Hivi Dokta Dau hana jema hata moja?

George Smiley

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
471
266
UKURUGENZI MKUU NSSF 1997 – 2016
HIVI DOKTA DAU HANA JEMA HATA MOJA?
2016%2B-%2B1

Kabla ya kuanza kuandika chochote kuhusu maudhui yenye anuani hiyo hapo juu, niwakumbushe wasomaji wangu ‘kisa’ kimoja nilichohadithiwa na rafiki yangu ambaye alikishuhudia yeye mwenyewe katika nchi moja (sipendi kwa leo kumtaja wala kuitaja hiyo nchi).
Dereva wa gari ambaye ni mzaliwa wa nchi hiyo aligonga gari ya mwenzake ambaye ni raia wa kigeni kwa dhahiri shahiri. Huyu dereva mzalendo ndiye aliyevunja utaratibu lakini cha ajabu yeye akawa akimlaumu, akimgombesha na kumtukana matusi mazito mazito yule aliyemgonga.
Yule aliyegongwa baada ya kuona watu wamejaa katika eneo la tukio akauliza: “Jamani! Katika hali hii mimi hapa kosa langu ni lipi?” Yule mzalendo aliyemgonga akamjibu hivi (na hapa ndipo kwenye nukta ninayoikusudia):“Kosa lako wewe ni kuwepo hapa nchini petu kwani kama ungekuwa kwenu, Je ningekuja kukugonga huko?”

Kisa hiki kinanikumbusha kwamba kuna baadhi ya makosa yanasababishwa na kumchukia tu mtu mwenyewe na wala si kuangalia kosa kama kosa katika mizania ya sheria.
Katika muktadha huo, ni vizuri tukajiuliza maswali kadha wa kadhaa juu ya ‘mlipuko’ wa baadhi ya wanahabari kumshambulia kwa kasi kubwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dokta Ramadhan Dau. Kulikonii? Au kosa lake ni kwamba alikalia mahala pa watu ambapo leo pamerudishwa kwa wenyewe?

Baadhi ya Watanzania wamestaajabishwa sana na ‘mlipuko’ huo mkubwa wa kumtangaza na kumshambulia Dokta Dau kwa tuhuma za ufisadi kwa sababu:

a)Hao ‘washika bango’ wa kuutangaza huo waliokwishauhukumu kuwa ni ufisadi hawaonekani kama wana lengo la kuhabarisha bali wamejipa kabisa mamlaka ya kuhukumu kwa kiwango ambacho hata hawakuhitajia kumhoji huyo wanayemtuhumu, jambo ambalo linaitia kasoro taarifa yao hiyo kwa jamii.

b)Wakati wanamjengea ‘kuchafuka’ huko katika jamii ya Kitanzania wamesahau kwamba ndio ‘wanamkejeli’ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli, kana kwamba hana vyombo makini vya kumpa taarifa na ‘akapotoka’ kwa kumteua kuwa Balozi mtu ambaye kwa mtazamo wao ni ‘mhalifu’ anayehukumiwa hata bila ya kustahiki kuulizwa na kujitetea.

c)Wakati washika bango hao wakikazia kumchafua Dokta Dau huku wakisahau kwamba katika uhalifu wowote ambao ni ‘shirikishi’ kumng’ang’ania mtu mmoja tu tena kwa kumtuhumu tuhuma nzito huku wakiwaacha wengine, ni dalili ya kuwepo ‘ajenda’ zilizofichwa nyuma ya mpango huo.

d)Washika bango hao wanastaajabisha kwa ufahamu wao juu ya taarifa za Dokta Dau lakini ‘wakazikalia’ mpaka alipoondolewa ndipo ‘wapumue’ kwa kuzitoa. Je,waliogopa nini kuzitoa hapo awali? Na kwanini sasa hawaogopi kuzitoa taarifa hizo?

Kama ni kweli kwamba chanzo chao kikuu cha taarifa ni Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) (Ripoti ambayo tayari Ofisi ya CAG imeshaikana), hivi Watanzania leo hii tumefikia kuifanya taarifa ya ukaguzi kuwa ndio hukumu halafu eti huo tuuite ndio utawala bora unaofuata sheria? Hivi Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inajadiliwa kwanza na wanahabari kisha wafikie au iwafikie watuhumiwa katika kadhia husika?

Amma kwa upande wa pili ndipo linapozalika swali ambalo huenda lingekuwa ndio ufumbuzi wa dhana ya chuki ‘binafsi’ dhidi ya Dokta Dau. Nayo ni kwamba huyo Dokta Dau aliyetumikia katika Shirika la NSSF kwa zaidi ya miaka kumi; hivi hana hata jema moja linalofaa kutangazwa?

