Hivi hawa wanaishiaga wapi?

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Matokeo ya Kidato cha nne 2009

Division I + II + III = 42,627 sawa na Asailimia 17.85

Divisheni IV = 130,651 sawa na Asilimia 54.66

Divisheni 0 ( Sifuri) = 65,708 sawa na Asilimia 27.49

Najiuliza hivi hawa Zero + Four ambao ni Asilimia 82.15 Wanakwenda wapi?

Mwaka Jana tumezalisha wangapi? Mwaka Juzi Je na Je Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Mwakani inapunguza hiyo Zero na Four

Je Baada ya Miaka Kumi tutakuwa na Taifa Gani
 
Baada ya miaka 10, kutakuwa na matabaka. Nchi yetu itazidi kuwa nchi isiyoweza kusonga kutokana na kukosa wananchi waliokuwa qualified (walioelimika) ili kuweza kukabili changamoto za karne hii. Ninaamini hatutabadilika na hali hii ya umaskini itaendelea.

Hao vijana wanaofeli laki na nusu (NB: Div IV ni kufeli pia) tunaotengeneza kila mwaka, baada ya miaka kumi tutakua nao zaidi ya milioni moja. Na hawa ndio walioweza kufika sekondari, hatujawahesabu wale waliofeli darasa la saba na kushindwa kuendelea.

Matatizo mengi tuliyo nayo sasa ni kutokana na kuwa na watu wasiokuwa na elimu ya kutosha katika kazi zao; kuanzia walimu, administrators wa ofisi za serikali, mapolisi etc
 
Je hawataki kuwajibika kwa Sababu watoto wao wanasoma Olympio, Bunge, St. Fransis, Marian, Maria Goreth, Mzizima?
 
Najiuliza hivi hawa Zero + Four ambao ni Asilimia 82.15 Wanakwenda wapi?

Mkuu heshima mbele.

Naunga mkono kutaka kujua vijana walofel wanaenda wapi!

Lakini nakujulisha tu kua Division IV zipo ambazo zinaenda form five.
So ktk uchambuzi huu tunakosakujua kati ya wenye Div IV wangapi wana credit tatu (i mean 3 C's) ambazo zinawawezesha kuingia form five. Coz si wote wamefel kuna wengine wako eligible kuendelea.

Asan10
 
Ni kweli. Nawajua mabinti fulani wawili walipata four wakaenda kwa kuchechemea Form five private school cha ajabu walienda kuibuka na Div I kule huwezi kuamini.
 
Watoto wa wenye nazo watarudishwa shuleni kusoma tena. Hata kama uwezo hawana, watalazimishwa kufaulu na bila shaka watafanikiwa kufanya hivyo. Watoto wa maskini, wataishia kuwa matapeli, majambazi, makuli, wapiga debe, wazururaji, wauza unga na wakijitahidi sana wanaweza kuwa wakulima au wamachinga.
Inapendeza sana kwamba umeuliza baada ya miaka kumi itakuwaje!!! kusema ukweli, ni kwamba utakayeona athari za hiyo miaka kumi ya kuzalisha zero na four ni wewe (kama ni maskini kama nilivyo mimi). Lakini kwa hao wenye nazo na hao wenye madaraka katika nchi hii hawatakaa waone madhara ya hizo ziro na four kwa kuwa pamoja na umbumbu wao bado watakuwa na nafasi ya kuendelea na masomo katika ngazi mbalimbali.
Lakini labda kilicho wazi zaidi na pengine ndiyo mkakati kamili wa serikali yetu ni kuwa na watoto wa watawala (wachache) wakiendelea kushika nafasi nzuri za kazi na watoto wa maskini (wengi) wakiendelea kuwa ni vibaraka wa hao wenye nazo. Kuzalisha kundi la watu zaidi ya laki mbili wenye div four na ziro ni kuukejeli umma wa watanzania. Lakini wote tumemsikia Mahiza akisema hizo four na zero wala hazijaishitua serikali. Wanaona ni matokeo ya kawaida tu. Ni sawa kwa kuwa walijenga shule za yeboyebo kwa ajili ya kupigia kampeni, na kuwadanganyishia wazazi masikini kwamba wanawajali, ilihali zile shule hazikuwa na sifa za kumfundisha mtoto wa kitanzania. Hii ina maana gani basi, kama si ushahidi tosha kwamba serikali inazalisha ziro kwa makusudi?
 
