Chief Kabikula
JF-Expert Member
- Jan 1, 2019
- 7,567
- 9,026
Chama cha Mapinduzi(CCM) ni kikongwe barani Afrika kikifuatia chama ANC Cha Afrika Kusini kwa umri, Sasa cha ajabu chama Kikongwe kinakosa demokrasia hata ya kuruhusu watu kujitokeza na kugombea urais ili wanachama wafanye maamuzi, kama mtu amefanya vizuri kwanini asishindanishwe na ambao hawajafanya chochote ili awashinde ndani ya chama demokrasia ichukue mkondo wake ,hizi kauli za utaratibu lazima Rais amalize mihura miwili sio demokrasia kabisa ,yaani mpaka wanasema mtu achukue fomu anaanzia wapi?
Maana yake ni kuwazuia wenye nia ya kugombea,hongera chama kikongwe.Kila siku huwa Ni Mbowe dikteta hataki kuachia uenyekiti ,hebu chama kikongwe onesheni mfano wa demokrasia ndani ya chama chenu tuone, demokrasia Ni kuiishi kwa vitendo sio maneno matupu.