Hivi CCM ni chama kikongwe kwa umri wake au kwa kufanya maamuzi yenye busara na hekima?

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,567
9,026
Chama cha Mapinduzi(CCM) ni kikongwe barani Afrika kikifuatia chama ANC Cha Afrika Kusini kwa umri, Sasa cha ajabu chama Kikongwe kinakosa demokrasia hata ya kuruhusu watu kujitokeza na kugombea urais ili wanachama wafanye maamuzi, kama mtu amefanya vizuri kwanini asishindanishwe na ambao hawajafanya chochote ili awashinde ndani ya chama demokrasia ichukue mkondo wake ,hizi kauli za utaratibu lazima Rais amalize mihura miwili sio demokrasia kabisa ,yaani mpaka wanasema mtu achukue fomu anaanzia wapi?

Maana yake ni kuwazuia wenye nia ya kugombea,hongera chama kikongwe.Kila siku huwa Ni Mbowe dikteta hataki kuachia uenyekiti ,hebu chama kikongwe onesheni mfano wa demokrasia ndani ya chama chenu tuone, demokrasia Ni kuiishi kwa vitendo sio maneno matupu.
 
CCM ndio chama pekee kinachowawekeaga wananchigombea asiekubaliwa na wengi,
Yaani mtu Kama Mkapa anaweza akaawaamulia watu 45m Nani awe Rais wao,wamtake wasimtake yeye haangalii.
Watu hawana Uhuru wa kuchagua kabisa.
 
[SUB]
IMG_20200617_195359.jpg
[/SUB]
 
Back
Top Bottom