Hivi Gambo, Hii Kero Ya Br. Ya Kijenge -mwanama-engutoto Huioni?

Muhumba wa Mukinyaa

JF-Expert Member
Nov 12, 2022
683
1,233
Mh Mbunge ungepunguza KULALAMA na tumia muda wako mwingi kutatua kero za wapiga kura wako.

Moja ya kero ni hii barabara ya Kijenge- Mwanama -Engutoto..barabara hii imaliziwe kuwekewa lami toka hapo Mwanama Kona hadi huku Viwandani Engutoto kwani imekuwa chanzo cha kukosekana kwa magari mazuri na imara kwa ajili ya abiria waishio kata hii ya Oleriani..

Ni jambo la kawaida kabisa kwa muda wa asubuhi na jioni abiria kukaa vituoni saa 1-2 wakisubiri gari..Hii imekuwa ikisababisha watu kuchelewa maofisini,wanafunzi kuchelewa mashuleni na wagonjwa kuchelewa hospitalini

Pia inasababisha kuongezeka kwa gharama za USAFIRI kwa wananchi, ambapo baadhi huamua kupanda bodaboda hadi njia ya MOSHONO-MJINI ilikupata usafiri ambapo huwalazimu kulipa zaidi ya Tsh 1500/=

Mwisho, njia hii ya Kijenge - Mwanama- Engutoto ndio njia pekee ambayo hizi Bajaj zinazuiwa kutoa HUDUMA kwa wananchi licha ya changamoto ya ukosefu wa vihiace..kuna WAHUNI wameanzisha serikali yao,kazi yao ni kuwazuia waendeaha Bajaji wote wanaopita njia hii..wanabarrier yao hapa Darajani mita chache toka lilipo TAWI la CRDB Kijenge
Nikuombe dhibiti WAHUNI hawa ili Bajaj ziweza hudumia wananchi wa ukanda huu wanaoteseka na huduma mbovu kabisa ya usafiri

Mwisho kabisa..kwanini lami ya njia ya PEPSI -PPF Kijenge -Mwanama kona iliishia ndani ya hizo nyumba za PPF Kijenge..hawa wananchi wanaokaa mbele huku hadi kilipo Kituo cha Afya MOSHONO wao ndio hawastahili kupata huduma ya LAMI?..
 
Muache ameshamuomba mama jimbo ligawanywe kwa kuwa mwenye arusha yake amekuja yeye muache aendelelee kugawa majiko ya kupikia :cool::cool:
 
KABISA, KABISA

Kama anataka kura za Wana Arusha msimu ujao ahakikishe ametatua kero hii na Miundo mbinu ya Arusha kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom