Benito Mussolini
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 381
- 322
Wanabodi,
Ninakubali kwamba kuna mapungufu makubwa kwenye sheria ya uchaguzi, kwenye tume yetu ya uchaguzi na vilevile kwenye katiba yetu. Kurekebisha mapungufu haya kutahitaji washika dau wote kukaa meza moja na kuwasilisha hoja zitakazo ibua zaidi mapungufu haya.
Ingawa mapungufu haya yapo, sidhani kama ni jambo sahihi kwa wana CHADEMA kufikiria kwamba tofauti yao na CCM katika safu ya siasa ni katiba tu au tume huru. Siasa za Tanzania bado hazijawa za ushindani sana kwa wapinzani kusema kwamba tume huru au katiba mpya ni jambo linalo wafanya wawe disadvantaged sana kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Ila bado kuna umuhimu wa kuwa na mipango mizuri kwa ajili ya vizazi vijavyo vya Tanzania. Ndio maana kuna mantiki kwa chama tawala kufanyia kazi changamoto zinazo kabili jumuia ya siasa na wanasiasa nchini.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kama Chama mama na kama viongozi waliopewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania kwa miaka mingi ijayo, ni vyema kwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kuwa na mtazamo wa busara kwenye masuala yanayohusu siasa za Tanzania na hali ya wanasiasa wote nchini.
Hii haimaanishi kuwa na ahadi na kuona umuhimu wa kuwa na katiba mpya na tume huru tu bali ni kuwa mipango thabiti ya kuchochea siasa safi, ya kulinda haki ya wanasiasa wote na kutambua mchango wa vyama vya siasa vyote katika kuisogeza Tanzania mbele. Kukosea kwa mwanasiasa yoyote hakumpi yoyote ridhaa ya kumteka au kumpoteza bali ni ishara ya kuwa na sheria za ziada kwa ajili ya kuchochea shughuli za siasa zisizo kuwa na dosari na mahakama huru ya kutekeleza sheria hizi kwa haki na usawa
Hili likitiliwa maanani, kesi za watu kutekwa, kupotezwa au kunyimwa haki kwasababu ya maoni yao na sio kwasababu ya vitendo vya uhalifu zitatokomea. Pia sheria hizi zitasaidia kuhakikisha kwamba mikwaruzano yoyote au uhalifu wowote unaohusu siasa una amuliwa mahakamani na sio mitaani kwa nguvu ya dola.
Tafakari, ilani ya uchaguzi ya CCM itakugusa moja kwa moja au kwa njia zisizo moja kwa moja. Ridhaa ya wananchi itumike vizuri kutetea wananchi wote