Hivi CCM hamuoni aibu kwa haya?

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
1. Sungura textile....mmeua mkauza
2. Mwatex mmeua mkauza
3. Tipper mliua
4. Killitex mmeua...mkanywa
5. Bandari ...mmeuza
6. NBC...mmeuza mkala
7. TTCL...mmeuza mkala
8. General Tire...mmekula...ikafa
9. TRC...mmekula......mkauza
10. Urafiki textile....mmekula....mkauza
11. Loliondo...mmeuza ....mkala
12. EPA, kagoda.....CCM
13. Meremeta, Tangold....mmekula
14.
15.
16
.
.
.
.
 
14. Mashule yetu ya msingi na sekondari hawayajali kabisa
15. Rasilimali (dhahabu, almasi, Tanzanet n.k) zetu wamegawa bure kabisa!
16.
17.

Fisadi anaona aibu baba! yeye huweza hata kuua ili kujitajirisha kwa kutumia mbinu mbali mbali hata kama si za halali!


 
mwizi na fisadi ana sifa ya kutokuwa na aibu - hapo ni kumaliza chochote kilicho mbele yake - then waturudie sisi wananchi watupe mzigo mkubwa wa kodi ili kutumalizia kabisa.
 
Tatizo ni kuwa na viongozi wenye ufinyu wa elimu ambayo ni elimu ya UPE(Elimu Pasipo Elimu) na wenye tamaa za kijinga ndio maana tupo hapa tulipo.
 
Mshipa wa aibu wa CCM ulishakatika zamani kwao kashifa ni kama zeze
 
wenyewe wanasema wako katika juhudi za kuongeza ajira, kwa kua hayo mashirika/kampuni.
 
hahaaa nicheke mie as if yanafurahisha!

Kweli kabisa, mzima lakini? hahahahahaha nilioina avatar ikabidi niiangalie kwa muda kidogo ;). Avatar zingekuwa zinasema hahahahahahah! hii ingelalamika sana...LOL!

Tukirudi kwenye mjadala 99.9%ya matatizo ya nchi yetu yanasababishwa na CCM kuwepo madarakani.
 
Hivi mwenyekiti wa CCM unapotembea mitaani unajisikiaje pale unapokuta kila kona wananchi wanalia njaa na ni wachafu wa kupindukia?

Angalia pale UDSM ktk college of engineering majengo yote yanavuja mvua ikinyesha na tangu aondoke mjerumani aliyeyajenga hakuna hata kibanda kimoja kimeongezwa. Sasa wewe kama mwenyekiti wa CCM Taifa huwaulizi waliotawala pale miaka 20 waliendeleza nini?? Na kama pesa hukuwapa huoni aibu??

Lile li mlimani city kodi yake inaenda wapi??? Kwa nini msiongeze madarasa na mabweni pale UDSM?

Mzumbe University ndo hoi hata ofisi za walimu hakuna hao wanafunzi wanaosoma pale si watakuwa mafisadi nao kwa sababu mazingira yao ni magumu??
 
Kweli kabisa, mzima lakini? hahahahahaha nilioina avatar ikabidi niiangalie kwa muda kidogo ;). Avatar zingekuwa zinasema hahahahahahah! hii ingelalamika sana...LOL!

Tukirudi kwenye mjadala 99.9%ya matatizo ya nchi yetu yanasababishwa na CCM kuwepo madarakani.
hahaa inataka kulalamika lkn na yenyewe ni bubu!
mi cjambo,god has bin wonderful to me!
 
Ndo mana kila anaye jitoa ccm wanasema alikuwa mzigo kwa chama. Inavyoonekana wote ni mizigo na wanaogopa kutajana hadi mtu ahame chama. Tutaendelea kuongozwa na mizigo hadi lini. Walishashindwa kuongoza nchi hii siku nyingi. Mikataba wanayoingia na wawekezaji yote feki na wala hawajifunzi kutokana na makosa. Wao na dili za ulaji kila sehemu yenye kuweza kula inaliwa. Tubadilike sasa na kusema inatosha sasa!
 
Alafu wanawekana serikali kwa kujuana.....Nchi inateketea hivi hivi na sisi wananchi tunaona!!
 
Kipengele no.7 Kampuni hiyo chini ya wazalendo pamoja na matatizo yaliyokuwepo ilijipanga vizuri kutekeleza majukumu yake, wakasema no way ni lazima ibinafsishwe. Tangu imebinafsishwa ni matatizo ya utawala kila siku mara management contract mara celtel iwe kampuni kamili kutoka TTCL, ili mradi ubinafsishaji haukuwa na tija yoyote kwa taifa.

Mwisho kabisa malengo yao yametimia na kuanza kuona aibu wameamua kuirudisha serikalini, kinachowasumbua ni utata katika kugawana kilichopatikana wakati wa uendeshaji huu wa ki wizi. Tuendelee kusubiri labda neema yaja!!
 
Migodi Yooote, imeuzwa ....miji iliyong'ara kutokana na madini inadidimia.....fika Arusha, hakuna tena jeuri ya pesa za vijana wale.
 
Jamani hawa watu lazima tufanye kitu maana wamezidi sana,tufanye watu wetu waelewe ni kiasi gani inchi hii imekwisha.
 
Wana jamvi naomba msome report ya Mwadui katika gazeti la Raia Mwema ili muone hawa washenzi wanavyotufanya,pambaf zao!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom