Hivi CHADEMA mpaka leo haina watu wao huko Magereza?

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,178
2,000
Wandugu,

Kwa siasa za Tanzania zilipopitia, upinzani hasa CHADEMA ilitakiwa iwe na watu wao wanaowapa taarifa zote wanazohitaji katika idara zote za nchi hii. Niliwahi kuelezea humu ndani nini upinzani wanatakiwa kujifunza kutoka kwa Muslim Brotherhood.

Kama huko nyuma iliwezekana kupata taarifa nyeti na mkazitumia katika majukwaa ya kisiasa, leo inashindikana nini?

Tatizo kubwa ninaloliona ni kuwa kila taarifa mlizikuwa mnapata mlikuwa mna haraka ya kuzitumia kisiasa. Zingine mlitakiwa kuzitumia kuzichakata hizo taarifa zaidi ili kujijengea uelewa mpana wa nchi inavyoendeshwa na kuwatambua vizuri watoa taarifa na kupima uaminifu wao. Wakati mwingine kutozitumia taarifa mnazopewa kungewafanya msieleweke kirahisi na watawala na hivyo wangewaogopa sana.

Hii changamoto ya kwamba Mwenyekiti Mbowe yuko ndani halafu hamna watu wenu huko ndani wa kumlinda (Askari Magereza na wafungwa) na kuwapa kila taarifa mnazotaka, inafikirisha sana. Hii panicking mliyoionyesha leo haileti picha nzuri.
 

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,496
2,000
Inakuwa ngumu sana chadema kupata informers kutoka serikalini kwa sababu ina watu (viongozi) ambao hawaeleweki, leo unakuwa informer kesho yule mtu ambae unampa taarifa unasikia kahamia ccm.
Je, mtoa taarifa unakuwa katika wakati upi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom