Hivi haya maisha mpaka lini jamani?

Hivi haya maisha mpaka lini jamani?

dracular

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Posts
770
Reaction score
1,075
Habari za majukumu wana JF wote,

Nina matumaini mu wazima wa afya njema na kwa wale wagonjwa Mungu awasaidie muwahi kupona..

Back to the point..
Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 26 nina degree moja(B.A education from UDSM) nimemaliza chuo mwaka 2015.

Nilipokuwa mdogo wazazi wangu walinisisitiza sana juu ya elimu na mara kwa mara walinikaripia na hata kunichapa kabisa pindi ninapoleta uzembe shuleni.
Wazazi wangu waliujua sana umuhimu wa elimu japo wao hawakubahatika hata kuingia darasani kwenye maisha yao.

Mama yangu hajui kusoma wala kuandika lakini humdanganyi chochote kuhusu kuyafahamu masomo kwa majina sijui biology sijui geography yote kaisha yakariri pia anazijua division zote kuanzia one mpaka zero na points zake. Bila kusahau comb zote PCM, HGL etc anazijua.

Wazazi wangu wanaamini elimu ni ufunguo wa maisha na mtu akifanikiwa kusoma automatic atakuwa na maisha bora. Sasa ni mwaka wa pili tangu nimalize chuo bila mafanikio yoyote ya kupata kazi.

Nimetuma maombi mpaka shule za primary za english medium lakini hata kuitwa tu kwenye usaili imekuwa ni ndoto. Nafikiri nimetuma maombi karibu shule zote za private za wilaya yangu kuanzia secondary mpaka primary,
nimezunguka sana kutafuta kazi narudia tena nimezunguka sana lakini sijaambulia chochote.

Lakini cha ajabu watu wanao kuja nyuma yangu kuomba kazi sehemu hizo hizo hupata tena wengi wao hata GPA nimewazidi na masomo ni yale yale kama yangu. Kuna kipindi namdanganya mama kwamba kuna sehemu nimeitwa kwenye interview ili angalau afarijike then naamka asubuhi sana naenda kukaa sehemu tulivu kisha narudi nyumbani jioni.

Nilijaribu kuwauliza wenzangu waliofanikiwa kupata kazi ila majibu yao karibu wote walikuwa na watu wa kuwashika mikono na wengine walihonga kabisa pesa ili wapate kazi. Kuna kipindi nahisi mawazo yananizidi mpaka naongea peke angu. Sina mtu wa kunishika mkono wala pesa ya rushwa kazi nitapata vipi?

Kama kuna boss yoyote atakae soma huu uzi namuomba aache kutoa kazi kwa upendeleo na ubaguzi maana huu mfumo huu unatuumiza sana watoto wa maskini. Ili upate kazi mpaka utoe hela wakati tunafuta kazi ili tupate pesa tusaidie na sisi wazazi wetu.

Just imagine kama na wewe mtoto wako anateseka kutwa nzima kubeba zege ili atoe saport kwa familia alafu zinatoka nafasi za kazi ananyimwa ili apewe mtoto wa tajiri alietoa million utajisikiaje? Hivi ndivo familia za wanyonge zinavoumia na huu mfumo wa pesa na kujuana. Hali ya kukata tamaa kuna kipindi inakuja lakini najipa moyo kuwa hali hii itapita tu maana Mungu anatupenda wote kwa kiwango kimoja na hana upendeleo.

RUSHWA NI ADUI WA HAKI NA INATESA SANA VIJANA WANYONGE WASIO NA UWEZO KIFEDHA WALA NDUGU MABOSI. Ewe boss mpokea rushwa na unaetoa nafasi kwa ndugu zako tu wakati nafasi ni kwa watanzania wote kaa ukijua Mungu anakuona na hapendi hivo.

Ahsanteni
 
Pole saaana mkuu, wahenga walisema aliye nacho huongezewa...

Mtangulize Mungu kwenye kila jambo, yeye ndo hufanya njia pasipo na njia...

Halafu unaweza kufanya hata vishughuli vya kujiajiri wakati ukisubiri kuajiriwa
 
Usife Moyo mambo itakuja kua nzur tu..halaf we unaona miaka 2 muda mrefu ila tambua wako wenzako kama wewe wana miaka hata 5 No Job.but usijali
 
wazazi wako ni watu wa Mungu sana, makuzi uliyo lelewa na pia sala za wazazi wako haziendani na ushetani na unyonyaji damu
Uwiiiiiiiii haaaa haaaa daaah Bujibuji bana hili nickname tu la jf...
 
Usife Moyo mambo itakuja kua nzur tu..halaf we unaona miaka 2 muda mrefu ila tambua wako wenzako kama wewe wana miaka hata 5 No Job.but usijali
Ahsante mkuu kwa kunipa moyo nashukuru sana
 
Usikate tamaa endelea kupambanaa....one day mambo yatakunyookea.

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Pole saaana mkuu, wahenga walisema aliye nacho huongezewa...

Mtangulize Mungu kwenye kila jambo, yeye ndo hufanya njia pasipo na njia...

Halafu unaweza kufanya hata vishughuli vya kujiajiri wakati ukisubiri kuajiriwa
Ahsante mkuu kwa kunipa moyo na ushauri wa kujenga kabisa matumaini mapya
 
Pole sana mkuu. Ajira siku hizi ni ngumu usitegemee sana kuajiriwa. Pambana ujiajiri mwenyewe haya maisha siyo ya kuyaonea aibu. Fikiri nje ya box fursa zipo nyingi tu usibague kazi kwa kuangalia elimu yako. Kuna jamaa alianza kufuga kuku na bachelor yake saivi hataman hata kuajiliwa. Kumbuka waliofanikiwa ni kwa sababu hawakati tamaa na wanaokata tamaa hawafanikiwi.
 
pole sana mkuu,anzisha private tuition hapo nyumbani kwako,au kituo cha watu wanaosoma as private candidates,hutakosa hela ya kula.
 
Anzisha Mradi, umesomeshwa uelimike sio uajiriwe fight uanzishe cha kwako usikariri Maisha yanabadilika!!!

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
Wewe umeanzisha mradi gani,maana hata mradi pia kuanzisha ni pesa kama bado hana pesa ya kuanzisha mradi atafanyaje?maana pesa zote yawezekana walitumia kumsomesha wakijua kunasiku atatoka,mradi wako ulionzisha wewe unaweza kumpa kazi?

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom