Hivi famous ''Malaika'' song ni Wa kenya au Tanzania, wakenya kama kawa wadai wao

Moneyowner

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,423
1,252
Jamani kuna huu wimbo wa malaika, uliotungwa enzi hizo, malaika nakupenda malaika, wakenya eti wanadai ni wa kwao , wakati miriam makeba aliaknowledge kuwa wimbo huo ni wa tanzania, Inasemekana katika wikipedia wimbo huo ulitungwa na mtanzania mwaka 1945, ukaja recodiwa na mkenya mwaka 1960, sasa wakenya mapovu yanawatoka.

Kwanza nashangaa kenya kiswahili cha mule ndani sijawahi sikia wakiongea , mana wao ni wazee wa broken swahili, sasa nashangaa ati wanasema wimbo wao,

Mashairi hapo chini, sasa toa mchango wako kama unajua asili ya huu wimbo je ni tz au kenya

Malaika, nakupenda Malaika
Angel, I love you angel
Malaika, nakupenda Malaika
Angel, I love you angel
Nami nifanyeje, kijana mwenzio
and I, what should I do, your young friend
Nashindwa na mali sina, we,
I am defeated by the bride price that I don't have
Ningekuoa Malaika
I would marry you, angel
Nashindwa na mali sina, we,
I am defeated by the bride price that I don't have
Ningekuoa Malaika
I would marry you, angel

Kidege, hukuwaza kidege
Little bird, I think of you little bird

Ningekuoa, Malaika
I would marry you, angel

Pesa zasumbua roho yangu
The money (which I do not have) depresses my soul
Pesa zasumbua roho yangu
the money (which I do not have) depresses my soul
Nami nifanyeje, kijana mwenzio
and I, what should I do, your young friend
Ningekuoa Malaika
I would marry you, angel
Nashindwa na mali sina, we
I am defeated by the bride price that I don't have
Ningekuoa Malaika
I would marry you, angel

pia link ya kuusikiza hii hapa
 
Jamani nimeambia kuwa john kitime ana historia nzuri ya huu wimbo embu tumtafuteni atuambie, mana wengine wanasema huu mziki ulikuwa maarufu toka enzi na enzi kabla hata ya huyo mkenya kuurikodi rasmi 1960, KITIME POPOTE ULIPO. maana hawa wakenya wezi sana
 
Mods rudisheni huu uzi jukwaa la habari mchanganyiko, maana huko ndo kuna wazee wa zamani, kuuficha uzi muhimu kama huu wa kihistoria huku kwa vijana wa bongo fleva wa mwaka 2000 sio fair
 
Sio povu, Wakenya wako sahihi, Fadhil William ni raia wa kenya na ndie mtunzi wa wimbo huo nijuavyo mimi!
 
Nyimbo ya tanzania io then n moja ya kivutio kikubwa kwa nchi
Peace kwa mtunzi wa nyimbo hiyo jina nimesahau
Source: kikao fulan iv cha bunge enzi zile
 
COSOTA wanaeza kulisemea hili mana ishu apo ni copyrights za uo wimbo..
 
Sawa nimebugi; Huyo Kungubayo ni wa wapi? Hebu tupe profile yake kidogo!

Omari Kungubayo ni mzaliwa wa Tanga, akakulia Pemba na maisha mengi alikuwaga Mombasa. Wayajua tena mambo ya Pwani. Hivyo alikuwa Kenya mpaka enzi za Mzee Jomo alipowatimua wasio wazawa Kenya. Kwa kuwa kungubayo alikuwa mwimbaji mwenye kipaji alijulikana sana Mombasa. Hivyo alikuwa miongoni mwa wale watimuliwa wa kwanza kule.
Kungubayo aliporudi nyumbani hakuwa na maisha sana, akaimba wimbo mmoja very famous ukiitwa "Ajuaye Bwana Mungu, mgonjwa kuwa mzima na alomzima kuwa mfu". Wimbo ulitumiwa sana na RTD kwa salaam za wagonjwa enzi hizo. Na nyimbo zake nyingi sana hata sizikumbuki. Wengine waweza zikumbuka waziweke hapa. Tatizo letu wa Tz ni kuwa hatunaga ile ham ya kuwainua wengine. Mtu ana struggle mwenyewe.
 
Thanx a lot
 
Nilishaweka uzi hapa.

Wimbo wa "MALAIKA" kwa mara ya kwanza kabisa uliimbwa na kijana mdogo wa eneo la Kaloleni Arusha miaka ya 70 mwishoni na alitumia zeze alilotengeneza mwenyewe kumuimbia mtoto wa kihindi.

Baadaye wakenya ndio akatokea jamaa mmoja wa Kenya sijui Fadhili nani na kusema ni wimbo wake huo.

Kisha ukaimbwa na Mirium makeba na watu wengine wengi mpaka Wazungu.

HUO NDIO UKWELI.
 
Back
Top Bottom