Kuna watu ambao wamejipa mamlaka ya kuwasahihisha wengine huku wao nao wanafanya makosa yale yale,peke yake hili ni tatizo,lakini kwenye tafsiri ya kuvaa vibaya na vizuri nadhani hapa kuna namna tofauti kutokana na eneo husika
Kwenye nchi nyingi hapa Africa hasa hapa Africa ya mashariki kuna maungo ambayo mwanamke kiutamaduni hatakiwi kuyaonesha,kama vile magoti,mgongo,mapaja n.k,tatizo linakuja kuwa sidhani kama hii ni sheria na kama ipo sijui wa kuisimamia itekelezwe ni nani
Lakini pia,nashangaa serikali kukaa kimya kwenye matukio haya,binafsi sioni kama ni jambo jema mtu kuonesha maungo yake hadharani lakini sioni kama ni jambo la kiungwana mtu kwenda kuvua nguo hadharani yule ambae ameyaonesha maungo yake,kiustaarabu kuna namna ya kufanya kama watu wameamua kutaka kuondoa jambo hili kwenye jamii,lakini hili ni vyema liende sanjari na kuwaadabisha vijana wa kiume pia na sio kuwaacha wao waendelee kuvaa kiajabu ajabu tu
Tatizo nchi yetu hii ili lionekane jambo fulani ni tatizo ni hadi pale litakapoingilia maslahi ya wakubwa ndio litashughulikiwa!