi hawajui hali iliyopo kwenye soko la ajira wao wanajua ukimaliza tu shule hasa elimu ya juu kazi moja kwa moja

Ila kutokata tamaa ndio msingi wa ushindi

Mungu ni wetu sote
 
0k anajiita Kevoo 27 yuko na hio fursa..Changamka baba'angu.

Sent from my SM-J120F using JamiiForums mobile app
 
Kuna fursa ishajitokeza upande wa 2 kuna mdau anatafta customer/accounts mwnye deploma ama degree Avatar yake sijui anajiita nani tena ukimpata unijuze.

Sent from my SM-J120F using JamiiForums mobile app
Poaaaaaa mkuu
 
Jianjiri mkuu. Kuna shughuli nying tu ata ukianzisha kimgahawa

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
 
Jianjiri mkuu. Kuna shughuli nying tu ata ukianzisha kimgahawa

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
Tatizo mtaji mkuu kama ningekuwa na hela ningekuwa na kazi maana ningetoa rushwa kupata kazi
 
Achana na jina la dracular Linakuletea mikosi, wazazi wako ni watu wa Mungu sana, makuzi uliyo lelewa na pia sala za wazazi wako haziendani na ushetani na unyonyaji damu
Bujibuji aisee nimejaribu kubadili user name ila nimeshindwa hebu twende pm u nielekeze...
 
Wengine toka 2012 tupo mtaani and life linasonga, ni marufuku kukata tamaa, ni kukomaa mpk kieleweke
 
Dont give up, Bring it on..[emoji1491]


Ukimaindi natuma tena.
 
Jiite baracuda

Sent from my G7-L01 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom