Hivi baadhi ya Viongozi wetu huwa wanasimamia kitu gani?! Au ni bendera fuata upepo tu ili mradi mkono uende kinywani!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Suala la kusitishwa kwa mradi wa Bagamoyo almaarufu Bandari ya Bagamoyo ni suala muhimu linalohitaji maelezo ya kina!

Nimesoma maelezo ya Mhe.Zitto Kabwe, ameeleza kwa upana japo kuna mengine sikubaliani naye kabisa!
Mfano Mhe.Zitto haelezi details za makubaliano namna ambavyo Serikali yetu itapata mapato direct kutokana na hizo Meli kubwa za 4th Generation .

Pili Mhe.Zitto haelezi kama Bandari hiyo ya Bagamoyo itahudumia Meli aina zote au la,na kama itahudumia Meli aina zote basi Serikali yetu iko makini sana kwani China/Omani watavuta mizigo yote kwenye Bandari "YAO" ya Bagamoyo kwa muda wote wa mkataba na hivyo kuuwa kabisa Bandari ya Dar es Salaam na Serikali itakosa hata kile kidogo ambacho kwa sasa tunapata kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Tatu Mhe.Zitto hayuko sahihi kabisa kusema kuwa mapato ya PAYE ya waajiriwa 20,000 yatakuwa makubwa kuliko mapato yote yapatikanayo kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Mwisho na ndio msingi wa hoja yangu, nimemsikiliza vizuri Mhe.Spika Job Ndugai akielezea namna mradi huu ni kosa kubwa kwa Serikali kuuacha,na wakati akieleza nimeona Waziri mwenye dhamana Mhe. Issack Kamwelwe akipiga makofi! Waziri anaashiria nini kupitia makofi yake?!

Je,Waziri anakiri kuwa Serikali imefanya makosa kuuacha mradi huu kwa mujibu wa Spika Ndugai?

Je,Waziri anakiri kuwa Serikali imefanya makosa kuanza na ujenzi wa SGR kabla ya Bandari kwa mujibu wa Spika Ndugai?!

Kama ndivyo Waziri Kamwelwe anasubiri nini kujiuzulu kutoka katika Serikali ya Rais Magufuli?!
 
Back
Top Bottom