Hivi jicho lenye uadilifu linaweza kuangalia mapungufu ambayo ni dhana na likawacha mafanikio ambayo ni hakika?
Je, washika bango wanakitazama Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa mtazamo upi?
Je, wanaitazama miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi inayofadhiliwa na NSSF kwa mtazamo upi?
Je, wanalitazama Daraja la Kigamboni kwa mtazamo upi?
Je, hayo na mengineyo kwa mtazamo wao ni mafanikio au mapungufu?

Hivi utendaji wa Dokta Dau katika Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutokea mwaka 1997 hadi 2016 mwanzoni, hakuna jema hata moja linalofaa kutamkwa kabla ya kupekua kinachoonekana kuwa ni mapungufu?

Watanzania lazima tuwe wakweli na kamwe tusiache kujifunza kutokana na msemo wa Waswahili usemao:“Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.” Kitendo cha kusahau kabisa mambo mema na mafanikio ya Dokta Dau katika Shirika hilo, hapo ndipo inapopata nguvu ile dhana kwamba Waislamu katika Tanzania hawatarajiwi kuwa raia wa daraja sawa na wenzao wa dini nyengine. Kwa hiyo, Muislamu ‘msomi’ katika Tanzania akishika wadhifa wowote katika serikali au shirika la umma hata kama atafanikisha mafanikio makubwa, anaonekana amefanikiwa kwa bahati mbaya tu kwa sababu sio matarajio Muislamu kutegemewa kuwa na uwezo katika utendaji.

Tumeshuhudia mara zote ambazo Waislamu wamekuwa viongozi wa juu katika nchi hii au katika idara, taasisi na mashirika mbalimbali ya serikali wamekumbana na matatizo na vizingiti kadha wa kadhaa mpaka walipobadilishwa na kupewa ‘wenyewe’ nafasi hizo, hapo sasa ndipo utulivu hupatikana.

Katika nchi yenye uwiano wa kukaribiana kiidadi raia wake kiimani ni aibu kubwa kuona kila eneo katika idara, taasisi na mashirika ya serikali kujazwa na raia wa dini fulani na akipatikana mmoja tu wa dini nyengine katika idara, taasisi au shirika lolote la serikali ‘atachimbwachimbwa’ mpaka ang’olewe na akishang’olewa kwa sababu tu amekalia sehemu ya ‘watu’ atachafuliwa ili jamii iaminishwe kwamba alistahili kuondolewa.

Katika hali ya ubaguzi wa aina hiyo, Watanzania Waislamu wanajiuliza: Hivi kweli tatizo ni kuwa Waislamu ‘hawakusoma?'

Hivi kwa nchi iliyo huru kwa takriban miaka hamsini sasa yule aliyewabagua raia wake kwa misingi ya dini mpaka kundi moja likapewa fursa ya elimu na kundi jengine likanyimwa; Je, huyo ni mzalendo au ni mbaguzi? Na Je, ni kweli kwamba Waislamu hawakusoma? Je, hawa Waislamu waliofikia viwango vya kushika urais, uwaziri, ukatibu mkuu wa wizara, ukurugenzi na kadhalika, sio Watanzania?

Ukweli ni vizuri ukasemwa kwamba Dokta Dau ashukuriwe kwanza mpaka Watanzania wajiridhishe kwa mafanikio haya makubwa yanayoonekana kabla ya kugeukia hayo yanayoitwa mapungufu. Huo ndio uungwana na ndio ustaarabu.

Katika hali hiyo sio vyema kukaa kimya kwani jamii kama inavyobadilika kitabia basi inabadilika kiuvumilivu na viwango vya subra.

Hivi ni kweli Dokta Dau hana jambo jema hata moja katika utumishi wake kama Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kiasi cha kuandamwa na ‘kusulubiwa’ namna hiyo? Na kama lipo, basi litajwe kwanza kwa sababu jema lipo wazi na linaonekana lakini mapungufu ni dhana inayohitaji ushahidi uliothibitishwa katika vyombo husika.

Hii ndiyo kauli yangu ya wiki hii na mjadala uko wazi.

Mwandishi wa makala haya ni Mwenyekiti wa ARRISAALAH ISLAMIC FOUNDATION.

Unaweza kuwasiliana naye kwa namba: +255 754 299 749, +255 784 299 749.

