Hivi hawa jamaa zabuni ya ummantile walitangaza lini?

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Kitendo cha waziri Ummy Mwalimu, kufuta utaratibu wa kuuza chakula kwa wagonjwa wanaolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ni sawa kabisa. Tena huo utaratibu wala usifikiriwe kuanza. Ni uhuni tu ule!
Kama migahawa na lile soko la matunda Havitoshi basi watenge eneo lingine wauze vyakula na wagonjwa/ndugu wanunue kwa hiari yao na/au kwa maekekezo ya madaktari. Haina maana kumpangia mgonjwa ratiba ya kula tena kwa pesa yake mwenyewe. Itoshe kuwashauri wagonjwa vyakula wanavyopaswa kula kulingana na hali zao na kisha wao na ndugu zao watajua, wakanunue wapi au kama ni kukopa wajiongoze.
Kuhusu msonganano, watafute mbinu nyingine ya kuupunguza;
'Wagonjwa wabaki kuwa wateja wa huduma za afya, sio kuwafanya wateja wa biashara ambazo zabuni zake hazikuwahi kutangazwa'!
 
Back
Top Bottom