Matokeo ya Kidato cha nne 2009

Division I + II + III = 42,627 sawa na Asailimia 17.85

Divisheni IV = 130,651 sawa na Asilimia 54.66

Divisheni 0 ( Sifuri) = 65,708 sawa na Asilimia 27.49

Najiuliza hivi hawa Zero + Four ambao ni Asilimia 82.15 Wanakwenda wapi?

Mwaka Jana tumezalisha wangapi? Mwaka Juzi Je na Je Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Mwakani inapunguza hiyo Zero na Four

Je Baada ya Miaka Kumi tutakuwa na Taifa Gani

Matokeo haya yana i indict system yenyewe zaidi ya kuonyesha kwamba watu wanafeli. Unapokuwa na division 4 na 0 zaidi ya 50% ni lazima ujiulize what's wrong with this system, not the students.

Siamini kama 54% ni wajinga kiasi hicho.

Hivi mitihani yetu ni migumu sana? Walimu hawafundishi?
 
Ni kweli. Nawajua mabinti fulani wawili walipata four wakaenda kwa kuchechemea Form five private school cha ajabu walienda kuibuka na Div I kule huwezi kuamini.

Uko sawa wanaofeli na kujiendeleza kwa kurudia mitihani wengi wao hufaulu na kwenda hadi chuo Kikuu!
Hivyo tatizo ni mfumo mzima wa elimu ndio mbovu!! Kuanzia wizara yenyewe hadi waalimu mashuleni! Wanafunzi wanafundishwa na waalimu wasioelewa(voda faster), ndio maana unaona wengi wanakata rufaa baada ya matokeo, wakiamini walichoandika ni kweli kumbe sivyo!!
 
Najiuliza hivi hawa Zero + Four ambao ni Asilimia 82.15 Wanakwenda wapi?
***wanabaki mitaani na kujihusisha ba kazi za kila siku. Kazi tu za kawaida!

Je Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Mwakani inapunguza hiyo Zero na Four
?
***Suala la kufaulu sio la serikali. Ni suala la wanafunzi husika. Unata serikali iwape majibu? serikali imewasaidia vipi hao wanafunzi waliopata div 1, 2, 3?

*** wanafunzi ndio wanapaswa wajitahidi. Si lazima wote wasome O level au A level. Kama 'uwezo' haupo kitaaluma basi wengine wajiunge hata na VETA.

Ohoo, wanaopata IV wanaingia ualimu wengine. Yaani hao ndio moto unaoendeleza this vicious cycle. Mtu kafeli hesabu lakini anaenda kusomea ualimu wa shule ya msingi na anakuwa mwalimu wa hesabu
 
Ohoo, wanaopata IV wanaingia ualimu wengine. Yaani hao ndio moto unaoendeleza this vicious cycle. Mtu kafeli hesabu lakini anaenda kusomea ualimu wa shule ya msingi na anakuwa mwalimu wa hesabu
Hao ndio sawa na waalimu wa UPE
 
hao wanaopata Division IV umekosea kidogo sema waliokosa credit sio Div. IV ok hapo tutakuwa sawa kwani wengine wanaendelea Form V wengine ualimu, Polisi, Jeshi wanaopata Div IV point 30 na kuendelea mpaka ZERO ndio tuwajadili.
 
Matokeo ya Kidato cha nne 2009

Division I + II + III = 42,627 sawa na Asailimia 17.85

Divisheni IV = 130,651 sawa na Asilimia 54.66

Divisheni 0 ( Sifuri) = 65,708 sawa na Asilimia 27.49

Najiuliza hivi hawa Zero + Four ambao ni Asilimia 82.15 Wanakwenda wapi?

Mwaka Jana tumezalisha wangapi? Mwaka Juzi Je na Je Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Mwakani inapunguza hiyo Zero na Four

Je Baada ya Miaka Kumi tutakuwa na Taifa Gani

Wachache wanarudia mitihani hata mara 10 kutafuta credit ili kuendelea na masomo, wachache wanaishia kwenye vibarua vya utarishi katika ofisi za sirikali na watu binafsi, polisi, jeshi, magereza, lakini wengi wao hasa wenye Div 0 wanaishia katika ajira zisizo rasmi kama vile ujasiri wa mali mtaa wa Ohio, ukabaji mitaani, kuuza bwimbi nk.
 