Mohamed Said: HIVI DOKTA DAU HANA JEMA HATA MOJA? NA SHEIKH MOHAMED IDDI
 
hivi huyu Dr. Dau ni mufti ,shehe au,mbona anatetewa na misikiti, hakuna mtu mwenye haki ya kumsafisha Doctor bali vyombo husika na sio msikiti wala kanisa,mbona Abdul Jumbe alionewa na hakutetewa hivi,mbona kuna majipu kibao ya imani yake yanatumbuliwa lakini hayapati watetezi
ufisadi hauna dini,rangi wala kabila,kama ni jipu atatumbuliwa tu
 
hivi huyu DK dau ni mufti ,shehe au,mbona anatetewa na misikiti, hakuna mtu mwenye haki ya kumsafisha doctor bali vyombo husika na sio msikiti wala kanisa,mbona Abdul Jumbe alionewa na hakutetewa hivi,mbona kuna majipu kibao ya imani yake yanatumbuliwa lakini hayapati watetezi
ufisadi hauna dini,rangi wala kabila,kama ni jipu atatumbuliwa tu
Mkuu nadhani unafaham tofauti ya Bakwata na Uislam!
Huyo Dr Dau ni M BAKWATA kwaiyo BAKWATA wameamua kumtetea BAKWATA mwenzao.
Na Sisi waislam tulikuwa tunajiuliza kila siku hivi hawa bakwata kila jambo la Serikali wanaunga mkono hata likienda kinyume na Imani yao?tumekuja kujua kumbe ni hivi vibali vya sukari na haya maufisadi ya NSSF!
 
mwandishi unaweza ukawa na hoja nzuri, shida hoja yako imebeba ajenda fulani ndani yake! mfano, 'Dr. Dau alikalia kiti cha watu...' watu gani?? hii inakupunguzia credits nyingi manake hata wewe unakosa objectivity kwa kuingiza mawazo ambayo huwezi kuthibitisha! Miradi unayohitaja inaweza kuwa ni mizuri lakini swali ni je hiyo ndo primary objective ya kuwepo kwa NSSF??? tumeona jinsi wastaafu walivyotaabishwa na kukosekana/kucheleweshewa malipo yao halali ya jasho lao...je pesa zilipelekwa wapi????
Nakubaliana nawe kwa hoja moja tu kwamba waandishi wengi, ukiwemo wewe, hawawezi kubalance story wala kufanya uchunguzi yakinifu!
 
Nyongeza hapo. Pia mwandishi amekiri kwa namna moja au nyingine kuwa kwa nini wamuandame tu Dk. Dau ulihari ubadhirifu au Makosa aliyoyafanya kayafanya na wengine. Na kwanini hao wengine wasiandamwe? Hii ina maana hata Mwandishi mwenyewe hajui nini anachotaka kufikisha kwa wasomaji wake.
 
Ndugu una hoja yenye mashiko sana tena sana ila umeiaribu mwenyewe kwa kuingiza vitu ambavyo kwa hakika uwezi kuvielezea kwa mfano unaweza kutuelezea kwa hakika uisalam ndiyo sababu ya Dr Dau kutolewa kwenye nafasi haliyokuwa nayo au unaweza kuelezea hao watu wenye hicho kiti ni kinanani?hoja ya kwamba na mema pia aliyotenda yasemwe hilo ninakubaliana na wewe
 
Jamaa amekaa NSSF tangu 1997 mpaka 2016 bado analalamika? Yaani u DG miaka yote hiyo? Hii si sawa ndio maana aliota mizizi!! Kinachoshangaza waislam wanamtetea kama masihi wao!! Inatia kinyaa!!
 
Nyongeza hapo. Pia mwandishi amekiri kwa namna moja au nyingine kuwa kwa nini wamuandame tu Dk. Dau ulihari ubadhirifu au Makosa aliyoyafanya kayafanya na wengine. Na kwanini hao wengine wasiandamwe? Hii ina maana hata Mwandishi mwenyewe hajui nini anachotaka kufikisha kwa wasomaji wake.
Nyongeza juu ya nyongeza!, nyoka huwa anapigwa kichwani. Kama makosa Ni ya wengine, bosi wao ndio anabeba msalaba. Dr. Dau kutetewa Na media/ waandishi wa dini kwa mtizamo wa kidini Ni tatizo zaidi ya tatizo
 
Dhana: Muda wote mtumishi wa umma/mwajiriwa wa serikali/shirika la umma hutarajiwa kutenda yaliyo mema kwa mujibu wa sheria. Dhana hii ndio kiini cha mtumishi husika kulipwa mshahara na marupurupu manono. Kila jema lolote hugharimiwa mishahara na malipo mengine kila mwezi. Kwa hiyo hakuwezi kuwa na jema la kukumbukwa isipokuwa kama nhusuka hakuwa analipwa chochote, bali alijitolea. Lakini ikibainika na kuthibitika kuwa kuna mambo kadhaa mtumishi husika aliyafanya kinyume na sheria basi huchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa malipo ya mishahara yake ya awali yalifanyika kwa dhana kuwa alifanya mema na kwa mujibu wa sheria.
ni hayo tu.
 
