Hivi faida ya "show off" ni nini?

Hivi faida ya "show off" ni nini?

Kujionesha kwamba una nyumba kubwa!

Kujionesha kwamba una ujauzito (Tumbo kubwa!)

Kujionesha kwamba na wewe unaitwa baba mtandaoni.

Kujionesha kwamba una gari kali.

Kujionesha kwamba wewe una Shamba kubwa! Tupia picha za mahindi yako, matikikiti yamejaa shambani huku umenyoosha mikono na mengineyo yanayofanywa huko mitandaoni.

Cha ajabu kuna watu wanafanya makubwa zaidi ya hayo lakini wapo kimya.

Timiza malengo yako kimyakimya utatoboa. Achana na kiki!
Fanya kitu roho inapenda watu hatuwezi kufanana
 
Hivi kabla ya social medias hizi show offs zilikua zinafanyikaje? Tusiopost chochote huko watsapp status tunaonekana kama wanama/washamba flani.
Hivi kabla ya social medias ulikuwa unacomment wapi? Kwanini usiendeleze ulivyokuwa unajadiriana na kuishi kabla ya social media? Kwanini leo uko JF? Hoja utakayotoa ndiyo hiyo hiyo inayofanya wanaopost watsapp na kwningine wafanye hivyo.
 
Kujionesha kwamba una nyumba kubwa!

Kujionesha kwamba una ujauzito (Tumbo kubwa!)

Kujionesha kwamba na wewe unaitwa baba mtandaoni.

Kujionesha kwamba una gari kali.

Kujionesha kwamba wewe una Shamba kubwa! Tupia picha za mahindi yako, matikikiti yamejaa shambani huku umenyoosha mikono na mengineyo yanayofanywa huko mitandaoni.

Cha ajabu kuna watu wanafanya makubwa zaidi ya hayo lakini wapo kimya.

Timiza malengo yako kimyakimya utatoboa. Achana na kiki!
Punguza wivu
 
Hulka ya binadamu kujionesha, kuringishia alicho nacho, kipya au kizuri. Nakumbuka kuona tabia hizo tangu utoto wangu hadi ukubwani. Nahisi anayefanya hivyo anapata furaha nafsini mwake hasa kwa watoto, kwa watu wazima ni kukomoa, au kuumiza wengine wasio na hicho anachoringia.
 
Unakoelekea utakuwa mchawi wewe. Wivu+majungu=uchawi.

Tutaendelea kupost nyumba na magari yetu ili uumie zaidi.
 
Kila Binadam Ana Vinasaba vya Kujikweza..

Kila Binadam Ana Kiu ya kupata Kitu Fulani.. na Akikipata huwa na Muhemko wa Kuonyesha.. " YES I MADE IT"

ishi Maisha Yako....
 
Show off ni ulimbo mkuu, thats why vijana wanapenda sana show off!

Kuna kundi kubwa la watu hasa wanawake ambao ndio wanakuwaga intimidated na maisha
mazuri hata kama sio halisia sababu hawahitaji kujua hilo 😂😂😂!

Ni njia ya kuhadaa watu wengine tu wakuone una maisha safi ila kimsingi unaweza kuwa broke nigga tu. Inarahisisha zaidi shughuli za ulaghai!
 
Baadhi ya watu wamekula/ liwa kimasihara sababu ya "show off " za watu.
 
Show off ni ulimbo mkuu, thats why vijana wanapenda sana show off!

Kuna kundi kubwa la watu hasa wanawake ambao ndio wanakuwaga intimidated na maisha
mazuri hata kama sio halisia sababu hawahitaji kujua hilo [emoji23][emoji23][emoji23]!

Ni njia ya kuhadaa watu wengine tu wakuone una maisha safi ila kimsingi unaweza kuwa broke nigga tu. Inarahisisha zaidi shughuli za ulaghai!
Loh kumbe hii jinsia yenzetu iko hivyo
 
Back
Top Bottom