Hivi bila kuwapo shetani Dini na Mungu zingekuwapo?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720
1686968924060.png


Dini zote nyemelezi zinatuaminisha kuwa Mungu aliumba kila kitu zikiwemo dhambi, shetani, kifo na mabaya yote. Je kwanini Mungu aliumba shetani kama lao siyo moja?

Je bila shetani, dini na Mungu vingekuwa na mashiko au pa kujificha? Je shetani ni nani? Je ni mbaya kama tunavyoaminishwa? Yeye na aliyemuumba nani mbaya?

Je kwanini Mungu alimpa shetani mamlaka ya 'kupotosha' watu? Je kwanini shetani hashughuliki na wanyama?

Je shetani na binadamu nani aliumbwa kwanza na mwisho na kwanini? Tunaaminishwa kuwa Mungu anajua kila kitu hata ambacho hakijatendeka?

Kama alijua shetani angekuja kuwa mbaya, kwanza, aliumba wa nini, na pilil, kwanini alimkasirikia na kumlaani kama ni kweli wakati alipaswa kujua ambavyo angetokea kuwa?

Je kwanini Mungu ni mbaguzi? Rejea shetani anavyoonyeshwa akiwa mweusi au weusi unavyoonyesha ubaya kwenye dini zote nyemelezi hata lugha za kigeni.

Kwanini vitabu vya 'Mungu' viliandikwa na kutetewa na wanadamu? Leo ukimtukana mfano, Mungu, utaasomewa fatwa kana kwamba Mungu ni kichanga asiyejua umemtukana.

Kwanini wahusika wasimuache Mungu ajitetee mwenyewe? Zipo dini zinajiita dini za Mungu. Ajabu ya maajabu zinatetewa na binadamu tena kwa ukatili na pofu. Osama, yule habithi wa kiarabu aliwachochea watu wamfie Allah wakati yeye akiishi kwa kujificha uvunguni mwa kitanda.

Kwanini hakujiweka mstari wa mbele ili ampiganie Allah wake na mwishowe aende janna au peponi kama kweli aliamini aliyohubiri?

Kwanini Mungu wa dini nyemelezi alipenda kuonekana milimani, kwenye mapango na majabari sawa na waswahili walivyokuwa wakiamini lakini wakaaminshwa kuwa dini zao ni za kishenzi?

Je kumtoa kafara mtu au kupiga mawe mnara aka shetani au kuchungulia na kubusu jiwe siyo ushenzi? Je kusujudu kuelekea makka siyo ushirikina? Je kunywa damu ya mtu siyo umumiani?

Waafrika tulizoea kunywa ulabu na kutoa kafara na sadaka vya wanyama. Wenzetu wanatoana wao kwa wao tena kwa kusulubishana. Leo wanatuaminisha kuwa pombe ni haramu lakini hapo hapo wanatuahidi pombe peponi!

Wanatufundisha kuomba na kula mikate na tende kana kwamba mazao yetu ni haramu!

Wanatufundisha kuchamba kana kwamba ndiyo waliotufundisha kunyaaa!

Wanatubatiza na kutusilimisha bila kujua waliotuzaa ni washenzi hao hao! Je wanaweza kuchuja damu ya hao washenzi lau tutakate? Je Mungu na shetani lao siyo moja? Je hii siyo karata tatu ya kiimani?

Sitaki kusema mengi japo nina mengi kuepuka kuwachosha. Nangoja kusikia elimu yenu wanangu.

Ni baba yenu wote
 
Haya ni maswali ya watu waliopigwa na maisha,wanatafuta visingizio
Wewe kwa mfano unauliza ,kwanini alimuumba shetani wakati akijua ataleta balaa. kwa akili yako nani atajibu hili swali zaidi ya huyo muumba mwenyewe?
jitahidi tu kufuata mafundisho yaliyopo, hayo maswali yako utamuuliza ukifika mbinguni

Kumbukumbu 29:29​

Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.
 
Bila Mungu we ungekuwepo,au unajitoa ufahamu?. God is the source of everything.
 
Haya ni maswali ya watu waliopigwa na maisha,wanatafuta visingizio
Wewe kwa mfano unauliza ,kwanini alimuumba shetani wakati akijua ataleta balaa. kwa akili yako nani atajibu hili swali zaidi ya huyo muumba mwenyewe?
jitahidi tu kufuata mafundisho yaliyopo, hayo maswali yako utamuuliza ukifika mbinguni

Kumbukumbu 29:29​

Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.
Good!
 
Back
Top Bottom