mtanganyika tz
Member
- Dec 3, 2011
- 55
- 9
jamani nikinunuaa bundle ya net inaisha kama upepo! mpaka sielewi muhimu wake! bundle la mwezi linaisha siku moja! hapo nimesurf kidogo na wala sijadownload chochote! au voda ni wezi?:embarassed2:
Posible mkuu 50 MB ni kidogo mno huwezi ukatumia mwezi mzima. Hamia AIRTEL mkuu kwa sh 2500 utapata 400MB, Wengine wote wezi
sasa hii ya 400MB unaomba kama nini?datasiku or ina jina gani?
chakachua modem yako, uepuke kuyafaidisha makampuni ya matapeli
Badala ya bundle nunua Bomba, nami niliwahi kuwa kwenye maumivu kama yako lakini sasa naenjoy. Kwa mfano Bomba 30 ambayo ndio huwa naitumia unapata 2gb, zikiisha kabla ya mwezi unakuwa unasurf kwa 64kb mpaka tarehe igote (bomba 30 ni tsh 30,000). Wakati kununua bundle ya 2gb inaweza kuwa zaidi ya laki, jaribu bomba unaweza kuipenda.jamani nikinunuaa bundle ya net inaisha kama upepo! mpaka sielewi muhimu wake! bundle la mwezi linaisha siku moja! hapo nimesurf kidogo na wala sijadownload chochote! au voda ni wezi?:embarassed2:
Da! Kumbe tunaotumia Blacberry tunatesa
Cha kufanya ni rahisi, weka vocha yako ya elfu 30 kama unataka bomba 30, au kama unataka bomba 7 weka vocha elfu 10. Baada ya hapo nenda kwenye msg andika bomba 30 toka kwenda #15300, utapata msg kukujulisha kuwa umeshaingizwa kwenye mpango wa bomba na kupewa tarehe ya mwisho wa matumizi. Watakupa pia maelezo kuwa una 2gb na ukizimaliza utaendelea kutumia hadi mwisho wa tarehe yako lakini kwa speed ya 64kbps.mkuu hiyo term "bomba" naona kama siipati vizuri! kama ntakusumbua nisamehe ila naomba unielezee kwa kina!!
Ndugu yangu usimkatishe tamaa mwenzio, mimi huo natazama elp kupitia premiumtv na natumia modem ya voda. Natumia bomba 30 na huwa naweza kufika mpaka karibu tar 20 nikiwa bado sijamaliza 2gb nilizopewa. Inaweza kumsaidia.Kiukweli mpaka sasa hatuna mtandao ambao ni cheap na uhakika katika maeneo yote ya nchi. Inawezekana tu endapo matumizi yako ni ku surf tu pages za kawaida ambapo kwa wastani hautazidi 20MB/day. Ikiwa ni hivi mitandao yote itakufaa, ila ktk maeneo kadhaa tu. Kwa mfano Airtel ambayo unatumia Tsh2500/400MB ina speed nzuri katika maeneo ambapo utatumia WCDMA lakini kuana maeneo mengi tu mikoani ambapo inatumika EDGE tu ambayo speed yale inaload slow kupita maelezo. Lakini hata hivyo 400MB sio kitu kwa mtumiaji mkubwa wa internet works.
Sina hakika na tigo, maana inasemekana speed yake ni nzuri kwa wale wanaokaa Dar, ila huku mikoani tunatumia EDGE ambayo kiukweli iko slow kupindukia.
Vodacom speed yake ni nzuri kutegemeana na bundle unayotumia. Ukinunua 20MB/500tsh ni sawa ila haina matumizi mengine zaidi ya kusurf pages tu kwenye fb, emails etc kitu ambacho kwa mtumiaji mzuri wa internet hawezi kukifikiria. Tukisema ununue bundles kubwa ni very expensive. Dial: *149*01# uangalie bei na ukubwa wa bundle kisa ujipime mwenyewe. Kuna utumbo mwingine wanaita Unlimited ambao wanasema wamekusudia kwa watumiaji wakuwa na wastani binafsi sioni unafuu wake. Kwa mfano unlimited ya wiki moja ni Tsh 10,000/= ambapo unapata 750MB @ max. speed, wanasema zikishaisha hizo 750MB unakuwa unatumia 64kb/sec. Lakini kiukweli speed huwa inashuka sana,japo itakuwa inaonesha kwenye panel hadi 220kb/sec lkn uanapokuwa unatumia speed inakuwa haiendani na kilichoandikwa kwenye panel. Kwa maana nyingine ni kama umenunua 750MB/10,000tsh coz baada ya hapo kinachofuata ni utumbo mtupu.
Zantel speed yake ipo juu, ila nahisi it is the most expensive package. Minimum ni 250MB/6000tsh/day na max. ni 10GB/270,000TSH. Ukijaribu kulinganisha na Airtel unaona kabisa haiwezekani.
TTCL (Prepaid) speed yake ni nzuri ila ukitaka kununua bundle utakimbia mwenyewe. Kuna baadhi ya maeneo kama Dar unawezatumia unlimited kwa tsh1000/saa, so inategemea wewe kama umeridhika na rate hiyo, fine. Ila kuna wale wanaotumia broadband(postpaid) sijawahi kutumia so siwezi kucomment, watusaidie waliowahi kutumia.
Sasatel haipo mikoani. So sijaitumia.
Kuna wale wanaotumia LAN, hizi zinazotumia madish unless umeunganishwa na mkongo wa taifa, speed yake sio nzuri sana. Hata mimi nategemea zaidi modem, coz ofisini kuna LAN ambayo kwenye panel inaonesha 100Mb/sec lakini unapokuwa unatumia it's an extraordinary slow.
So kwa mahesabu hayo hapo juu, huwezi kutegemea mitandao yetu hii kutumia internet kama vile kuangalia live tv programs kama football, news channels, kudownload movies. Speed inaweza kuwa nzuri, ila huo mkwanja wake baba...!!
Ndugu yangu usimkatishe tamaa mwenzio, mimi huo natazama elp kupitia premiumtv na natumia modem ya voda. Natumia bomba 30 na huwa naweza kufika mpaka karibu tar 20 nikiwa bado sijamaliza 2gb nilizopewa. Inaweza kumsaidia.
jamani nikinunuaa bundle ya net inaisha kama upepo! mpaka sielewi muhimu wake! bundle la mwezi linaisha siku moja! hapo nimesurf kidogo na wala sijadownload chochote! au voda ni wezi?:embarassed2: