Nimekuelewa..
Ila mkuu mke wa mtu ni mtamu lakini siku ukikamatwa na mumewe anakua mchungu sana .
Achana nae haraka sana. mbona mabinti wabichi na ambao hawana watoto wapo ndugu, tafuta binti mmoja mbichi ambae injini haijashushwa wekeza huko akili zako na sio hisia. Akili zikikuambia weka ndani fanya chapu ndoa ni BARAKA,
Ila hakikisha akili ndiyo inayo kuambia weka ndani na siyo hisia.
Huyo mke wa mtu kuhusu kutofuta namba zako isikupe shida , akikucheki mpotezee ila mkikutana akikuchangamkia mjibu kistaarabu alafu uwe serious sana ila uwe mstaarabu na hayo ndiyo maisha na maana ya busara na hekima.
Ipo siku atakuja kukuheshimu sana pia hakikisha usije ukamvua chupi mkuu ili hali unajua wazi ni mke wa mtu.
KUMBUKA .Sisi vijana tunavuaga chupi wale wake za watu ambao hatujui kama ni mke wa mtu tukizania ni single mama tuu. Ila tukijua ukweli ni mke wa mwanaume mwezangu tunajutiaga sana nainaumaga sana na kuomba toba. Japo hatuwekagi wazi kama tunajutia.
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app