Ohoo, wanaopata IV wanaingia ualimu wengine. Yaani hao ndio moto unaoendeleza this vicious cycle. Mtu kafeli hesabu lakini anaenda kusomea ualimu wa shule ya msingi na anakuwa mwalimu wa hesabu
Katika nchi ambazo viongozi wake wako makini katika maendeleo ya nchi zao hili lisingekuwa tatizo kubwa kiasi hicho, tatizo naliona pale ambapo viongozi hawana maadili unategemea nini katika taifa la jinsi hiyo.

Mifano ipo mingi ila ninayo ikumbuka haraka kama namna ya kuonyesha kwamba viongozi wetu hawana maadili ni pale ambapo sisi kama nchi badala ya kufanya huduma za afya ziwe nzuri kwa watu wote, badala yake viongozi wanaenda kutibiwa nje (Bahati mbaya kwenye mtego huu hata baba wa taifa alinaswa).

Kuhusu elimu ambayo ndio mada ya msingi ni kwamba elimu yetu itakuwa nzuri tu endapo kutakuwa na haki sawa kwa wote katika elimu. Lakini kwa mchezo huu tunaoucheza sasa wa viongozi kwenda kusomesha watoto wao nje au hizo zinazoitwa International school kwa kodi zetu halafu utegemee watasimamia elimu ya nchi hii ni mchezo wa kuigiza!!

Kutegemea kwamba mwalimu anayelalamikia kila siku maslahi yake na bila kusikilizwa ataweza kufundisha vizuri mwanao pia ni utani mwingine. Achilia mbali walimu wa voda faster.

Tunavyoelekea uchaguzi tukumbuke kwamba unapomchagua huyo kiongozi wako unampa nafasi ya yeye kuwasomesha vizuri wanawe ili waje kuwa viongozi wa mwanao kama ambavyo yeye ni kiongozi wako. Kwani ndio mfumo wa nchi corrupt ulivyo.
 
Kazi si kusoma tu wajaameni, japo kusoma ni muhimu kuna watu hazi-click huko na wanahitajika sana huko kwetu kwenye informal sector...mafundi, casual labour, drivers, the list goes..

Na huku ndhiko kazi nyingi zilipo hapa bongo formal sector (professional jobs) ni chache mno..
 
Ni sawa, kazi si kwa waliosoma tu. Ila kuwa na failures zaidi ya 100,000 kila mwaka haina manufaa yeyote. Tunahitaji jeshi katika informal sector lakini sio jeshi la wananchi 100,000. Kama tutatengeneze jeshi la vijana 100,000 kila mwaka watakao kuja kuwa mainjinia, wanasayansi, wachumi, nk hapo nchi itakuwa na mwelekeo.
 
Nafikiri tukiwa na mainjinia wanaotengeneza viwanda 100 ni bora zaidi kuliko mainjinia na wachumi wenye vyeti wanaomba kazi ...
 
Kazi si kusoma tu wajaameni, japo kusoma ni muhimu kuna watu hazi-click huko na wanahitajika sana huko kwetu kwenye informal sector...mafundi, casual labour, drivers, the list goes..

Na huku ndhiko kazi nyingi zilipo hapa bongo formal sector (professional jobs) ni chache mno..

Ebo! Hivi hawa hawahitaji Elimu ee! Kila mwaka Zero + Four Laki Mbili jamani halafu hatuoni kama kuna Tatizo, hivi tutaweza kweli Kupambana katika EAC na hali kama hii?
 
Nimeleta hii mada baada ya Kushtushwa na mdogo wangu mmoja aliponiambia the way wanavyofundishwa Kingereza

Jamani watoto siku hizi wanakaririshwa hata Kingereza? Imagine Mwalimu anawapa Mbinu wanafunzi kwamba

Katika Mtihani Ukiona If basi jawabu lake ni then kama ukiona Whom basi jibu lake ni You yaani kuna formula za namna ya Kujibu maswali ya Kingereza siku hizi!

Sasa najiuliza Tatizo liko wapi?

Walimu hawaandaliwi Vizuri au hawana knoledge ya kile wanachopaswa kufundisha au Wanafunzi wanasukumwa kutoka Primary kwenda Secondary!

Ni wapi makosa yamefanyika jamani kwa maana the situation is worse than what someone can imagine
 
Back
Top Bottom