Hivi hawa waimba Singeli huko nyuma walikuwa wanaimba nini?

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,829
15,791
Nauliza tu, maana kuanzia mwakajana kumeibuka utitiri wa vijana wanaoimba muziki huu, je kabla haujaaanza kutambulika mtaani walikuwa wanaimba nini, au walikuwa hawaimbi?
 
Inategemea ni waimba singeli wa pande zipi! Wa huku Ushenzini kwetu walikuwa ndo waimbaji wa mchiriku, mnanda, segere... na wengine mdundiko kabisa!!! Ni wale huku ushenzini kwetu demu mmoja amezinguana na mwenzake anakukodia vigoma hadi mlangoni pako!!!

Halafu nakutana na binti mmoja hivi halafu ananiambia eti nihamie sijui wapi cjui... aaaargh!!
 
Tungekuwa tunathamini vya kwetu kama tunavyothamini vya ulaya basi mchiriku,mnanda,vanga na segere ingekuwa mbali sana,mkuu kuna madogo huku kitintale wanapiga vigoma vya hatari,tatizo muziki wenyewe unaimbwa na wa huni na umekaa kihunihuni
 
Inategemea ni waimba singeli wa pande zipi! Wa huku Ushenzini kwetu walikuwa ndo waimbaji wa mchiriku na mnanda... na wengine mdundiko kabisa!!! Ni wale huku ushenzini kwetu demu mmoja amezinguana na mwenzake anakukodia vigoma hadi mlangoni pako!!!

Halafu nakutana na binti mmoja hivi halafu ananiambia eti nihamie sijui wapi cjui... aaaargh!!

We kweli mshenzi wa ushenzini..
 
Ndio hawa waimbaji walio changanya ladha kutoka mdundiko kigodoro ivyo kuingia kwenye media ndio kukaitwa singel
 
We kweli mshenzi wa ushenzini..
Mshenzi ni tusi zito sana lakini kwavile User ID yako inaakisi huku kwetu, nitaacha yapite!! Huaga hatufanyiani hinda wenyewe kwa wenyewe. Ukisikia masela wananong'onezana "...ng'ombe hilo, ng'ombe hilo..!" Jua washajua kwamba huyu ni baki tu na kwahiyo ni halali; lakini sio wenyewe kwa wenyewe kwa sababu wanajua ukimfanyia mwana mtiti wake si mdogo!!!
 
Hahahahaaa walikua wanakaba mkuu walikua hwaimbi ndio maana wnajiita machizi boti
 
Mshenzi ni tusi zito sana lakini kwavile User ID yako inaakisi huku kwetu, nitaacha yapite!! Huaga hatufanyiani hinda wenyewe kwa wenyewe. Ukisikia masela wananong'onezana "...ng'ombe hilo, ng'ombe hilo..!" Jua washajua kwamba huyu ni baki tu na kwahiyo ni halali; lakini sio wenyewe kwa wenyewe kwa sababu wanajua ukimfanyia mwana mtiti wake si mdogo!!!
Hahahahaaa mshenz sio tus moja kwa moja n mtu alikua sio mstaarabu kwa hiyo washenz ni kinyume cha kitokua starabu
Ni kweli kuna watu hawana stara wala aibu waache wajiite washenz ndio walivyo
 
Naupenda mmoja choras anasema
Utatoa hutoi........ Nauliza utatoa hutoi
Sijui ameimba nani
 
Napenda singeli ila zile staili watoto wakiume wanazocheza zipo kishoga shoga hadi naona aibu kuangalia na watu wazima, yaan unakuta mtoto wa kiume kajifunua shati kapiga mlegezo na kabinua makalio anakata nyonga bila aibu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom