Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 9,446
- 19,227
Nimekaa hapa wiki moja nzima, mabomba hayatoi maji.
Nadhani serikali imeharakisha kuhamishia makao makuu hapa Dodoma kabla suala la maji halijatengemaa.
Awesu ndo yupo Italy anakula bata tu.
====
UFAFANUZI KUTOKA DUWASA
====
Nadhani serikali imeharakisha kuhamishia makao makuu hapa Dodoma kabla suala la maji halijatengemaa.
Awesu ndo yupo Italy anakula bata tu.
====
UFAFANUZI KUTOKA DUWASA
====
Mdau pole kwa changamoto hiyo
Mimi ni Mkurugenzi wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira hapa DUWASA.
Kwanza ningependa kufahamu eneo uliloishi kwa muda huo wote ukakosa maji, pili nielewe kwa kifupi kuhusu hali ya maji jijini Dodoma.
Pamoja na kuhudumia Dodoma Mjini, DUWASA pia inahudumia miji ya Chamwino, Kongwa, Bahi na hivi karibuni tumeongezewa kibaigwa.
Ukiongelea Dodoma mjini, utakumbuka kuwa kati ya mwaka 2017/18 yalifanyika mabadiliko ya Serikali kuhamia Dodoma ambapo immediately kama taasisi tulitarajia ongezeko kubwa la mahitaji ya maji. Wakati huo tulikuwa tumekamilisha mradi wa maji hapa mjini ambao uliongeza uwezo wa uzalishaji na usambazaji maji kutoka lita 30 milioni hadi kufikia lita 61.5 milioni kwa siku. Mradi huu ulikamilika 2015, na miradi ya maji husanifiwa kwa kipindi cha kati ya miaka 20 mpaka 30.
Kutokana na hali hii ya ongezeko la mahitaji ukilinganisha na uwezo uliopo, hatua kadhaa zimechukuliwa na zinatekelezwa na DUWASA chini ya Wizara ya maji kutatua changamoto hii.
Mahitaji kwa sasa ni lita 133 milioni kwa siku wakati uwezo ni wastani wa lita 68 milioni kwa siku. Hii inatulazimu kutoa maji kwa mgao. Ndiyo maana nimeuliza eneo uliopo ili kujua nini kilitokea.
Tunaendelea na utatuzi wa changamoto hii katika hatua za Muda Mfupi (uchimbaji wa visima pembezoni Mfano Nzuguni), Muda wa kati (Ujenzi wa bwawa pa Farkwa), Muda Mrefu ( Kutoa maji ziwa Victoria)na Mpango wa Dharula (kutoa maji bwawa la mtera)
Yote hii ni kuhakikisha Dodoma inakuwa na huduma toshelevu ya majisafi.