Hivi battle ya Rais wa Kenya, William Ruto na aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua kwa hapa Tanzania tunaweza kuwapa kina nani?

Hivi battle ya Rais wa Kenya, William Ruto na aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua kwa hapa Tanzania tunaweza kuwapa kina nani?

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Wakuu,

Nimeona battle inayoendelea kati ya Rais wa Kenya na aliyekuwa Naibu Rais wake Rigathi Gachagua ambapo kwa Tanzania nafasi yake ni sawa na Makamu wa Rais.

Gachagua alichagulia kuwa Naibu Rais Agosti 2022 lakini Oktoba 2024 aliondolewa madarakani akikabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo kutomtii rais, kuchochea vurugu za kikabila, rushwa, kuidhoofisha serikali na utakatishaji fedha, miongoni mwa mengineyo ambayo yeye aliyakana

Hawa jamaa hivi karibuni wamekuwa wakirushiana maneno ya kashfa wazi kabisa kwenye mikutano yao ya hadhara na wananchi, mbaya zaidi ni kama kila mtu anajua michezo na uchafu wa mwenzie.

Kauli aliyotoa Ruto jana alimtuhumu Gachagua ni kwamba jamaa aliwahi kumpa mimba binti mdogo na kumuua



Gachagua naye alijibu kwa kumshambulia Ruto kwa maneno machafu



Nikajiuliza, hivi kwa Malawi hii ya kina Abduli hii battle inaweza kutokea kati ya nani na nani, au nani ni Ruto na nani ni Gachagua huku Malawi
 
Back
Top Bottom