A

Ahsante!, mwerevu shule yako kaipata, lakini Si unaona udini ndio msingi wa mjadala?, akili zote twatia mfukoni tunaanza kushindania misahafu
 
Ukishika ofisi kubwa uwe tayari kuyapokea mengi tu ya namna hiyo...binafsi nakubaliana na mwandishi kuwa yawezekana anaandamwa na wapinzani wake si lazima wawe wa mlengo anaodhani yeye mwandishi maana tunajua pesa hazina mlengo ule tu zina milengo mingi. Lakini pia Dr Dau kwanza aliteuliwa na Mkapa na akarithiwa na JK na sasa Magu amefanya mabadiliko ambayo nadhani kiutawala ni sawa maana miaka hiyo ktk kiti kile si mchezo. Tumwombee ayapokee haya yanayosemwa na wapinzani wake wachache maana kama ni watanzania wengi hawako huko aliko mwandishi wa makala hii. Dau endelea na kazi yako umelitumikia taifa kwa uaminifu usiwe chanzo cha wengine kutugawa.
 
Utetezi wa kijinga sana. Eti kwakuwa nilifanya mema mengi basi nikifanya kosa moja nisisemwe kabisa.

Sijawahi kuona utetezi kama huo katika vitabu vyote vya sheria
 
hivi huyu DK dau ni mufti ,shehe au,mbona anatetewa na misikiti, hakuna mtu mwenye haki ya kumsafisha doctor bali vyombo husika na sio msikiti wala kanisa,mbona Abdul Jumbe alionewa na hakutetewa hivi,mbona kuna majipu kibao ya imani yake yanatumbuliwa lakini hayapati watetezi
ufisadi hauna dini,rangi wala kabila,kama ni jipu atatumbuliwa tu
Atetewe kwani ana kosa lipi?

Hapa unaopingwa ni uongo anaozushiwa
 
mwandishi unaweza ukawa na hoja nzuri, shida hoja yako imebeba ajenda fulani ndani yake! mfano, 'Dr. Dau alikalia kiti cha watu...' watu gani?? hii inakupunguzia credits nyingi manake hata wewe unakosa objectivity kwa kuingiza mawazo ambayo huwezi kuthibitisha! Miradi unayohitaja inaweza kuwa ni mizuri lakini swali ni je hiyo ndo primary objective ya kuwepo kwa NSSF??? tumeona jinsi wastaafu walivyotaabishwa na kukosekana/kucheleweshewa malipo yao halali ya jasho lao...je pesa zilipelekwa wapi????
Nakubaliana nawe kwa hoja moja tu kwamba waandishi wengi, ukiwemo wewe, hawawezi kubalance story wala kufanya uchunguzi yakinifu!
Na hawa ndugu zetu sijui ni nini, hivi kama kingekuwa KITI CHA WATU kama anavyo dai angekaa miaka 15 huyo mpendwa wake? na kabla yake ali kuwapo Mustapha Mkulo kwa takriban miaka 10 sasa hao wenyewe ni akina nani? Acheni kuongozwa ni Hisia zinazo wapeleka kuumba uongo eti ufanane na ukweli hii nchi ni ya Watanzania wote,mbona wakiondolewa madarakani wale mnao tofautiana kiimani hazi sikiki kelele toka dhehebu lolote, Au ili takiwa awe NSSF labda kwa miaka mingapi ndio nyoyo zenu zikwatuke?Hebu mamlaka ipewe nafasi ifanye kazi na kwanini Dau tu,what's so special,kuna nini? Na hii ina ashiria kuondoka kwake kumeathiri maslahi fulani bila shaka.
 
Ukiacha figisu figisu nyingi ambazo nchi yetu inapitia na ufisadi anaosemekana kuwa alipiga, kuna ishu moja aliwahi kusema Dk. Dau ambayo kwa kweli mm naona ndio suluhu ya matumiz ya rasilimali za nchi iko kwenye uwekezaji wa gesi ambapo kwa mujibu wa ZeMarcopolo (0ct 2013) Dk dau alisema Tanzania inaweza kuwekeza kwenye gesi nadhan alimaanisha kuwa hata visima vichache na mm naamin hiyo ni moja ya suluhu ya changamoto za uwekezaji. Nani ana hakika na hawa wawekezaji wa nje? Nigeria visima vya mafuta viko kwa mgongo wa wawekezaji lakin kumbe wanasiasa ndo wana miliki kwa asilimia kubwa, so to me Dau alikuwa na idea ambayo ni ya msingi sana.
 
Back
Top Bottom